NTSA YAWAONYA MADEREVA KUHUSU ULAGHAI

Mamlaka ya usalama barabarani NTSA imewatahadharisha madereva kuhusiana na kundi la wahalifu linalojifanya maafisa wa NTSA na kuitisha faini kupitia SMS kutoka kwa madereva kwa misingi kwamba madereva hao wamevunja sheria za trafiki. Kupitia notisi, NTSA imesema washukiwa wamekuwa wakituma tovuti kupitia SMS kuwaelekeza madereva namna ya kulipa faini zinazodaiwa. Mamlaka hiyo imejitenga na tovuti […]

AFCON YABISHA

Mashindano ya Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, AFCON, yanaanza rasmi Jumapili hii nchini Morocco, yakishirikisha mataifa 24 kutoka bara hili. Wenyeji Morocco, ambao ndio washindi wa AFCON mwaka 1976, wanalenga kukata kiu cha kusubiri taji hilo kwa zaidi ya miaka 40, wakilenga kutumia faida ya uwanja wa nyumbani watakapoanza kampeni yao kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Comoros. Mabingwa watetezi Ivory Coast, ambao wamewahi kushinda taji la AFCON mara tatu—mwaka […]

POLICE FC WATIWA PINGU

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya KPL Police FC walipoteza fursa ya kurejea kileleni mwa ligi baada ya kutiwa pingu zao, walipofungwa bao 1-0 na Murang’a Seal katika pambano la aina yake. Bao la Joe Waithira katika kipindi cha kwanza lilitosha kumaliza msururu wa mechi 5 bila ushindi kwa Murang’a Seal, mbali na kuwapa […]

KENYA YAJIONGEZEA MEDALI ANGOLA

Matineja wa Kenya wanaoshiriki michezo ya vijana wa Afrika mwaka huu nchini Angola wamevuna medali 6 zaidi na kufikisha jumla ya medali 23 katika michezo hiyo. Ushindi wa medali hizo za jana ulianzishwa na mwanamichezo chipukizi wa kunyanyua vyuma Amanda Lina, aliyeshinda nishani 2 za fedha na shaba 1 katika katika vipengele vya snatch and clean and jerk, akifikia […]

WAITITU, MKEWE MAHAKAMANI

Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye anatumikia kifungo cha miaka 12 gerezani kwa kosa la ufisadi unaohusisha shilingi milioni 588, anatarajiwa kufika mahakamani leo na mkewe Susan Wangari kuhusiana na kesi inayotaka mali yao kutwaliwa. Maagizo ya kufika mahakamani yalitolewa na jaji wa mahakama ya kupambana na ufisadi Nixon Sifuna, baada yao kukosa kufika […]

MARAGA: SINGAPORE GANI!

Jaji mkuu wa zamani David Maraga ameibua madai kwamba azma ya Rais William Ruto kubadilisha Kenya kuwa katika viwango vya mataifa yaliyoendelea kiuchumi duniani inalenga tu kuvutia ufadhili na hakuna lengo la kuafikia azma hiyo. Maraga amependekeza Rais kukomesha ufisadi katika serikali yake, akisema hilo litafanikisha kuokoa fedha zaidi za kuwekeza katika miradi ya maendeleo […]

RUTO AAGIZA UFADHILI WA MASOMO KWA “WACHACHE”

Azma ya watoto wanaotoka katika jamii za watu wachache kupata elimu imepigwa jeki baada ya Rais William Ruto kuagiza uzinduzi wa mpango wa kitaifa wa kila mwaka wa kufadhili masomo ya shule za upili na vyuo vya kadri kwa watoto hao. Rais amesema ufadhili huo unalenga kuwawezesha Watoto kutoka jamii hizo na zile zilizotengwa kupata […]

MGOGORO MPYA WANUKIA UON      

Huenda shughuli za masomo zikayumbishwa tena katika chuo kikuu cha Nairobi iwapo serikali haitatekeleza matakwa ya wahadhiri chuoni humo, ikiwemo kutia saini na kutekelezwa kwa mkataba wa maelewano wa pamoja CBA. Katika kikao na waandishi wa habari, wahadhiri kupitia muungano wa UASU wameilaumu serikali kutokana na kucheleweshwa kwa mkataba huo, na madai kwamba serikali inavuruga […]

LUIS SUÁREZ ASAINI MKATABA MPYA NA INTER MIAMI

Mshambuliaji wa zamani wa Uruguay Luis Suárez amesaini mkataba mpya na Inter Miamikwa msimu ujao, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) imethibitisha.Suárez, atakayefikisha umri wa miaka 39 mwezi Januari, alijiunga na kikosi cha Lionel Messimwaka 2024 na kusaidia Inter Miami kutwaa taji la MLS Cup pamoja na ubingwa wa EasternConference.Mshambuliaji huyo wa zamani […]

STELLAH WAFULA AREJEA KUIPA KENYA LIONESSES NGUVU

Kenya Lionesses wamepata nguvu kubwa baada ya kurejea kwa kiungo mahiri StellahWafula kuelekea mashindano ya HSBC Sevens Series 2026 yatakayochezwa Februari 14–15katika Uwanja wa Nyayo.Wafula alikosa ushindi wa Kenya wa 14–10 dhidi ya Uganda mwezi Oktoba, ushindiuliowawezesha Lionesses kurejea na taji la Safari Sevens. Pia hakuwemo Kenya ilipopotezafainali ya Africa Cup Sevens kwa kufungwa 22–0 […]