MVUA KUBWA KUENDELEA, RIPOTI

Wakenya wamepewa tahadhari kuhusiana na mafuriko kutokana na mvua kubwa ambayo imebashiriwa kuendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya nchi. Katika ripoti yake ya hivi punde, idara ya utabiri wa hali ya anga imetangaza kuwa mvua hiyo itaendelea katika maeneo ya nyanda za juu za bonde la ufa, ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani, nyanda za […]

UHURU ALENGWA KUPOKONYWA MANUFAA

Mswada wa kumpkonya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta marupurupu yake umeratibiwa kuwasilishwa leo katika bunge la seneti, Kenyatta akituhumiwa kuendelea kujihusisha na siasa licha ya kustaafu. Mswada huo umefadhiliwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei, anayesisitiza kuwa ni ukiukaji wa sheria kwa Kenyatta kuendelea kuikosoa serikali, hatua hii ikijiri baada ya rais huyo wa zamani kuishutumu serikali […]

UBORA WA CBE WATILIWA SHAKA, WANAFUNZI WAASI MASOMO

Imebainika kuwa zaidi ya wanafunzi 151,000 waliofanya mtihani wa kwanza chini ya mtaala wa umilisi CBE waliachia njiani masomo yao ya sekondari msingi, idadi ambayo imeibua hofu kuhusiana na uwezo wa utekelezaji wa mtaala huo. Kulingana na takwimu za baraza la mitihani ya kitaifa, KNEC, wengi wa wanafunzi waliokosa kukamilisha masomo yao ni wavulana, wasichana […]

RUTO AELEZA KIINI CHA KIWANDA CHA MAFUTA TANGA

Rais William Ruto ametetea pendekezo la kuanzishwa kwa kiwanda cha kikanda cha kusafisha mafuta mjini Tanga nchini Tanzania, akisema pendekezo hilo halikuwa uamuzi wa upande mmoja bali ni sehemu ya majadiliano mapana kuhusu viwanda na matumizi ya raslimali za kikanda. Akizungumza wakati wa mazungumzo ya pamoja na mwenzake wa Tanzania Samia Hassan jijini Dar es […]

GUARDIOLA ATOA MAONI KUHUSU MUSTAKABALI WA GREALISH

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wa mchezaji Jack Grealish, akisisitiza kuwa anamtakia kila la heri katika hatua yake ya sasa. Guardiola amesema Grealish alikuwa na mchango mzuri alipokuwa akipata muda wa kucheza, akitaja pia athari yake katika msimu wa ushindi wa mataji matatu kwa klabu hiyo. Ameongeza kuwa jeraha […]

JUNIOR STARLETS YATAJA KIKOSI CHA AWALI

Kocha wa Junior Starlets Mildred Cheche ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya miaka 17 dhidi ya Uganda. Cheche amedumisha sehemu kubwa ya kikosi kilichofanya vyema katika raundi iliyopita ambapo waliifunga Namibia kwa jumla ya mabao 7–1 na kufuzu hatua inayofuata. Kikosi hicho kinatarajiwa […]

POLICE BULLETS YALENGA UBINGWA WA TATU MFULULIZO

Kocha wa Kenya Police Bullets David Vijago amesema ana imani hakuna kitakachowazuia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa mara ya tatu mfululizo. Timu hiyo ilithibitisha ubora wake baada ya kuichapa Vihiga Queens mabao 9–0 katika uwanja wa Police Sacco, huku Margaret Kunihira na Emily Moranga wakifunga mabao mawili kila mmoja, na wenzao kuchangia […]

NGATIARI NA NJERI WANG’ARA MIGA GOLF CLUB

Anthony Ngatiari na Teresia Njeri wameibuka washindi wakuu katika duru ya 10 ya Mfululizo wa Gofu wa NCBA 2026 iliyofanyika katika Migaa Golf Club mwishoni mwa wiki, huku mbio za kufuzu fainali kuu zikiendelea kushika kasi. Katika kitengo cha Wanaume, Ngatiari alionyesha mchezo wa kiwango cha juu na kutwaa nafasi ya kwanza katika kundi lililokuwa […]

WANAFUNZI WA UON WATISHIA MGOMO KUHUSU MAKAMU CHANSELLA

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wametishia kugoma wakidai kuteuliwa kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho. Wanafunzi hao wanasema kucheleweshwa kwa uteuzi huo kumeathiri uongozi na uendeshaji wa chuo, hali wanayodai inasababisha sintofahamu miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri. Wameonya kuwa watachukua hatua za mgomo iwapo suala hilo halitashughulikiwa haraka na mamlaka husika. Imetayarishwa na Cyrus […]

MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA KIFO CHA DAKTARI OBWAKA

Mwanamke anayetajwa kuwa mtu wa kuhojiwa kuhusiana na kifo cha daktari bingwa wa wanawake na mkurugenzi wa Hospitali ya Nairobi, Daktari Job Obwaka, amefikishwa katika Mahakama ya Kibera. Beatrice Wangari alikamatwa Mei 2baada ya kubainika kuwa alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu mwenye umri wa miaka 79 katika Hospitali ya Nairobi. Daktari Obwaka alitangazwa kufariki alipofikishwa […]