3K FC YALENGA KUENDELEZA REKODI NZURI DHIDI YA GUCHA STARS

Timu ya 3K FC inayoshiriki Ligi ya Daraja la Kwanza (NSL) inatarajiwakuendeleza kiwango chake kizuri inapowakaribisha Gucha Stars katikamzunguko wa tisa wa ligi hiyo kwenye uwanja wa Moi Stadium kauntiya EmbuKikosi hicho kutoka Embu kimeonyesha maboresho makubwaukilinganisha na msimu uliopita na kwa sasa kinashikilia nafasi ya tatukwenye msimamo kwa alama 15 baada ya mechi nane.Akizungumza […]

GHARAMA YA KUBADILI KENYA IWE SINGAPORE NI SH 5 TR, RUTO

Mpango kabambe wa Rais William Ruto wa kubadilisha Kenya hadi nchi ya kwanza ulimwenguni na kupigiwa mfano kama vile nchi za Singapore, Japan, Korea Kusini na Malaysia, utahitaji angalau Ksh.5 trilioni. Akizungumza wakati wa Hotuba ya Hali ya taifa Bungeni, Rais Ruto amefichua kuwa utawala wake utaweka vipaumbele vinne vya kugeuza mpango huo kuwa ukweli ambayo ni Pamoja […]

DROO YA UEFA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA YAKAMILIKA

Mabingwa mara 4 wa kombe la dunia Italia, watakabiliana na North Macedonia katika kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao kupitia mwondoano yaani playoff, baada ya kukosa tiketi ya moja kwa moja. Kwenye droo iliyofanyika hapo jana jijini Zurich, iwapo Italia watashinda mechi hiyo ya tarehe 26 mwezi Machi mwaka ujao, watamenyana na […]

ZARIKA ‘KUMSHUSHA BEI’ VUNJABEI KWENYE FEATHERWEIGHT

Bingwa wa zamani wa pigano la WBC Super bantamweight Fatuma Zarika ameratibiwa kudhihirisha ni kwanini akapewa jina la Mkono chuma ama Iron Fist atakapomenya na Mtanzania Halima Vunjabei katika pigano la Super Featherweight katika jumba la Masshouse eneo la Ngong Racecourse hii leo. Pigano hilo ambalo limeandaliwa kupitia ushirikiano wa tume ya wanamasumbwi nchini KPBC, […]

UBABE WA HANDIBOLI WATARAJIWA WIKENDI

Fataki zinatarajiwa katika ulingo wa mchezo wa handiboli nchini Jumapili hii wakati mabingwa watetezi wa ligi ya shirikisho la handiboli kwa wanaume National Cereals Board NCPB, watalenga kuzuia uharibifu wa nafaka yao kutoka kwa risasi za mahasimu wao wa jadi Ulinzi ugani Nyayo. Kocha mkuu wa NCPB Bryan Mathews ameelezea matumaini ya kuendeleza ubabe wao […]

AFUENI YA SARATANI

Wagonjwa wanaosaka matibabu ya saratani nchini wamepata afueni kufuatia hatua ya serikali kuongeza fedha inazolipia matibabu yao kutoka shilingi elfu 550 hadi elfu 800 kwa mwaka chini ya mpango wa afya ya jamii SHA. Kwenye hotuba yake kwa taifa kupitia bungeni, Rais William Ruto amesema malipo hayo yataanza kutolewa mwezi ujao, huku akitetea bima ya […]

WAATHIRIWA WA MAPOROMOKO CHESONGCH KUZIKWA LEO

Watu 31 walioangamia kwenye maporomoko ya ardhi katika eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet wameratibiwa kuzikwa hii leo katika kaburi la pamoja, huku wengine 4 wakizikwa na familia zao kwenye mashamba yao. Watu 32 zaidi wanaendelea kuuguza majeraha kutokana na maporomoko hayo huku wengine 9 wakikosa kujulikana waliko, na zaidi ya familia 600 zikiachwa […]

UPINZANI WADAI NJAMA YA KUWAHONGA WAPIGA KURA

Muungano wa upinzani umeibua madai kuhusu kuhongwa kwa wapiga kura katika maeneo yanayojiandaa kwa chaguzi ndogo wiki ijayo ambako wagombeaji wa upinzani wanamenyana na wenzao wanaoegemea serikali ya Kenya Kwanza. Katika kikao na wanahabari, muungano huo ukiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka umesema wapiga kura wameahidiwa hadi shilingi 5,000 iwapo watathibitisha kwamba wamewapigia kura […]

IEBC KUSAMBAZA VIFAA VYA UCHAGUZI

Maandalizi ya chaguzi ndogo za Alhamisi wiki ijayo yameingia hatua za mwisho, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikitarajiwa kuanza usambazaji wa vifaa vya kupiga kura kuelekea maeneo hayo hii leo. Kupitia taarifa, IEBC imesema miongoni mwa vifaa hivyo ni karatasi na masunduku ya kupigia kura, helikopta zikitumiwa kusafirisha vifaa hivyo katika maeneo yaliyo […]

Aviatrix’s Jackpot Potential: Cumulative Vs Fixed Prizes

When engaging yourself with Aviatrix’s jackpot’s choices, you’ll discover yourself considering the uncertain allure of cumulative jackpots against the steady certainty of stable rewards. Progressive jackpots, driven by collective player wagers, promise exhilarating increase and potential transformative wins. Conversely, fixed rewards offer a consistent payout, attracting those who favor measured risk. Understanding these dynamics can […]