EQUITY HAWKS WAJIAMINI LIGI YA MPIRA WA KIKAPU INAPOANZA

Msimu wa 2026 wa Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu kwa Wanawake nchini unaanza wikendi hii, huku kocha wa Equity Hawks, Benson Oluoch, akieleza imani kuwa kikosi chake kilichoboreshwa kitaanza kwa kishindo baada ya kukosa kufika fainali msimu uliopita. Oluoch amesema timu hiyo imejiandaa vyema na ina ari ya kuonyesha mabadiliko mapema katika msimu huu […]

NTSA YAONYA BODA BODA KUHUSU NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU

Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama Barabarani, (NTSA), imewataka waendeshaji wa boda boda kuacha kutumia njia za watembea kwa miguu na badala yake kufuata barabara zilizotengwa kwa magari. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa X NTSA imebainisha kuwa njia za watembea kwa miguu zinazidi kuwa nyembamba katika miji mingi kutokana na ongezeko la […]

UDA YAIMARISHA KAMPENI WEST KABRAS

Shughuli za kampeni zimepamba moto katika Wadi ya West Kabras, Kaunti ya Malava, huku viongozi wa chama cha UDA wakihamasisha uungwaji mkono kwa mgombea wao, Elphas Shalakha, kuelekea uchaguzi mdogo ujao. Msafara wa kampeni uliongozwa na msaidizi wa Rais Farouk Kibet, Naibu Gavana Ayub Savula pamoja na Mbunge wa Malava David Ndakwa. Viongozi hao walizunguka vituo […]

 SERIKALI YASISITIZA SHA INAFANYA KAZI

Serikali imethibitisha kuwa mpango wa Bima ya Afya ya Jamii, SHA, unaendelea kufanya kazi ipasavyo na kuwataka Wakenya kuendelea kujisajili ili kufaidika na huduma zake. Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, akizungumza katika Misheni ya Segera, Laikipia Kaskazini, alisema serikali imetenga fedha za kutosha kuhakikisha wanachama wote waliosajiliwa wanahudumiwa kikamilifu. Koskei alisisitiza kuwa huduma […]

KALONZO APINGA UHAMISHO WA MAJUKUMU YA NAIROBI

Kiongozi wa upinzani Kalonzo Musyoka amepinga vikali hatua ya kuhamisha majukumu ya Kaunti ya Nairobi kwa serikali kuu, akisema mchakato huo hauna uwazi na haujafanyika kwa mashauriano ya kutosha. Kalonzo amesema ugatuzi ni haki ya kikatiba ya wananchi na unapaswa kulindwa kwa gharama yoyote, akionya dhidi ya hatua zozote zinazoweza kudhoofisha mamlaka ya kaunti. Amesisitiza […]

POLISI WATIBUA NJAMA YA UGAIDI NAIROBI

Maafisa wa usalama nchini wamewekwa kwenye hali ya tahadhari baada ya idara ya polisi kutibua mpango wa shambulizi la kigaidi jijini Nairobi kufuatia operesheni ya kijasusi iliyowalenga watu wanaoaminika kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Shabaab lililoko nchini Somalia. Kwa mujibu wa idara ya polisi, NPS, operesheni hiyo ilikuwa kilele cha uchunguzi, ukaguzi […]

OBADO BADO AKANA

Gavana wa zamani wa Migori Okoth Obado, amekana kumwua aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Beryl Otieno, akiiomba mahakama kuu kumwachia huru kutokana na ukosefu wa ushahidi. Kwenye mawasilisho yake ya mwisho kupitia kwa wakili Kioko Kilukumi, Obado amehoji kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kumhusisha moja kwa moja na kifo cha Sharon, akisema kesi hiyo […]

SACCO ZATANGAZA NJIA ZA KUREJESHA FEDHA ZA KUSCO

Kikosi kazi kilichoteuliwa na Wizara ya Vyama vya Ushirika kimependekeza kwamba SACCOs zitenge sehemu ya ada zao za uanachama na bidhaa ili kusaidia kifedha Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (KUSCCO) unaotatizika. Kama ilivyoripotiwa, shirika hilo kuu, lililodhoofishwa na kashfa ya kifedha ya shilingi bilioni 13.3 iliyohusishwa na maafisa wa zamani na kushindwa […]

DHAHABU YA IKOLOMANI ITAWAFAIDI WAKAZI, BUNGE LAAHIDI

Bunge la kaunti ya Kakamega limewahakikishia wakazi wa eneo la Ikolomani kwamba litalinda maslahi yao wakati wa uchimbaji wa madini ya dhahabu ambao umeratibiwa kuanza hivi karibuni na mwekezaji wa kibinafsi. Spika wa bunge hilo James Namatsi, amekiri kuwa bunge hilo limepokea malalamishi ya wakazi walio na hofu ya kudhulimiwa wakati wa zoezi hilo ambalo […]

PETER WANYAMA AKUBALI MATOKEO LSK

Wakili Peter Wanyama amekubali matokeo ya uchaguzi wa chama cha wanasheria nchini LSK wa hapo jana ambapo alimaliza wa pili nyuma ya mshindi Charles Kanjama, ila akalalamikia alichokitaja kuwa kutojitolea kwa mawakili kushiriki uchaguzi huo. Wanyama ambaye alitangaza kuwania kiti hicho Septemba mwaka jana, amesisitiza kuwa uongozi unahiaji unyenyekevu katika kushinda na kushindwa. Amesema licha […]