WAZIRI WA ELIMU ATAMIA KUBADILI MFUMO WA AJIRA KATIKA SHULE ZA UMMA

Wizara ya elimu ninawazia kubadili jinsi ya kuwaajiri maafisa waasifu katika shule za umma ili kukabili ufisadi na matumizi mabaya ya raslimali za umma. Kwa mujibu wa Waziri wa elimu Ezekiel Machogu hali ya sasa ambapo wahasifu walioajiriwa na bodi za usimamizi wa shule wanatoa mwanya wa ufisadi na ubathirifu wa mali ya umma. Imetayarishwa na Janice Marete

RAILA AJIPIGIA DEBE KUWA MWENYEKITI WA AU HUKO ZANZIBAR

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ameendeleza kampeni za kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa umoja wa africa AU huko Zanzibar ambapo alihudhuria kongamano la mawaziri wa jumuiya ya afrika mashariki. Akizungumza katika kongamano hilo Odinga amesema kuwa afrika ina nafasi nyingi sana za kujiimarisha kiuchumi na vile vile kujiendeleza kama bara huku akishinikiza kupanuliwa […]

DAVJI ATELLAH; AKAUNTI YA KMPDU YA X IMEDUKULIWA

Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, nchini (KMPDU) Davji Atellah amesema kwamba akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa X imedukuliwa. Katika taarifa ya leo Jumatatu, Atellah amekanusha kusimamishwa kwa maandamano yao yaliyopangwa “Occupy MOH”. Ameongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kurejesha udhibiti wa akaunti hiyo. Imetayarishwa na Janice Marete

AULIWA BAADA YA KUMUUA MKEWE KWA SABABU YA SHILINGI 30

Maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa cha kusikitisha ambapo mzee wa miaka 60 anadaiwa kumdunga kisu na kumuua mkewe katika mzozo wa Sh30 katika kijiji kimoja Kaunti ya Siaya. Mwanamume huyo aliyetambulika kama Ben Odweso baadaye aliuawa na kundi la watu waliojawa na gathabu baada ya kisa hicho katika kijiji cha Nyalula. Alidaiwa kumdunga kisu na […]

EACC KUTOA USHAHIDI KATIKA KESI YA OBADO KUHUSU KESI YA UFISADI INAYOMKABILI

Mahakama ya Kupambana na Ufisadi EACC hii leo itaendelea kusikiza kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado, watoto wake na mawakili wake. Hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Victor Wakumile atasikiliza kesi hiyo. Washtakiwa hao wanane wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutenda uhalifu wa kiuchumi, mgongano wa kimaslahi, kujipatia mali […]

KMPDU YATANGAZA MIGOMO MPYA IKIWA MADAKTARI WANAGENZI HAWATAPEWA AJIRA

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU) umesitisha mpango wao wa kupiga kambi katika majengo ya Wizara ya Afya katika Kituo cha Afya House jijini Nairobi. KMPDU ilikuwa imetangaza mipango ya kupiga kambi katika majengo majengo hayo leo jumatatu, ili kuhakikisha kwamba madaktari wanagenzi wametumwa katika vituo vya afya kote nchini […]

CAS, WASHAURI WACHONGWA

Ni rasmi kwamba makatibu waandamizi ama CAS hawataajiriwa chini ya serikali ya sasa, rais William Ruto akiweka wazi kwamba hatua hiyo imechukuliwa kupunguza matumizi ya fedha za umma. Wengine ambao wameathirika ni washauri wa Rais ambao watapunguzwa kwa asilimia 50, saw ana kuondolewa kwa bajeti katika afisi za mke wa rais na Naibu wake, na […]

MASHIRIKA 47 YAVUNJWA

Kama njia mojawapo ya kubana matumizi ya fedha za umma baadaa ya kutupiliwa mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024, Rais William ruto ametangaza mikakati ambayo imechukuliwa na serikali, ikiwemo kuvunja mashirika 47 ambayo huendesha shughuli zinazofanana. Katika hotuba kwa taifa, Ruto amesema mashirika hayo hayajakuwa yakitengeneza faida, huku yakitumia mabilioni ya fedha za mlipa […]

MURKOMEN ALIIDHINISHWA KUTEKELEZA MRADI WA UHAMAJI MIJINI

Baraza la Mawaziri limempa Katibu wa Wizara ya Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen idhini ya kutekeleza Mradi wa Kuboresha Uhamaji Mijini nchini Kenya (KUMIP). Katika taarifa kwenye mtandao wa X Katibu wa Baraza la Mawaziri amesema kuwa mradi huo utahusisha kufufua Huduma ya Reli kwa Wasafiri na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa […]

RAIS RUTO KULIHUTUBIA TAIFA SAA SABA MCHANA

Rais William Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa saa saba alasiri ya leo. Kulingana na Katibu katika wizara ya mawasiliano ya Ikulu Emmanuel Talam, Rais atahutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi saa saba kabla ya mazungumzo ya Ruto X-Space na Gen Zs. Imetayarishwa na Janice Marete