BABU AASHIRIA KUANZISHA CHAMA KIPYA CHINI YA LINDA MWANANCHI

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amedokeza uwezekano wa kuanzishwa kwa chama kipya cha kisiasa chini ya vuguvugu la “Linda Mwananchi,” akionyesha mabadiliko yanayoweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Akizungumza katika mahojiano, Babu amesema Wakenya wanapaswa kutarajia chama kipya chenye mwelekeo na uongozi tofauti, akionekana kujitenga na chama chake cha sasa cha ODM. Aidha, mbunge huyo ametangaza […]

CHERARGEI AWASILISHA HOJA YA KUSITISHA MARUPURUPU YA UHURU

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amewasilisha hoja katika Seneti akitaka kusitishwa au kupunguzwa kwa marupurupu ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Kupitia hoja hiyo, Cherargei anataka Bunge kufuta, kubadili au kugawa upya fedha zinazohusiana na marupurupu ya kiongozi huyo wa zamani, akipendekeza fedha zitakazookolewa zielekezwe kwa maslahi ya wananchi. Hatua hiyo inajiri wakati washirika wa Rais […]

RUTO AWATAKA MAJAJI KUDUMISHA UADILIFU

Rais William Ruto amewataka majaji wapya kudumisha uadilifu, uhuru na ufanisi katika utoaji wa haki. Akizungumza wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Majaji 37 wa mahakama mbalimbali, Rais amesema jukumu kuu la mahakama ni kulinda katiba na haki za wananchi, akisisitiza kuwa mamlaka yao yanatokana na katiba na yanapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewakumbusha […]

COFEK YAANGAZIA UPYA UKIUKAJI WA MATUMIZI YA KSH30B ZA EUROBOND

Shirikisho la watumizi wa bidhaa nchini, COFEK, limetoa ripoti mpya kuhusu  matumizi ya mapato kutoka kwa Eurobond ya Ksh bilioni 193.9 bilioni (dola bilioni 1.5) ya Kenya, na kusisitiza kwamba maswali yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu bado hayajatatuliwa. Ingawa matokeo ya utafiti yaliwasilishwa Bungeni wiki kadhaa mapema, COFEK inasema ukubwa wa uvunjaji na mapungufu katika uwajibikaji unastahili kuendelea […]

CARRICK AZUNGUMZIA NAFASI YAKE UNITED

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Michael Carrick, amesema hana shinikizo katika wadhifa huo licha ya shinikizo tele ambazo watangulizi wake wameshuhudia. Carrick aliyasema haya baada ya kuiwezesha United kufuzu kombe la klabu bingwa bara Ulaya msimu ujao kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool hapo jana. Alipochukua hatamu kutoka kwa Ruben Amorim […]

TIMU ZA KPL KUMENYANA SEMI FAINALI YA FKF CUP

Klabu ya Police FC itachuana na Bandari FC kwenye awamu ya nusu fainali ya kombe la FKF kufuatia ushindi wa klabu hizo mbili katika awamu ya robo fainali. Bao la pekee la mchezo la Abud Omar kupitia ikabu liliwapa maafande hao ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Shabana FC na kuwapa tiketi ya nusu […]

GOR MAHIA WAFUNGUA PENGO LA POINTI 9 KILELENI

Klabu ya Gor Mahia ilinufaika na bao la kujifunga kujipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Kakamega Homeboyz hapo jana, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL kwa mara ya 22. Kwenye mechi iliyoshuhudia ukame wa nafasi za ufungaji kutokana na nidhamu na tahadhari kutoka […]

GACHAGUA AMTETEA UHURU DHIDI YA SHUTUMA

Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amemtetea Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta dhidi ya shutuma za viongozi wanaounga mkono serikali kuhusu msimamo wake kisiasa kama kinara wa chama cha Jubilee. Akiwa kwenye ziara yake katika kaunti ya Kajiado, Gachagua amesisitiza kuwa Kenyatta ana haki kikatiba kutoa maoni yake kuhusu siasa za taifa, na uamuzi wa […]

KANG’ATA ABASHIRI MWANGUKO WA UDA

Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema kuwa chama tawala cha UDA kimepoteza umaarufu katika eneo la Mlima Kenya, na kwamba kitaporomoka kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Kang’ata amesema mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yamesababisha chama hicho kupoteza umaarufu wake. Kauli yake inajiri saa chache baada ya awali kutangaza kuwa hatawania […]

MAENEO 59 TANA HATARI KUTOKANA NA MAFURIKO

Jumla ya watu 18 wamefariki kutokana na mafuriko katika siku za hivi karibuni baada ya watu 3 zaidi kufariki, serikali ikisema watu wengine 63 hawajulikani waliko huku wengine zaidi ya 60,000 wakiachwa bila makao. Kulingana na takwimu za serikali, vifo hivyo vimeripotiwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki, Kati, Bonde la Ufa, Nairobi na pwani huku […]