FODEN ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER CITY

Kiungo wa Manchester City Phil Foden amesaini mkataba mpya utakaomweka klabuni hapo hadi Juni 2030, huku makubaliano hayo yakithibitishwa rasmi. Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo imeonyesha imani kubwa kwa Foden, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Mkataba huo mpya pia unajumuisha kipengele cha kuongeza muda wa kuendelea hadi […]

SIRAJ MOHAMMED ANG’ARA KCB

Uchezaji wa beki wa kushoto Siraj Mohammed akiwa katika klabu ya KCB  umeendelea kuimarika, baada ya kipindi cha mkopo kilichompa nafasi ya kurejea katika kiwango chake cha juu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anayefahamika kwa jina la utani “Mastermind,” alijiunga na KCB mwezi Februari 2026 baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika klabu ya  Gor […]

FELIX OLOO AFARIKI KATIKA AJALI MAREKANI

Kocha wa zamani wa Kenya Lionesses na mchezaji wa zamani wa Nakuru RFC Felix Oloo amefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani nchini Marekani. Inaripotiwa kuwa Oloo aligongwa na gari alipokuwa akijaribu kuvuka barabara kuu ya Interstate 405 katika eneo la Bothell, Washington, katika tukio lililotokea mapema Jumatatu asubuhi ambalo bado linachunguzwa. […]

DCI YAWAKAMATA WASHUKIWA WAWILI WA UHALIFU TRANS NZOIA

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai DCI katika Kaunti ya Trans Nzoia wamewakamata watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu uliopangwa kufuatia operesheni ya kiusalama eneo hilo Kupitia taarifa iliyotolewa, DCI imesema washukiwa hao walikamatwa katika msako ulioongozwa na taarifa za kijasusi uliofanywa na maafisa wa Kituo cha Polisi cha Kitale kwa kushirikiana na kikosi maalum cha upelelezi. […]

IEBC YASISITIZA USIRI WA KURA

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imesisitiza dhamira yake ya kulinda usiri wa kura, ikitetea pendekezo la kupiga m arufuku upigaji picha wa karatasi za kura zilizopigwa. Kamishna wa IEBC Anne Nderitu amesema kulinda uadilifu wa mchakato wa uchaguzi ni muhimu zaidi kuliko matakwa binafsi ya kushiriki chaguo la kura mitandaoni. Alionya kuwa kuruhusu wapiga kura […]

OGAMBA AHIMIZA UTEKELEZAJI WA CBE

Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa wito wa kuharakishwa kwa utekelezaji wa mfumo wa elimu unaozingatia ujuzi wa mwanafunzi, CBE. Ogamba amesisitizaumuhimu wa mfumo huo katika kukuza ubunifu na kuwajengea wanafunzi ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Wadau wa elimu pia wameitaka serikali kuunga mkono ubunifu na kuwekeza zaidi katika rasilimali na miundombinu ili kuhakikisha […]

RUTO AZUA VICHEKO BUNGENI TANZANIA

Rais William Ruto amewachekesha wabunge wa Tanzania baada ya kueleza kwa utani sababu ya kutumia lugha ya Kiingereza badala ya Kiswahili wakati wa hotuba yake. Akihutubia bunge hilo, Ruto alitoa maelezo ya kihistoria kwa kuhusu Kiswahili kabla ya kuamua kutumia Kiingereza, akisema hataki kukosea katika matumizi ya lugha hiyo. Kauli hiyo ilizua vicheko miongoni mwa […]

USIKU MKUBWA WA ARSENAL

Katika kinachoonekana kuwa tukio kubwa zaidi katika historia ya uwanja wa Emirates, Arsenal itakuwa mwenyeji wa Atletico Madrid katika mkondo wa pili wa mechi ya semi fainali ya klabu bingwa bara Ulaya, wanapolenga kucheza fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu ufunguzi wa uwanja huo mwaka wa 2006. Viktor Gyokeres na Julian Alvarez […]

ARSENAL WAFAIDI HASARA YA CITY DHIDI YA EVERTON

Bao la Wing’a Jeremy Doku katika dakika za mwisho lilinusuru pointi moja kwa Manchester City katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Everton, sare ambayo imewaacha Arsenal wakiwa wameshikilia usukani wa taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL. Arsenal walio na pointi 76, 5 mbele ya City, sasa watahitaji kushinda mechi zao zote […]

MUNGUTI ALENGA KUTIFUA KIVUMBI SHANGHAI

Bingwa wa kitaifa wa mbio za mita 1,500 mwaka wa 2023 Daniel Munguti, ana matumaini ya kuanza safari yake ya kuwinda ubingwa kimataifa kwa kishindo, atakaposhiriki mbio za mita 3,000 katika mashindano ya Diamond League ya Shanghai baadaye mwezi huu. Munguti alianza kampeni ya msimu wake kwa kumaliza wa tatu katika mbio za Kip Keino […]