STARLETS UFARANSA KWA MAZOEZI

Kikosi cha wanawake wa timu ya taifa ya soka Harambee Starlets kitacheza mechi 2 za kirafiki dhidi ya Benin na Ivory Coast, na kisha kufanya kambi ya mazoezi nchini Ufaransa. Haya ni katika maandalizi ya dimba la taifa bingwa barani Afrika kwa wanawake, WAFCON 2026, litakaloandaliwa mwezi ujao nchini Morocco. Rais wa shirikisho la soka […]

CHERUIYOT ATARAJIA MSIMU WA KISHINDO 2026

Mshindi wa medali ya fedha katika mbio za mita 1,500 kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, Timothy Cheruiyot, ana matumaini makubwa ya kuwa na msimu wa 2026 wa kishindo, huku akilenga kutawala jukwaa la dunia katika michezo ya Jumuiya ya Madola, mzunguko wa Diamond League na ubingwa wa Dunia wa Ultimate. Cheruiyot alitoa onyo yake ya kwanza Februari 14 katika mashindano ya Sirikwa Classic […]

VURUGU ZAWAACHA MAKUMI NA MAJERAHA KISII

Makumi ya watu wanaendelea kuuguza majeraha kufuatia makabiliano baina ya makundi mawili ya vijana katika maeneo ya Keroka na Kisii muda mfupi kabla ya viongozi wa upinzani kuandaa mikutano ya hadhara maeneo hayo hapo jana. Mikutano hiyo ilikuwa imeandaliwa na naibu kinara wa Jubilee Fred Matinag’i, ambaye amewalaumu polisi na wanasiasa wanaoegemea chama tawala cha […]

INGONGA AILAUMU DCI, IPOA KWA UCHUNGUZI

Huku waathiriwa wa ukatili wa polisi wakisubiri haki, imebainika kwamba idara ya upelelezi wa jinai, DCI, na mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi, IPOA, zimekosa kuwasilisha faili za uchunguzi kwa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ili kuwafungulia mashtaka polisi wanaodaiwa kukiuka sheria. Akizungumza jijini Nairobi alipokuwa akizindua mtaala kuhusu mashtaka ya ugaidi, mkurugenzi […]

KMPDU YATOA MAKATAA COAST GENERAL

Serikali ya kaunti ya Mombasa ina siku 7 kuchukua hatua na kumrejesha kazini afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya rufaa ya Coast General Daktari Iqbal Kandwalla la sivyo madkatari wasitishe huduma zao na kulemaza matibabu kwenye hostali hiyo. Kandwalla alisimamishwa kazi kwa madai ya utepetevu kazini unaohusishwa na kifo cha Ali Kibwana hospitalini humo, aliyekuwa […]

UPASUAJI WA MAITI WAFICHUA KIINI CHA KIFO MUKUMU

Imebainika kuwa mama mjamzito aliyefariki alipokuwa akijifungua katika hospitali ya kimisheni ya Mukumu kaunti ya Kakamega alifariki kutokana na majeraha na kuvunjika kwa viungo, familia ikishinikiza haki kutoka kwa hospitali hiyo. Kwa mujibu wa ripoti ya upasuaji, mwathiriwa kwa jina Grace Wambui Misiko, alivunjika viungo vya mwili zikiwemo mbavu na sehemu ya uzazi. Familia imesema […]

SERIKALI YASAMBAZA CHAKULA CHA MSAADA TURKANA

Zaidi ya wakazi 300,000 wanaokabiliwa na makali ya njaa kutokana na ukame katika kaunti ya Turkana wanatarajia kupata msaada wa chakula ambacho kimeanza kusambazwa na serikali kuu katika juhudi za kudhibiti makali ya njaa. Kwa mujibu wa Waziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku, serikali imetuma malori 21 yenye chakula hicho kikiwemo cha Watoto wachanga, […]

MAN UNITED KUTAFUTA USHINDI

Manchester United wataingia uwanjani hii leo kupambana na Everton katika mechi ambayo United watakua wakitafuta ushindi ili waweze kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Jedwali la Ligi kuu ya Uingereza. United ambao wamekua na matokeo mazuri baada ya Kocha Michael Carrick Kuchukua usukani watakua na kibarua kigumu ikikumbukwa kuwa walipoteza mechi ya mkondo […]

BARCELONA YAREJEA KILELENI MWA LA LIGA

Klabu ya FC Barcelona ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Levante  na kurejea kileleni mwa msimamo wa La Liga . Baada ya Real Madrid kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya  Osasuna , kikosi cha kocha Hansi Flick kilipanda kileleni kwa tofauti ya alama moja kufuatia ushindi huo uliopatikana katika uwanja wa Camp Nou. Marc […]

MURWA ANG’ARA DAYSTAR IKIICHAPA QUINS KENYA CUP

Kocha mkuu Caleb Bosire amempongeza kwa dhati mchezaji wa nafasi ya flyhalf, Paul Murwa, baada ya kuiongoza Daystar University Falcons kuibuka na ushindi wa alama 30-23 dhidi ya Kenya Harlequin  katika mechi muhimu ya Kenya Cup iliyochezwa Jumamosi. Murwa, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, alionyesha utulivu mkubwa na kufunga alama 15 kupitia penalti tatu na mabadiliko matatu, hatua iliyodumisha matumaini ya Daystar kufuzu […]