X-SPACE YA RUTO NA GEN Z HAIJASHAURIWA –KIPRUTO ARAP KIRWA

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Kipruto Arap Kirwa amesema kuwa mpango wa Rais William Ruto wa kufanya mkutano katika mtandao wa wa X-Space na Gen Z sio ushauri sawa. Kwa mujibu wa Kirwa Rais lazima aache kuwa katikati ya kila jambo ambalo haliendi sawa nchini na Kusisisitiza kuwa lazima ajue kuwa hawezi kutatua kila changamoto inayoikabili […]

VITAMBULISHO, VYETI VYA KUZALIWA TAYARI KUCHUKULIWA

Wakenya waliotuma maombi ya kupata vitambulisho, Leseni za Kuendesha Magari Mahiri na Cheti cha Kuzaliwa wamehimizwa kutembelea Vituo vya Huduma center ili kuchukua stakabadhi zao. Katika notisi ya jana Ijumaa, Huduma Center ilifichua kuwa vitambulisho elfu 134,602 vya Kitaifa viko tayari kuchukuliwa katika Vituo vyote 53 vya Huduma center kote nchini. Vyeti vya kuzaliwa elfu […]

PESA ZA AFISI ZETU ZIKO WAPI? MCA BUNGOMA WALALAMA

Wawakilishi wa wadi wateuli katika bunge la kaunti ya Bungoma wanalalamikia hatua ya wabunge wa kaunti hiyo kuwanyima fedha za kuwaajiri wafanyikazi katika afisi zao licha ya fedha hizo kutengwa katika bajeti hatua ambayo kulingana nao imelemaza shughuli za maendeleo katika afisi zao. Imetayarishwa na Janice Marete

WATU 25 NDIO WALIAGA DUNIA 400 WAKIJERUHIWA; WAZIRI KINDIKI ASEMA

Waziri wa usalama na maswala ya ndani ya nchi prof Kithure Kindiki amepuuzilia mbali ripoti ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kwamba watu 49 waliaga dunia na wengine 600 kujeruhiwa. Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga humu nchini Kindiki amesema kuwa ni watu 25 pekee walioaga dunia na wengine 400 kujeruhiwa wakiwamo maafisa wa polisi 43. […]

KESI YA MBUNGE MBADI KUHUSU KUTUMWA KWA KDF KUAMULIWA LEO

Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi la Mbunge wa Suba Kusini John Mbadi na wengine wawili kushiriki katika kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria nchini Kenya kupinga kutumwa kwa maafisa wa kijeshi. Mbadi, Dkt James Nyikal na Wilberforce Ojiambo walitaka kuruhusiwa kujiunga na kesi hiyo kama wahusika wakisema wana ufahamu wa kina kuhusu jinsi utumwa huo […]

RUTO AZUNGUMZA NA MKUU WA IMF BAADA YA KUONDOA MSWADA WA FEDHA

Rais William Ruto amezungumza na Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva siku chache baada ya kuuondoa Mswada wa Fedha wa 2024 Mswada wa fedha uliojumuisha ongezeko la ushuru ulikuwa msingi wa mageuzi ya sera yaliyokubaliwa na nchi na IMF kama sehemu ya mpango wa ukopeshaji wa thamani ya dola bilioni 3.6. […]

SAKAJA AJITENGA NA UHUNI

Gavana wa naiorbi Johnson Sakaja, amepuzilia mbali madai kwamba alihusika katika kupanga njama ya kuchoma afisi za gavana zilizoko katika jengo la City Hall wakati wa maandamano ya kupinga serikali. Akiwahutubia wanahabari , Sakaja amesema kwamba amekuwa katika kaunti ya Mombasa na maafisa wake kufanya vikao kuhusu mwaka wa kifedha ambao umekamilika. Aidha, amesema kuwa […]

RUTO AKUTANA NA MAWAZIRI

Rais William Ruto anafanya kikao na baraza la mawaziri, wakati ambapo wengi wa mawaziri wake wanalaumiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao, mbali na kujihusisha na ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Kikao cha rais kimethibitishwa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed. Katika kikao cha seneti hapo jana, maseneta walitumia fursa hiyo kuwakosoa baadhi ya […]

NAFUU YA AFYA POKOT

Huduma za afya zinatarajiwa kuimarika katika kaunti ya West Pokot baada ya serikali ya kaunti hiyo kuboresha miundomsingi kwenye vituo mbali mbali vya afya. Nyingi za vituo hivyo ni vya maeneo ya mashinani, serikali ikisema hatua hiyo inalenga kupunguza gharama na changamoto za uchukuzi. Nao wakazi wa kaunti hiyo wameitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao […]

‘ALIYEMJERUHI’ POLISI AKAMATWA BONDO

Makachero wa idara ya upelelezi DCI wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kumshambulia afisa wa polisi wakati wa maaandamano ya kupinga mswada wa fedha katika eneo la Bondo kaunti ya Siaya Kulingana na DCI, mshukiwa huyo ambaye ametambuliwa kama Sostine Otieno alikuwa miongoni mwa wahalifu waliovamia kituo cha polisi cha Bondo wakiwa wamejihami na silaha butu ikiwa mawe […]