MADEREVA 18 WA KENYA KUSHIRIKI SAFARI RALLY NAIVASHA

Madereva 18 wa Kenya na wasaidizi wao 14 watakuwa miongoni mwa magari 46 yatakayoshiriki katika mashindano ya WRC Safari Rally Kenya, yatakayofanyika kuanzia Machi 12 hadi 15 mjini Naivasha. Mashindano hayo pia yatakuwa duru ya kwanza ya Kenya National Rally Championship. Safari Rally ya mwaka huu itakuwa duru ya tatu kati ya 14 za mfululizo wa World Rally Championship, […]

KOCHA WA TUSKER AKIRI UBINGWA UMEWAPONYOKA

Kocha mpya wa Tusker FC, Julien Mette, amekiri kuwa timu hiyo haina tena nafasi ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa msimu huu. Mette amesema sasa wataelekeza juhudi katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi, pamoja na kuwania kombe la mashindano ya ndani. Licha ya kupoteza kwa bao 1-0 […]

OMOLLO AONYA VIONGOZI DHIDI YA KUCHOCHEA GHASIA MIGORI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, ameonya viongozi wa kisiasa katika Kaunti ya Migori na maeneo mengine nchini dhidi ya kuwatumia vijana kuchochea ghasia. Akizungumza katika eneo la Suna Magharibi Omollo amesema serikali haitaruhusu wanasiasa kutumia vurugu kuwatisha wapinzani au kuvuruga shughuli za kisiasa. Omollo aidha amewataka viongozi wa Migori kukumbatia siasa za amani, akionya kuwa […]

GAVANA WAMATANGI AFIKA MBELE YA KAMATI YA SENETI

Gavana wa Kaunti ya Kiambu Kimani Wamatangi, amefika mbele ya Kamati ya Uhasibu ya Bunge la Seneti kujibu maswali kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 17. Wamatangi ametakiwa kueleza kwa kina jinsi fedha hizo zilivyotumika katika kaunti hiyo. Hata hivyo, kikao cha leo kimeahirishwa ili kutoa nafasi ya maandalizi bora kabla ya kuendelea na usikilizaji wa hoja hiyo. […]

RAIS APUUZA UKOSOAJI WA UPINZANI

Rais William Ruto amepuuza shutuma kutoka kwa viongozi wa upinzani wanaomkosoa kwa madai ya kukosa kuwajibika kwa Wakenya. Rais amesema rekodi yake ya maendeleo inajieleza, akitaja miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini kama ushahidi wa utendaji wa serikali yake. Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

EACC YAWAKAMATA MAAFISA 3 GARISSA 

Mwakilishi wa wadi kutoka kaunti ya Garissa ni miongoni mwa maafisa 3 wa kaunti hiyo wanaoendelea kuhojiwa na tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC baada ya kuwakamata kuhusiana na madai ulipaji wa shilingi milioni 51.5 kwa njia za udanganyifu. Washukiwa ni mwakilishi wadi huyo wa Balamabala Abdi Ibrahim Daar, aliyekuwa mkurugenzi wa huduma za […]

IEBC YAWAHIMIZA VIJANA KUJISAJILI

Tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, imewahimiza vijana kujisajili kwa wingi kama wapiga kura, kwa misingi kwamba malalamishi yao ya uongozi yanaweza tu kutatuliwa kwa kuwachagua viongozi walio na uwezo wa kuiendesha nchi. Akizungumza kwenye kaunti ya Machakos, kamishna wa tume hiyo Alutalala Mukhwana, amesisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utawapa jukwaa zuri […]

SHA KUGHARAMIA UZAZI LEVEL 2 NA 3- DUALE

Ni afueni kwa akina mama wanaojifungua katika maeneo ya mashinani baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bima ya afya ya kijamii SHA kulipia gharama za kujifungua katika hospitali za kiwango cha level 2 level 3 zilizosajiliwa kwenye bima hiyo. Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kamati itakayofuatilia akina mama wajawazito ili kudhibiti visa vya vifo […]

UJENZI WA TALANTA STADIUM KUGHARIMU BILIONI 10 ZAIDI YA BAJETI- RIPOTI

Gharama ya ujenzi wa uwanja wa Talanta jijini Nairobi wenye uwezo wa kuwabeba watu 60,000 imeongezwa kwa Ksh10.85 bilioni, kulingana  na Mkaguzi Mkuu wa serikali Nancy Gathungu. Katika ripoti mpya ya ukaguzi wa hesabu za Wizara ya Ulinzi ya 2024/25, Gathungu anahoji tofauti ya bei isiyoelezeka katika mradi huo, akibainisha kuwa Hazina ya Kitaifa iliidhinisha Ksh35 bilioni kutoka kwa Hazina ya Maendeleo ya Jamii ya Michezo […]

ARSENAL WAJIOKOA DHIDI YA SPURS, CITY WAKIMBIZA

Kiungo wa Arsenal Eberechi Eze aliwahangaisha Tottenham mara tena tangu kujiunga na Arsenal, akifunga mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 4-1 kwenye debi la London jana na kuwarejeshea Gunners uongozi wa pointi 5. Maangamizi mengine yalitekelezwa na Viktor Gyokeres ambaye pia alifunga mara 2, na kuzima juhudi za Kolo Muani kujaribu kuwarejesha Spurs mchezoni. Ushindi […]