HUDUMA YA MAGEREZA YAANZA MPANGO MPYA WA MICHEZO

Kenya Prisons Service imezindua mpango mpya wa michezo unaolenga kuimarisha afya ya akili ya maafisa, kuinua morali na kukuza mshikamano ndani ya idara. Mpango huo, uliozinduliwa wakati wa michezo ya mpira wa kwanza kabisa ya Kamishna Mkuu, utaunganisha maafisa kutoka mikoa 10 ya huduma hiyo kushindana katika mashindano 13, ishara ya jitihada za kurejesha mshikamano […]

NDUNG’U ATAKA USAFISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Mwanaharakati Ndung’u Wainaina ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kusafisha daftari la wapiga kura wakati zoezi la usajili wa wapiga kura likiendelea kote nchini. Wainaina, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Sera na Migogoro, amesema ukaguzi uliofanywa na KPMG kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ulibaini kasoro kadhaa katika sajili […]

KIBET AONYA DHIDI YA SIASA ZA UKABILA

Msaidizi wa Rais, Farouk Kibet, ameongeza joto katika mjadala wa kisiasa huku akionya viongozi wanaochochea siasa za kikabila, akihimiza siasa zinazolenga umoja wa kitaifa, ukuaji wa uchumi na maendeleo jumuishi kwa Wakenya wote. Akizungumza katika eneo la Chebarus, eneobunge la Cherangany, Kibet alisema eneo hilo lina nafasi kubwa ya kunufaika kupitia ushirikiano na serikali ya […]

IEBC YAANZA USAJILI MPYA WA WAPIGA KURA

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imetangaza kuanza kwa zoezi la Usajili Endelevu wa Wapiga Kura ulioboreshwa, huku ikibainisha baadhi ya maeneo yatakayoachwa nje ya zoezi hilo la kitaifa. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa X tume hiyo imesema zoezi hilo la siku 30 tayari limeanza na litakamilika Aprili 28,likilenga kuongeza idadi ya wapiga kura kabla […]

MUDAVADI ATETEA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA KAUNTI YA NAIROBI.

Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi, ametetea na kueleza athari pana za makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na Kaunti ya Nairobi. Mudavadi amesema mfumo huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa miundombinu ya jiji, utoaji wa huduma na ushindani wake kimataifa. Akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Ugatuzi na […]

MVUTANO NDANI YA ODM WAZIDI KUTOKOTA

Naibu kinara wa ODM, Abdulswamad Sharif Nassir, amewataka viongozi wa mrengo wa Linda Mwananchi kusitisha mashambulizi ya maneno dhidi ya kinara wa chama hicho, Oburu Odinga, akisema wengi wa wanachama wanaunga mkono uongozi wake. Akizungumza eneo la Jomvu wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara, Nassir amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya wengi ndani ya chama na […]

AFA YAONYA WAUZAJI BIDHAA NJE JUU YA UTUNZAJI WA PARACHICHI

Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) imewaonya wasafirishaji na wasindikaji wa parachichi kuwa kushughulikia matunda ambayo hayajakomaa kutasababisha kufutwa mara moja kwa leseni za usajili na usafirishaji wa parachichi. Maagizo hayo yanaambatana na kufunguliwa kwa msimu wa mauzo ya parachichi wa 2025/2026 kwa usafirishaji wa baharini, huku Kenya ikijiandaa kuingia katika soko la China chini ya […]

SPURS WATENGANA NA MKUFUNZI WAO TUDOR

Klabu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, EPL, imemfuta kazi kocha wake Igor Tudor, baada ya mechi 7 pekee klabu hiyo inapopambana kuepuka kushushwa daraja. Chini ya uongozi wake, Spurs walipoteza mechi 5 na kuachwa nje yak inyanng’anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa bara Ulaya, na sasa wana pointi moja pekee nje ya eneo […]

WAKENYA WAWIKA BERLIN

Wakenya walitangaza umahiri wao jijini Berlin kwenye mbio za Half Marathon, kutokana na kasi yao ya kuridhisha kwenye mbio hapo jana. Andrea Kiptoo alimaliza wa kwanza katika mbio za wanaume kwa muda wa dakika 59:11, sekunde 3 pekee mbele ya mkenya mwenzake Dennis Kipkemoi, huku Mjerumani Amanal Petros akifunga nafasi tatu bora. Katika mbio za […]

LEOPARDS MGONGONI PA GOR KUFUATIA USHINDI

Klabu ya AFC Leopards iliweka wazi nia yake ya kuwania ubingwa wa taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kariobangi Sharks ugani Nyayo hapo jana. Kwa sasa wanawaandamana viongozi wa ligi hiyo Gor Mahia, kwa pointi 4 pekee ingawa Gor wana mechi moja mkononi. Bao la pekee […]