VIPENGELE VINGINE HAVIKUWEKO KATIKA MSWADA;MBUNGE SEME ASEMA

Mbunge wa seme James Nyikal amesema kuwa kuna mapendekezo mapya yaliyopendekezwa katika mswada wa fedha na kuchangia ghathabu ya wakenya dhidi ya mswada huoNyikal ametaja kipengele cha kuongeza ada katika bei ya mafuta kwamba akikuwepo katika mswada hapo awali. Imetayarishwa na Janice Marete.

SERIKALI YATOA BILIONI 6.7B KULIPA MADENI YA WAKULIMA WA KAHAWA

Serikali imetenga Shilingi bilioni 6.7 kuwalipia madeni wakulima wa kahawa, huku kukiwa na onyo dhidi ya matumizi mabaya ya fedha hizo. Hii ni baada ya ripoti ya Baraza la Mawaziri la Wizara ya Vyama vya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Kati kuidhinishwa kusaidia wakulima kulipa madeni wanayodaiwa. Wakati wa mikutano ya […]

CJ KOOME ATOA HATUA 7 ZA USALAMA MAHAKAMANI

Jaji Mkuu Martha Koome ametaja hatua za usalama zitakazotekelezwa katika mahakama zote kufuatia kupigwa risasi kwa Hakimu Mkuu Monica Kivuti katika Mahakama ya Makadara. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Koome amesema kuwa polisi wa Mahakama kwa kushauriana na inspekta generali wa polisi watafanya msako mkali ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayefika mahakamani akiwa na […]

MALALA AWAONYA WABUNGE WA KENYA KWANZA DHIDI YA KUPINGA MSWADA 2024

Cleophas Malala ambaye ni katibu wa chama cha UDA amewaonya wabunge wa kenya kweanza dhidi ya kuenda kinyume na matakwa ya serikali wakati wa kujadili mswada wa fedha. Kwa mujibu wa Malala watakaokiuka msimamo wa vyama tanzu vya kenya kwanza watachukuliwa hatua kali za kinidhamu. Imetayarishwa na Janice Marete

KURIA AWASUTA WANAOPINGA MSWADA WA FEDHA

Mwenyekiti wa kamati yafedha katika bunge la kitaifa Kimani Kuria amewasuta wanaopinga mswad wa fedha 2024 kwa madai kwamba wanaoshinikiza wabunge wao kuupinga mswada huo hawajasoma na kufahamu vyema mswada huo. Kuria amesema kuwa baadhi ya madai yaliyoibuliwa mfano kuongezwa kwa kodi ya ardhi wamepotosha umma. Imetayarishwa na Janice Marete

UNASAFISHA MAJI CHAFU?;SIFUNA AWAAMBIA WABUNGE

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amepuuzilia mbali mpango wa serikali kufanyia marekebisho baadhi ya mapendekezo katika Mswada wa Fedha wa 2024 kwa akisisitiza kuwa wabunge wa mrengo wa Azimio wanapendekeza mswada huo ufutiliwe mbali kwa kuwa unalenga kupandisha gharama ya maisha kwa wakenya. Imetayarishwa na Janice Marete

UJERUMANI YAKABWA KOO

Mchezaji Niclas Fullkrug aliyetokea benchi aliifungia Ujerumani bao la kusawazisha dakika za lala salama walipookoa sare ya bila kufungana na Uswizi hadi kileleni mwa Kundi A. Uswizi  walikua na matumaini ya kuingia hatua ya 16 bora wakiwa washindi wa kundi baada ya bao la mapema kutoka kwa Dan Ndoye ila Fullkrug akawatoa matumaini hayo Lilikuwa […]

GOR MAHIA WATAWAZWA WASHINDI WA LIGI KUU

Benson Omalla alifunga mabao mawili huku mabingwa Gor Mahia wakiilaza wenyeji Bidco United 4-3 na kutia moyo kutawazwa kwao katika uwanja wa Machakos, michuano ya Ligi Kuu ya Soka ya Kenya msimu wa 2024 iliposhuka Jumapili. Omalla aliyeshinda Kiatu cha Dhahabu kwa mabao 19, alihakikisha K’Ogalo inakusanya jumla ya pointi 73, nane zaidi ya wapinzani […]

MATILI WABEBA USHINDI

Timu ya soka ya Matili TTI ilishinda Ligi ya FKF Kanda ya Magharibi kwa msimu wa 2023/24, kwa kuwalaza APS Seal 4-3 kwa mikwaju ya penalti Jumapili katika uwanja wa Shule ya Upili ya Kakamega. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali, ambapo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare tasa licha ya mashambulizi ya pande zote […]

KENYA LIONESS WALEMEWA NA CHINA

Ndoto ya Timu ya taifa ya raga ya wanawake ya Kenya, Kenya Lionesses,  ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 ikisambaratika baada ya kushindwa 24-7 na Uchina katika mchezo wa marudio kule mjini Monaco. Uchina iliwazidi nguvu Simba wa Kenya kupata tikiti yao ya Olimpiki, na hivyo kumaliza matumaini ya Simba kufuzu kwa […]