MHOLANZI ALIYEMSHAMBULIA POLISI AACHILIWA

Raia wa Uholanzi Elwin Ter Horst aliyekamatwa wiki 2 zilizopita kwa makosa ya kumshambulia afisa wa polisi katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, ameachiwa bila masharti yoyote baada ya mahakama kubaini kuwa ana matatizo ya msongo wa mawazo yaani bipola na hivyo hawezi kujibu mashtaka. Hakimu mwandamizi Joy Mutimba, ametoa uamuzi huo baada ya […]

UFARANSA WATINGA KOMBE LA DUNIA, NORWAY NA URENO ZIKISUBIRI

Timu ya taifa ya soka ya Ufaransa imetinga kipute cha kombe la dunia kitakachoandaliwa mwaka ujao, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ukraine jana usiku, mechi iliyosakatwa wakati Ufaransa ikiadhimisha miaka 10 tangu shambulizi la kigaidi la mwaka 2015. Mechi hiyo iliyojawa na hisia za ukumbusho iliandaliwa katika uwanja wa Parc des Princes, mabao […]

EAGLES WA NIGERIA WAPAA HADI FAINALI

Timu ya taifa ya soka ya Nigeria maarufu kama Super eagles itapapurana kucha na Leopards wa DR Congo kwenye fainali ya kusaka tiketi ya kushiriki mwondoano dhidi ya timu kutoka mabara mengine, kwenye safari ya kuelekea kwenye kipute cha kombe la dunia mwaka ujao. Mabao 2 ya mshambulizi wa Galatasaray Victor Osimhen katika muda wa […]

VIKOSI VYA AWALI VYA DEAFLYMPICS VYAONDOKA NCHINI

Vikosi vya mchezo wa handiboli na vikapu vimeondoka nchini kuelekea Japan kwa mashindano ya wanamichezo wasio na uwezo wa kusikia ya Deaflympics yatakayoandaliwa jijini Tokyo kuanzia kesho. Timu ya handiboli ya wanaume iliondoka jana asubuhi huku ile ya wanawake ya vikapu ikiondoka kwa awamu 2, mchana na jioni. Manahodha wa vikosi vyote wameelezea matumaini ya […]

EACC: VUNJILIA MBALI TRAFIKI FISADI

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imependekeza kuvunjiliwa mbali kwa kitengo cha trafiki katika idara ya polisi kutokana na ufisadi ambao umefanywa kuwa desturi katika kitengo hicho. Kwenye ripoti yake, EACC imesema ukaguzi uliofanywa kati ya Februari na Juni mwaka huu unaonyesha kitengo hicho ndicho kilichooza zaidi, waathiriwa wakubwa wakiwa wamiliki wa magari, wahudumu […]

MAGAVANA WAONYA AKINA MAMA WANAJIFUNGULIA NYUMBANI

Hatua ya wizara ya afya kusitisha ufadhili kwa huduma za uzazi katika hospitali za level 2 na zahanati imewaweka hatarini akina mama wanaojifungua katika maeneo ya mashinani, idadi ya wanaojifungua hospitalini sasa ikiripotiwa kupungua. Haya ni kwa mujibu wa magavana wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Pamoja wa uangalizi wa huduma za kujifungua, wakihofia […]

UBINAFSI WA JAMII KUBWA WAFICHULIWA

Jamii 5 kuu nchini ambazo ni Kamba, Luhya, Kikuyu, Luo na Kalenjin zinashikilia zaidi ya asilimia 70 ya ajira katika mashirika ya umma nchini, hofu ikiibuliwa kuhusu kusambaratika kwa mshikamano wa kitaifa kutokana na mwenendo huo. Katika ripoti ya ukaguzi, tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imesema kwa Pamoja na jamii za Gusii, […]

RUTO ATOA HATIMILIKI 15000 KITUI

Rais William Ruto leo ametoa hati miliki 15,000 kwa wakazi wa Kamuwongo, Mwingi kaskazini, kaunti ya Kitui, akizungumza katika hafla hiyo rais Ruto ameangazia uwezekano wa mabadiliko ya mpango katika hatua inayolenga kutatua changamoto za muda mrefu za umiliki wa ardhi . Imetayarishwa na Jones Koikai

WAZIRI RUKU AKASHIFU MADAI YA ALIYEKUWA NAIBU RAIS YA KUWAHUSISHA WASHIRIKA WAKE NA GHASIA ZA UCHAGUZI

Waziri wa utumishi wa umma,Geoffrey Ruku, amepuuza madai ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kuhusisha washirika wake na vitisho vya ghasia za uchaguzi.  Ruku amekashifu madai hayo kuwa matamshi ya chuki yanayochochewa kisiasa na yanayolenga kumharibia sifa zake. Hayo yanajiri  baada ya Gachagua kuandika barua akitaja kanda ya video ambapo watu watatu – Simon Njagi Njiru, Josiah Kariuki Ngari, na Susan […]

WAZIRI MKUU AONYA KUWA WAKENYA WALIO NA UJUZI WA MITANDAO YA MAGENDO KUWA TISHIO KWA TAIFA

Waziri Mkuu  Musalia Mudavadi ameonya kwamba baadhi ya Wakenya waliookolewa kutoka kwa mitandao ya magendo Kusini-mashariki mwa Asia sasa wanaweza kuwa tishio kwa usalama wa taifa. Mudavadi aMEsema serikali inazidi kuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya waathiriwa, ambao walipata mafunzo ya uhalifu wa mtandaoni wakiwa wamenaswa kutokana na  ulaghai wa mtandaoni, wanaweza kutumia ujuzi huo kuanzisha shughuli za ulaghai nchini Kenya. AMEsema […]