SAFARI YA MAAFISA 400 HAITI YANGOA NANGA

Kikosi cha Kenya kitakachoongoza ujumbe wa kimataifa kukabiliana na ghasia za magenge ya Haiti kimeondoka nchini usiku wa kuaamkia leo. Rais William Ruto ameongoza hafla ya kuwaaga na kuwakabithi bendera maafisa hao katika chuo cha kitaifa  cha polisi kilichoko katika eneo la embakasi jijini Nairobi. Katika taarifa rais Ruto ameeleza imani yake kwamba maafisa hao […]

“IMFIKIE INJENDI!”- WAANDAMANAJI MALAVA

Kundi la vijana waliokuwa wakiandanmana wamevamia mkutano wa mwakilishi wa kike kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda uliokuwa ukiandaliwa katika eneo bunge la malava wakimsaka mbunge wa eneo hilo Malulu Injendi ambaye alipiga kura ya ndiyo kuhusu mswada wa fedha wiki jana. Vijana hao wamechukua usimamizi wa hafla hiyo na kuamuru kwamba mbunge huyo asiondoke na […]

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

Kenya imelipa dola milioni 556.97 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 71.5 zilizosalia za Eurobond ya dola bilioni 2 kiwango sawa na shilingi bilioni 257 ambazo zilipaswa kulipwa kufikia leo. Takwimu za Ofisi ya Kusimamia Madeni ya Umma ya Hazina ya Kitaifa zinaonyesha kwamba deni hilo ambalo lilikuwa limesalia lilipwa siku ya ijumaa iliyopita siku […]

WITO WA KRA

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA imetoa wito kwa walipa kodi wote waliosajiliwa kusasisha maelezo yao ya usajili kwenye mfumo wa iTax. Katika notisi ya leo hii, Mamlaka hiyo imesema limeanzisha zoezi la kina la kusafisha data kwa maelezo yote ya usajili ya nambari za kibinafsi za walipa kodi (PIN). Maelezo yatakayosahihishwa ni pamoja na […]

‘MAANDAMANO YA PUNDA’ LAMU

Wakazi kisiwani Amu kaunti ya Lamu wameendeleza maandamano dhidi ya mswada wenye utata wa kifedha wa mwaka 2024, wakati huu wakitumia punda kuandamana wakitoa lalama zao kuhisiana na mswada huo. Wakati wa maandamano hayo, wakazi hao wamehofia kukamndamizwa kiuchumi iwapo mswada huo utapitishwa, na kuwakosoa wabunge wao waliopiga kura ya ndiyo na kupitishwa mswada huo […]

BONIFACE MWANGI, WILLY MUTUNGA WAJIWASILISHA DCI

Wanaharakati wawili ambao ni Bonface Mwangi na Hanifa Adan wamejiweasiwasilisha katika makao makuu ya idara ya jinai DCI kwenye barabara ya Kiambu wakiwa wameandamana na jaji mkuu wa zamanai Willy Mutunga na mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la kiraia la haki Africa Hussein Khalid. Wanaharakati hao ambao wamekuwa mafichoni wametaka kujua ni kwanini wenzao katika […]

“HATUWATAMBUI!” WAANDAMANJI BUNGOMA

Vijana kutoka maeneo bunge ya webuye magharibi na webuye mashariki kaunti ya Bungoma wameandamana mjini Webuye huku wakiwakosoa wabunge wao ambao ni Dan Wanyama na Martin Wanyonyi kwa kupiga kura ya ndio kuhusu mswada wenye utata juma lililopita. Wakati wa maandamano hayo, kijana mmoja aliyejitokeza kupinga maandamano hayo amejeruhiwa vibaya na waandamanaji. Aidha, vijana hao […]

MWANAMUME WA MIAKA 25 AFARIKI JIKONI KWA MAMAYE SIAYA

Polisi katika kaunti ya Siaya wameanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mkazi mmoja huko Ugenya.George Nyaginde Amenya mwenye umri wa miaka 25 amepatikana amefariki jikoni kwa mamake. Inaarifiwa kuwa marehemu alivamiwa katika kitongoji cha Nyalenya kilichopo Uyunya. Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo, kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha […]

SHULE ZOTE ZIFUNGWE MARA MOJA; WIZARA YA ELIMU YASEMA

Shule zote zifungwe kwanzia leo kwa likizo fupi, haya ni kwa mujibu wa wizara ya elimu ambayo imesema kuwa hatua hiyo imetokana na maandamano ambayo yamepangwa kufanyika hapo kesho na kundi la vijana Gen-Z kupinga mswada wa fedha 2024. Imetayarishwa na Janice Marete.

MAMA WA MIAKA 45 ANGAMIA KATIKA MKASA WA MOTO KIRINYAGA

Polisi katika Kaunti ya Kirinyaga wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 45 amefariki katika kisa cha moto katika kijiji cha Getuya eneo bunge la Ndia usiku wa kuamkia leo. Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Kirinyaga Magharibi Moses Koskei, maiti ya mwanamke huyo iligunduliwa ikiwa imechomwa kiasi cha kutotambulika na wakaazi […]