JAJI WA MAHAKAMA YA JUU AFARIKI

Idara ya utoaji haki imepata pigo kufuatia kifo cha jaji wa mahakama ya upeo Ibrahim Mohammed, aliyefariki jana alasiri baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kulingana na ripoti, jaji huyo alikuwa ameratibiwa kustaafu tarehe 1 mwezi ujao, baada ya kuhudumu katika idara ya mahakama kwa kipindi cha miaka 23. Kupitia taarifa, jaji Mkuu Martha Koome, […]

MAAFISA WA KLINIKI WATANGAZA MGOMO

Huenda wakenya wakatatizika kupata huduma za matibabu wakati wa sherehe za Krisimasi kutokana na mgomo wa maafisa wa kliniki KUCO, ambao wametishia kugoma kuanzia Jumanne wiki ijayo iwapo serikali haitatia saini mkataba wa maelewano wa kurejea kazini. Mwenyekiti wa KUCO Peterson Wacira, amemshtumu Waziri wa afya Aden Duale kwa kukosa kutia Saini mkataba huo walioafikiana […]

KCB WALENGA KUTETEA TENA TAJI LA KIPCHUMBA KARORI

Timu ya wanawake ya voliboli ya KCB imeelekeza macho yake katika kutetea taji laMashindano ya Kimataifa ya Kipchumba Karori yanayofanyika mjini Eldoret mwishoni mwawiki hii, ikilenga kudumisha ubabe wao katika anga ya voliboli ya ukanda wa AfrikaMashariki.Mashindano hayo yamepangwa kuanza Ijumaa, Disemba 19 hadi Jumapili, Disemba 22, nayanatarajiwa kuvutia klabu bora kutoka Kenya, Uganda na […]

KENYA YAANZA UTETEZI WA UBINGWA WA ROLL BALL KWA NGUVU DUBAI

Timu za taifa za Kenya za roll ball kwa wanaume na wanawake zimeanza kampeni yaokatika Kombe la Dunia la Roll Ball kwa kishindo kikubwa, zikionyesha wazi dhamira yakutetea ubingwa wao wa dunia mjini Dubai.Timu ya wanaume ya Kenya ilifungua mashindano kwa ushindi mnono wa mabao 18–0 dhidiya Poland, ikionyesha nidhamu ya hali ya juu na […]

KRU KUPANGA UPYA MUUNDO WA KENYA CUP ILI KUREJESHA USHINDANI

Muungano wa Raga Kenya (KRU) unapanga kufanya marekebisho makubwa ya mashindanoya Kenya Cup katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, hatua inayolenga kurejesha ushindanina kuvutia wadhamini zaidi wa kibiashara.Chini ya pendekezo jipya, ligi itagawanywa katika viwango viwili. Kiwango cha Kwanza(Tier One) kitakuwa na klabu sita bora, huku Kiwango cha Pili (Tier Two) kikijumuishaklabu sita za mwisho […]

KENYA YAIBUKA BINGWA WA JUMLA MICHEZO YA BUNGE YA EAC

Kenya imeibuka mshindi wa jumla wa toleo la 15 la Michezo ya Mabunge ya Jumuiya yaAfrika Mashariki (EAC) yaliyohitimishwa mjini Kampala, UgandaTimu ya Kenya iliongoza kwa jumla ya medali 20 zikiwemo dhahabu sita, fedha sita na shabanane, ikionyesha ubabe wake katika mashindano ya taaluma mbalimbali.Kenya ilitawala katika riadha, voliboli, kuvuta kamba, darts na gofu, huku […]

SHA KUGHARAMIA WAHUDUMU WA AFYA

Serikali kuu na zile za kaunti zimekubaliana kuwalipia wahudumu wakujitolea wa afya malipo ya sha bila na kuwakata chochote kwenye malipo yao kuanzia mwaka ujao.  kwa mujibu wa waziri wa afya Aden Duale, ngazi zote mbili za serikali zinatarajiwa kutoa  pesa nusu kwa nusu na kugharamia matibabu kamili ya wahudumu hawa wa afya wa nyanjani kwa mradi […]

WAKAAZI WA BUSIA KUTAFUTA MATIBABU YA NGOZI

Wito umetolewa kwa wananchi katika kaunti ya Busia walio na maradhi ya ngozi kutembelea vituo vya afya ili kufanyiwa ukaguzi wa kitaalam. Imebainika kuwa wanaougua maradhi hayo ikiwemo eczema hawatafuti matibabu hospitalini ipasavyo. Hata hivyo mapuuza ya kutafuta matibabu ya magonjwa ya ngozi hospitalini na badala yake kutumia madawa ya kienyeji hupelekea wakaazi kuathirika zaidi ugonjwa huo […]

EU YAPUNGUZA MIPANGO YA KUKOMESHA UUZAJI WA MAGARI YA PETROLI, DIZELI IFIKAPO 2035

Umoja wa Ulaya umepunguza mipango yake ya kupiga marufuku uuzaji wa magari mapya ya petroli na dizeli ifikapo mwaka 2035. Sheria za sasa zinasema kuwa magari mapya yanayouzwa kuanzia tarehe hiyo yanapaswa kuwa ya “kutotoa moshi”, lakini watengenezaji wa magari, hasa nchini Ujerumani, wamepinga hilo na kusubiria  nafasi ya mazungumzo. Kulingana na chama cha watengenezaji magari cha Uropa, ACEA, mahitaji ya […]

GEORGE KAMAL AMRITHI KILAVUKA KQ  

Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limemteua Kapteni George Kamal kama Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa na Afisa Mkuu Mtendaji kufuatia kuondoka kwa Allan Kilavuka ambaye muda wake wa kuhudumu ulikamilika. Katika taarifa yake, Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo la ndege imesema Kilavuka ataendelea na likizo ya mwisho kabla ya kumalizika kwa mkataba wake, kuashiria […]