CA YAPUUZA MADAI YA KULAZIMISHA UKUSANYAJI WA DATA

Mamlaka ya mawasiliano nchini imepuuzilia mbali madai ya mamlaka hiyo kuwalazimisha wahudumu wa mtandao wa simu kukusanya data ya kibayometriki chini ya kanuni mpya za usajili za kadi za simu zilizorekebishwa nchini. Katika taarifa iliyotolewa hii leo mdhibiti ametaja wasiwasi huo kuwa usio na msingi. Mamalaka hiyo imefafanua kuwa sheria zilizosasishwa na kuchapishwa mnamo  mei 2025 zinalenga kuwalinda wakenya dhidi ya ulaghai unaohusiana na kadi za simu, wizi wa vitambulisho,   na […]

WAITITU APATA MDHAMINI KATIKA KESI YAKE

Huenda aliyekuwa gavana wa kiambu Ferdinand   Waititu akaachiliwa baada ya kupata mdhamini wa benki katika kesi inayomkabili ya ufisadi. Kupitia wakili wake waititu amesema kuwa  amepata  . Dhamana ya benki ya shillingi milioni 53, hitaji muhimu katika azma yake ya kutaka kuachiliwa huru. Imetayarishwa na Jones Koikai

KINYANG’ANYIRO CHA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA ULAYA

Kampeni ya kuwania tiketi za moja kwa moja za kufuzu kombe la dunia kwa bara Ulaya inatamatika leo usiku kwa mechi kadhaa ambazo zimeratibiwa kusakatwa katika nyuga mbali mbali. Ubelgiji walio na pointi 15, 2 mbele ya North Macedonia, watahitaji ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Liechtenstein, nao North Macedonia watalenga kupata ushindi […]

HARAMBEE STARS KUJITATHMINI DHIDI YA SENEGAL

Timu ya taifa Harambee Stars itaendeleza safari yake ya kujiimarisha dhidi ya Senegal leo jioni katika mechi yake ya mwisho ya kirafiki katika kipindi cha likizo ya kimataifa itakayochezwa nchini Uturuki. Timu zote zinakutana kufuatia kichapo kwenye mechi zao za kirafiki za kwanza, Stars wakibamizwa 1-0 na Equatorial Guinea huku Senegal wakimenywa na Brazil 2 […]

JUNIOR STARS WAANZA KAMPENI YA AFCON

Timu ya taifa ya soka ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars wataanza safari yao ya kufuzu mashindano ya AFCON U17 ukanda wa CECAFA dhidi ya Somalia hii leo, wakilenga kuibuka na ushindi katika mechi yao ya ufunguzi nchini Ethiopia. Stars wamewekwa kwenye kundi A Pamoja na wenyeji Ethiopia, Rwanda, South Sudan na […]

THUNDER WALENGA KUNGURUMA BAL ELITE 16

Klabu ya Nairobi City Thunder inaanza kampeni yake katika michuano ya BAL Elite 16 Kanda ya Mashariki leo, ikiwa na matumaini ya kurejea katika hatua ya juu zaidi ya mpira wa vikapu barani Afrika. Thunder itashuka katika uga wa michezo ya ndani uwanjani Kasarani kuvaana na Namuwongo Blazers wa Uganda, ambao waliingia kwenye hatua hii baada ya kumaliza nafasi […]

TAREHE YA KESI YA OJWANG YAPANGWA 

Kesi ya mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang aliyeuawa katika kituo cha Central Police jijini Nairobi itaanza kusikilizwa tarehe 12 Januari mwaka ujao, upande wa mashtaka ukitegemea ushahidi kutoka kwenye kanda ya CCTV kuthibitisha kesi dhidi ya washukiwa. Miongoni mwa washtakiwa kwenye kesi hiyo ni aliyekuwa OCS wa kituo hicho Samson Taalam na maafisa […]

FAMILIA YA OGUTU YALILIA HAKI, YALAUMU UBALOZI

Familia ya mkenya John Ogutu aliyeuawa kwenye ghasia za uchaguzi nchini Tanzania imeitaka serikali ya Kenya kuingilia kati ili kuurejesha nchini mwili wa jamaa yao ambao haujulikani uliko kufikia sasa. Kwenye kikao na wanahabari, familia hiyo imelalamikia kukosa msaada kwenye idara husika ukiwemo ubalozi wa Tanzania humu nchini, wanaosema umekosa kutoa maelezo kuhusu hatma ya […]

MAKURUTU WA POLISI KUANZA MAFUNZO

Jumla ya vijana 10,000 kote nchini waliofaulu kujiunga na idara ya polisi kwenye usajili wa hapo jana wameratibiwa kuanza mafunzo yao hivi karibuni kwa lengo la kuimarisha usalama wa taifa. Kulingana na Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, naibu wake Eliud Lagat na mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI Mohammed Amin, vijana hao watajaza si […]

SERIKALI YACHUNGUZA UDUKUZI DHIDI YAKE

Serikali inaendeleza uchunguzi katika tukio la udukuzi dhidi ya tovuti za wizara za maji, usalama, afya, leba na elimu na kuathiri kwa muda utoaji huduma kwa wananchi hapo jana. Katibu mkuu katika wizara ya usalama Raymond Omollo, amehusisha udukuzi huo na kundi la PCP@Kenya, akiutaja udukuzi huo kuwa uvunjaji wa sheria. Udukuzi wa hivi punde […]