HSBC: SHUJAA, LIONESSES WAMALIZA JUKWAANI BRAZIL

Timu za taifa za raga za wachezaji 7 kila upande, Shujaa ya wanaume na Lionesses ya wanawake, zilimaliza kwa kishindo kwenye mkondo wa mwisho mashindano ya kwanza ya HSBC Division 2, zikijizolea nishani za fedha kwenye mashindano hayo yaliyokamilika jana jiji Sao Paulo, Brazil. Shujaa, ambao wamejikatia tiketi ya kushiriki dimba la Sevens World Championship […]

110: IDADI YA VIFO KUTOKANA NA MAFURIKO

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchuini imepanda na kufikia watu 110 kufikia jana jioni, serikali ikisema hali inaendelea kuwa mbaya katika maeneo ambako mvua hiyo inaendelea. Kwenye taaifa ya hivi punde, wizara ya usalama wa kitaifa imesema kuwa kaunti 30 zimeathirika kufikia sasa, Kilifi, Bungoma, Kirinyaga, Nyeri, Kiambu, Uasin […]

MUSYOKA AONYA UCHAGUZI WA KIMAPINDUZI 2027

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC kulihakikishia taifa uchaguzi huru na haki mwaka ujao, akionya kuwa uchaguzi huo utakuwa wa kimapinduzi. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Musyoka amesisitiza kuwa IEBC ina fursa ya kujitenga na dhana kwamba makamishna wake ni vibaraka wa Rais William […]

OYUU AWAONYA WANACHAMA WA KNUT

Huku uchaguzi wa muungano wa kutetea maslahi ya walimu KNUT ukikaribia, katibu mkuu wa muungano huo Collins Oyuu amewatahadharisha wananchama kuwa macho na wagombeaji anaodai wanalenga kuhujumu muungano huo. Kwenye kampeni zake mjini Homa Bay, Oyuu amewahimiza wanachama wa KNUT kuwachagua viongozi walio na maono ya kuuendeleza muungano huo na utetezi wa wananchama wake. Imetayarishwa […]

GACHAGUA ADAI SHA IKO MAGOTINI

Wizara ya afya imekanusha taarifa kwamba bima ya SHA itasambaratika ndani ya miezi 6 ijayo kutokana na mzigo wa madeni, jinsi ilivyoibuliwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua. Kwa mujibu wa Gachagua, ni wakati kwa hospitali za umma na za kibinafsi kudai malipo yao kutoka SHA kabla ya kutoa huduma kwa wagonjwa, akisema sekta ya […]

NYARIBO AITENGA SERIKALI YAKE NA MIILI 20 KERICHO

Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo, ameshinikiza uchunguzi kufanywa ili kubaini ilikotoka miili 20 ya ziada iliyofukuliwa kwenye kaburi la pamoja katika kaunti ya Kericho, akisisitiza kuwa serikali yake iliidhinisha miili 13 pekee kuzikwa kulingana amri ya mahakama. Akizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu utata huo, Nyaribo amekariri kuwa utawala wake ulifuata taratibu hitajika katika […]

MIMI KATIBU WA OBURU? MTANISAMEHE- SIFUNA

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, amekariri msimamo wake kwamba hatahudumu kwenye wadhifa huo chini ya kinara wa sasa wa chama hicho Oburu Oginga, kwa misingi kwamba Oburu hana haiba hitajika ya kukiongoza chama hicho. Kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa kaunti ya Mombasa, Sifuna aliyekuwa ameandamana na viongozi wamengine wanaoegemea mrengo […]

MIGAWANYIKO ODM MKAKATI WA ODINGA, WAKILI ADAI

Imeibuka kwamba mrengo wa waasi wa Linda Mwananchi ndani ya chama cha ODM ukiongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna, ulipangwa kimaksudi na aliyekuwa waziri mkuu marehemu Raila Odinga kama mkakati wake mpana wa kuondoka kwenye ushirikiano wa kisiasa na Rais William Ruto endapo matakwa yake hayangetekelezwa. Kwenye mahojiano, wakili Paul Mwangi, aliyekuwa mwandani wa siku […]

MAAFISA WA FKF WAPATA NYADHIFA NOC

Maafisa wanne wa Shirikisho la Soka nchini wamepata uteuzi katika Kamati ya Olimpiki ya Kenya, hatua inayotarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya uongozi wa soka na malengo ya michezo ya kimataifa. Msimamizi wa timu ya taifa, Nick Kimanthi, ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa kiufundi, huku mwakilishi wa wanawake Violet Kerubo Momanyi akipewa jukumu […]

KARIOBANGI SHARKS WAKABILIWA NA MTIHANI MGUMU

Kocha wa Kariobangi Sharks, William Muluya, anakabiliwa na mtihani mkubwa watakapomenyana na AFC Leopards katika uwanja wa Nyayo Jumapili huku hatima ya kusalia ligi ikiwa hatarini. Tofauti ya malengo inaonekana wazi, ambapo AFC Leopards wako nafasi ya pili wakiwa na alama 56 huku Sharks wakiwa nafasi ya 14 na alama 25, alama nne pekee juu […]