ODM YAJIANDAA BILA ODINGA

Kamati kuu ya usimamizi wa chama cha ODM imeratibu kikao maalum hii leo kujadili mustakabali wa chama hicho kufuatia kifo cha aliyekuwa kinara wake Raila Odinga. Mkutano huo utakaongozwa na kaimu kinara wa chama hicho Oburu Odinga, utafanyika katika makao makuu ya Orange House jijini Nairobi. Inatarajiwa kwamba wajumbe wa kitaifa wa ODM watamwidhinisha Oburu […]

PVK YAPINGA MSWADA WA MAKANISA 2024

Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya PVK umepinga mswada wa kudhibiti mashirika ya kidini wa mwaka 2024 uliopendekezwa na serikali, ambao kwa sasa uko katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi. Chini ya mwenyekiti wake Apostle Peter Manyuru ambaye pia ni kiongozi wa kanisa la JTM, muungano huo umeibua hofu kuhusiana na vipengee kadhaa […]

SERIKALI YATOA MALIPO YA INUA JAMII

Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 880,040,000 kama malipo kwa familia zilizo chini ya mpango wa Inua Jamii ambao ni mayatima na watu wengine walio na uhitaji wa hali ya juu. Kupitia taraifa ya wizara ya jinsia na huduma za Watoto, malipo hayo ni ya mwezi wa Septemba, kila anayelangwa akiratibiwa kupokea shilingi 2,000. Malipo […]

NYOKABI MIONGONI MWA WANAOLENGA KUWA MAJAJI

Tume ya huduma za mahakama JSC imewaorodhesha watu 100 atakaohojiwa kujaza nafasi za majaji 20 wa mahakama kuu, akiwemo aliyekuwa mwakilishi wa kike kaunti ya Nyeri Priscilla Nyokabi. Kupitia notisi, JSC imesema ilipokea maombi 377 kufuatia angazo ililochapisha kabla ya kuwateua 100 hao. Miongoni mwa walioorodheshwa na majaji wa mahakama za chini wanaolenga kupandishwa ngazi, […]

FOREST YAWAFUNIKA PORTO, VILLA YAFUNZWA

Klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Porto ya Ureno katika mechi za kuwania ubingwa UEFA UROPA na kumpa meneja Sean Dyche ushindi katika mechi ya kwanza baada ya kuteueliwa. Forest ambao alimpiga kalamu kocha wake Ange Postecoglou baada ya siku 40 pekee akiwa amewaongoza katika […]

SIKU YA STARLETS UGANI NYAYO

Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets ina imani kwamba itashinda mechi yao dhidi ya Gambia hii leo katika uwanja wa Nyayo katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika ya wanawake WAFCON.  Mlinda lango wa timu hiyo Lilian Awuor amesema  timu hiyo ina uwezo wa kukabiliana na Gambia akisema mechi hiyo ya leo ni fursa  kwa […]

WANARIADHA WA DEAFLYMPICS WAKAMILISHA WARSHA YA PUFYA

Wanariadha waliochaguliwa kuwakilisha kenya katika mashindano ya riadha ya wanariadha wal;io na changamoto za kusikia yaani Deaflympics jijni Tokyo  mwezi ujao pamoja na voingozi wao wamkamilisha warsha ya siku 4 kuhusu matumizi ya pufya ama dawa za kutitimua misuli. Warsha hiyo iliyoendeshwa na shirika la kukabiliana na dawa hizo ADAK kwa ushirikiano na wizara ya michezo inalenga kuhakikisha wanariadha wa Kenya wanashindana kwa mujibu wa mwongozo […]

SENETI YAWATAKA MCAS MAKUENI KUIWAJIBISHA SERIKALI

Kamati ya afya katika bunge la seneti imelitaka bunge la kaunti ya Makueni kuiweka mbioni serikali ya kaunti hiyo ili kuimarisha utoaji wa huduma za kiafya kwa Wakazi wa kaunti hiyo. Hii ni baada ya kamati hiyo kuzuru hospitali kadhaa za kaunti hiyo ikiwemo ile ya rufaa mjini Wote na kubaini ilichotaja kama uendeshaji mbaya […]

RUTO ATETEA SHERIA ZA MITANDAO

Rais William Ruto ametetea sheria za kudhibiti utumizi wa mitandao ya kijamii alizoidhinisha, akiwaonya wakenya anaosema wanaeneza uvumi kuhusu sheria hizo. Kulingana na Rais, sheria hizo zinalenga kudhibiti ugaidi, mahubiri potovu na ukiukaji wa maadili ya jamii, huku akijitetea kutokana na uamuzi wake wa kutia Saini sheria hizo wakati taifa lilikuwa kwenye maombolezo ya Waziri […]

MAHAKAMA UGANDA YATUPILIA MBALI KESI KUHUSU WANAHARAKATI

Familia za wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo zimepata pigo kutokana na uamuzi wa mahakama kuu nchini Ugandan kutupilia mbali kesi iliyoitaka mahakama kuvishurutisha vyombo vya usalama nchini humo kuweka wazi waliko wanaharakati hao. Kwenye uamuzi wake, jaji Simon Peter Kinube amesema idara ya polisi na jeshi la ulinzi nchini humo walitii maagizo ya mahakama […]