BINGWA WA ZAMANI WA U20 KUONJA BERLIN HALF MARATHON

Chipukizi wa Kenya Benson Kiplangat imeratibiwa kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya half Marathon jijini Berlin Jumapili hii, ikiondokea mbio za masafa mafupi kuingia masafa marefu. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 22, alitangaza uwepo wake katika fani ya riada katika mbio za ubingwa wa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka wa 2021, […]

GACHAGUA AWAHIMIZA VIJANA KUJIHAMI NA KURA

Huku zoezi la kitaifa la kuwasajili wapiga kura wapya likiendelea, vijana kote nchini wamehimizwa kujitokeza na kusajiliwa kwa wingi ili kuafikia mabadiliko ya uongozi ambayo wamekuwa wakishinikiza kupitia maandamano. Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, amesema muungano wa upinzani unategemea idadi kubwa ya wapiga kura wapya kumbandua madarakani Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu […]

UPASUAJI WA MAITI KUENDELEA KERICHO

Imebainika kwamba watoto 4 kati ya 25 waliofukuliwa kutoka kaburi la pamoja kwenye kaunti ya Kericho walifariki kutokana na majeraha ya kichwa, huku wengine 10 wakifariki baada ya kuzaliwa kabla ya siku zao kufika. Kulingana na ripoti ya upasuaji wa maiti iliyoongozwa na mwanapatholojia wa serikali Dakta Richard Njoroge, miili ya waathiriwa ilikuwa katika hatua […]

SERIKALI YAVUNJA KIMYA CHA PASIPOTI

Maswali yameendelea kuibuka kuhusu ni kwanini serikali imechukua muda mrefu kutoa msimamo wake kuhusu taarifa za kuwapa paspoti za usafiri makamanda wa kundi la wapiganaji la RSF nchini Sudan, na badala yake kujitokeza hapo jana baada ya wiki kadhaa kukanusha taarifa hizo. Katibu mkuu katika idara ya uhamiaji Dakta Belio Kipsang, amesema suala hilo linaangaziwa […]

KONGAMANO LIPI LA ODM?

Chama cha ODM kimeratibiwa kuandaa kongamano la kitaifa la wajumbe wake, NDC kwa mara ya kwanza tangu kifo cha kinara mwanzislishi wa chama hicho marehemu Raila Odinga, kongamano litakaloongozwa na kinara mpya Uburu Oginga. Kongamano hilo linajiri huku wanachama wakisalia njia panda kuhusu kongamano lipi watakalohudhuria, ikizingatiwa kuwa mrengo wa Linda Mwananchi unaowajumuisha katibu mkuu […]

MATHARE WOMEN WAWANIA USHINDI WA SITA MFULULIZO

Mathare Women United wanapania kuendeleza ubabe wao watakapokutana na Hildana Queens katika mechi ya Ligi ya Kitaifa mwishoni mwa wiki hii. Vinara hao wa ligi wamekuwa katika kiwango bora katika mzunguko wa pili wa msimu na sasa wanawania ushindi wa sita mfululizo ili kuimarisha uongozi wao kileleni mwa jedwali. Kocha mkuu Ann Aluoch ameonyesha imani […]

OGAM ATOA WITO WA NIDHAMU YA KIUFUNDI KABLA YA MECHI NA ESTONIA

Mshambuliaji wa Harambee Stars, Ryan Ogam, ametoa wito wa nidhamu ya kiufundi, uelewa wa nafasi na utulivu wa akili kuelekea mechi ya ufunguzi ya Fifa Series dhidi ya Estonia itakayochezwa Ijumaa katika Uwanja wa Amahoro. Mechi hiyo ya kwanza kati ya mataifa hayo mawili inakuja wakati muhimu kwa Kenya, ambayo iko katika kipindi cha mabadiliko ikitafuta mwelekeo […]

OMOLLO AONDOKA KCB KUELEKEA JAPAN

Klabu ya Raga ya KCB imethibitisha kuondoka kwa mchezaji chipukizi Andycolle Omollo ambaye anaelekea Japani kuanza masomo baada ya kupata ufadhili katika Chuo Kikuu cha Tenri. Omollo, aliyejiunga na KCB akitokea MMUST, anatarajiwa kusafiri Jumamosi, Machi 28, hatua inayochukuliwa kuwa muhimu katika safari yake ya masomo na raga. Mchezaji huyo ameonyesha kiwango cha juu katika […]

MASHINDANO YA RAGA YA SHULE ZA UPILI KWA WASICHANA KUREJEA

Mashindano ya kitaifa ya raga ya wasichana wa shule za upili yatafanyika kuanzia Aprili 6 hadi 10 katika Shule ya Maseno, kaunti ya Kisumu, yakirejea baada ya toleo la mwisho kufanyika mwaka 2024. Mashindano ya mwaka huu yana umuhimu mkubwa kwani mchezo wa raga ya wasichana utajumuishwa rasmi katika michezo ya muhula wa kwanza ya […]

MAHAKAMA YAONGEZA AMRI KUHUSU MCHAKATO WA KUMWONDOA DPP

Mahakama Kuu imeongeza muda wa amri ya kusitisha mchakato wa kuandaa kanuni za kumwondoa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.(DPP) Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mahakama kuthibitisha kuwa kesi inayotaka maafisa wa Tume ya Huduma za Umma kushtakiwa kwa kudharau mahakama ni ya dharura. Mahakama imeagiza maombi yawasilishwe kwa wahusika wote ndani ya siku tatu, huku […]