GOR WAONYESHA UBABE KASARANI

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya soka KPL Gor Mahia walitoka chini na kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Murang’a SEAL ugani Kasarani kwenye mechi ya ligi kuu hapo jana, na kupanda kileleni kwa jedwali kwa pointi 30 sawa na AFC Leopards. Gor waliporomoka ndani ya dakika 18 za mwanzo za mchezo na […]

SIKU KUBWA UGANDA

Mamilioni ya raia nchini Uganda wameratibiwa kushiriki uchaguzi mkuu hii leo huku viongozi wa upinzani na wanaharakati wakiibua madai ya uwepo wa njama ya udanganyifu kwenye uchaguzi huo hasa kutokana na na kuzimwa kwa mitandao ya mawasiliano. Rais Yoweri Museveni analenga kuendeleza utawala wake wa zaidi ya miaka 40 anapomenyana na mpinzani wake Robert Kyagulanyi […]

RUTO KUZINDUA NYOTA MACHAKOS

Jumla ya vijana 7,700 katika kaunti za Ukambani ambazo ni Makueni, Machakos na Kitui wameratibiwa kunufaika na fedha za kibiashara za serikali chini ya mradi wa NYOTA, zitakazozinduliwa hii leo mjini Machakos. Hafla hiyo itaongozwa na Rais William Ruto, shilingi milioni 169 zikitarajiwa kusambazwa kwa vijana hao wenye umri wa kati ya miaka 19-29 huku […]

ODM, UDA HURU KUANZA MAZUNGUMZO

Vyama vya ODM na UDA vinatarajiwa muda wowote kukutana na kupanga mikakati ya ushirikiano wa kisiasa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, baada ya kamati kuu za vyama hivyo kuidhinisha mazungumzo hayo. Kamati kuu ya uongozi ya UDA ni ya hivi punde kuafikia uamuzi huo hapo jana na kumwidhinisha kinara wake ambaye ni […]

WAGONJWA TAABANI NAIROBI

Huduma za matibabu katika hospitali za umma jijini Nairobi zinatarajiwa kutatizika zaidi kutokana na mgomo wa madaktari na maafisa wa kliniki ambao umeingia siku ya 4, huku wauguzi wakitarajiwa kujiunga na mgomo huo kuanzia leo. Madaktari na maafisa kliniki wamesusia kazi ili kuishinikiza serikali ya kaunti ya Nairobi kuwapa malipo yao ya kati ya mwezi […]

KESI YA MANDAGO KUENDELEA LEO NAKURU

Kesi kuhusu sakata ya ubadhirifu wa fedha za ufadhili wa masomo inayomhusisha seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago, washtakiwa wenza Joshua Lelei na Meshack Rono imeratibiwa kuendelea hii leo katika mahakama ya Nakuru. Watatu hao wanakabailiwa na mashtaka ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma kima cha shilingi bilioni 1.1, afisi ya mkurugenzi wa […]

BIASHARA ZA MAMILIONI  ZABOMOLEWA KARIBU NA UWANJA WA NYAYO 

Wafanyabiashara wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya mali za thamani ya mamilioni kuharibiwa wakati wa operesheni ya usiku wa kuamkia leo, karibu na eneo la Nyayo kuandaa njia kwa mradi ujao wa miundombinu. Picha zilizonaswa  zinaonyesha tingatinga na wachimbaji wakisawazisha miundo katika eneo hilo, wakiandamana na maafisa wa polisi waliokuwa eneo la tukio kusimamia shughuli hiyo.Ubomoaji huo ulifanyika […]

CARRICK ATEULIWA KUINOA UNITED

Manchester United imemteua Michael Carrick kama meneja mshikilizi hadi mwisho wa msimu kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim, akitwikwa jukumu la kuwarejesha United kwenye dimba la klabu bingwa barani Ulaya. Carrick mwenye umri wa miaka 44, alishinda mataji 12 makuu na klabu hiyo katika kipindi cha miaka 12 alichoichezea. Kiungo huyo […]

MABAO YA SEMENYO, CHERKI YAWAPA CITY USUKANI

Manchester City walitia guu moja ndani ya fainali za Carabao Cup jana usiku, kufuatia mabao ya sajili mpya Antoine Semenyo na Rayan Cherki yaliyowapa ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya bingwa mtetezi Newcastle United. Semenyo aliyewasili wiki jana kutoka Bournemouth kwa kima cha pauni milioni 65, ameonyesha ubabe wake, akiwa amefunga mara 2 na […]

AFCON 2025: USIKU WA NUSU FAINALI

Ulimwengu unakutanishwa nchini Morocco leo usiku ambapo semi fainali za kipute cha mataifa bingwa barani Afrika zitachezwa, zikiwaleta Pamoja miamba wa soka barani. Katika semi fainali ya kwanza, Lions of Teranga wa Senegal watatoa kucha zao dhidi ya Pharaohs wa Misri ambao ni bingwa wa kihistoria mara 7, katika pambano ambalo pia litawakutanisha wachezaji mahiri […]