WANAFUNZI MILIONI 10 KUNUFAIKA NA MPANGO WA CHAKULA 2030

Wanafunzi zaidi ya milioni 10 wanatarajiwa kufaidika na mpango wa chakula kwa wote, ambao Wizara ya Elimu inapanga kuzindua ifikapo mwaka 2030. Kwa mujibu wa Katibu Msimamizi wa wizara hiyo, Florence Aboyit, mpango huo utaanza kutekelezwa mara baada ya kukamilika kwa sera itakayotoa mwongozo wa kisheria. Imetayarishwa na Janice Marete

MWANGAZA MAHAKAMANI AKIPINGA KUAPISHWA KWA GAVANA MPYA

Kawira Mwangaza amewasilisha rufaa akipinga kuapishwa kwa Mutuma kama Gavana wa Meru, akidai hakutendewa haki na Mahakama Kuu. Wakati huohuo, mwanaharakati Mike Makarina pia ameenda mahakamani akipinga uapisho huo, akisema umeharakishwa kinyume na utaratibu wa siku 10 baada ya kiti cha gavana kuwa wazi Imetayarishwa na Janice Marete

MSAJILI WA WATU AAGIZWA KUFIKA MBELE YA MAHAKAMA YA ELDORET

Familia mbili zinakinzana kuhusu umiliki wa shamba la ekari 30 lenye thamani ya KSh. 30 milioni huko Uasin Gishu baada ya kuwasilisha vyeti vya kifo vinavyokinzana, vikimtaja marehemu Philip Cherono na Paul Kibet Cherono kama wamiliki wa awali. Kutokana na mkanganyiko huo, Mahakama ya Eldoret imemwagiza Msajili Mkuu wa Watu kufika Julai 21 ili kutoa […]

HAKIMU STELLA ATAMBO APATA AFUENI YA MUDA

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kesi ya ufisadi dhidi ya Hakimu wa Thika, Stella Atambo, ikizingatia ombi la kupinga uhalali wa mashtaka hayo. Atambo, kupitia mawakili wake, amedai kesi katika Mahakama Kuu na mahakama ya chini zinahusu masuala tofauti. Chama cha Mahakimu na Majaji wa Kenya (KMJA) kimeonya kuwa uhuru wa mahakama uko hatarini, kikilaani […]

GAVANA MPYA WA MERU APISHWA

Isaac Mutuma M’Ethingia, ambaye amehudumu kama Naibu Gavana wa Kaunti ya Meru tangu mwaka wa 2022, sasa ameanza majukumu ya ugavana. Hii inafuatia kuondolewa madarakani kwa Gavana Kawira Mwangaza kupitia mashtaka ya Bunge la Seneti mwaka wa 2024, hatua ambayo ilidhibitishwa na uamuzi wa mahakama mnamo Machi 14, 2025. Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa […]

MAWAZIRI WA USALAMA WA SADC NA EAC WAKUTANA KUJADILI GHASIA DRC

Mawaziri wa Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaendelea na mkutano wa pili leo, wakijadili suluhisho la kudumu kwa ghasia zinazoendelea nchini DRC. Hii inajiri baada ya juhudi zao za awali za kutatua mzozo huo kwa njia ya kijeshi kushindwa kuleta matokeo yanayotarajiwa. Waziri wa Masuala […]

LUSAKA AONYA WAKULIMA DHIDI YA KUUZA PEMBEJEO ZA RUZUKU

Wakulima wa Bungoma wameonywa dhidi ya kuuza pembejeo za kilimo zilizopewa ruzuku na serikali ya kaunti badala ya kuzitumia ipasavyo. Gavana Kenneth Lusaka amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaopatikana wakikiuka mpango huo, ambao unalenga kusaidia wakulima wadogo wakati wa msimu wa upanzi. Aidha, amethibitisha kuwa maandalizi ya usambazaji wa pembejeo za bure kwa mwaka […]

CHELSEA YATELEZA KWA KICHAPO CHA 1-0 DHIDI YA ARSENAL

Chelsea ilipoteza 1-0 kwa Arsenal, ikiyumba katika mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa. Mikel Merino alifunga bao pekee dakika ya 20, akiipa Arsenal nafasi ya pili. Chelsea ilimkosa Cole Palmer na haikuweza kutengeneza nafasi nyingi. Licha ya kubaki nafasi ya nne, ina ushindani mkali kutoka kwa timu tano zilizo karibu. Mchezo ulikuwa na mashambulizi machache, […]

NEWCASTLE YASHINDA KOMBE LA LIGI KWA KUICHAPA LIVERPOOL 2-1

Newcastle ilishinda Kombe la Ligi baada ya kuilaza Liverpool 2-1, huku Dan Burn na Alexander Isak wakifunga mabao muhimu. Huu ni ushindi wao wa kwanza mkubwa tangu 1969 na taji lao la kwanza la ndani tangu 1955 ushindi ambao unajiri baada ya kupoteza fainali ya 2023 dhidi ya Manchester United. Kwa Liverpool, kichapo hiki ni […]

KENYA PIPELINE YAICHAPA KCB 3-1 KATIKA KENYA CUP

Kenya Pipeline iliichapa KCB seti 3-1 (27-28, 25-17, 25-17, 25-22) katika mechi ya uzinduzi wa Kenya Cup, katika uwanja wa Kasarani. Licha ya KCB kushinda seti ya kwanza 28-27, Pipeline ilirejea kwa nguvu na kushinda seti tatu mfululizo, ikihitimisha ushindi wake kwa 25-22 katika seti ya mwisho. Kocha Geoffrey Owino aliisifu timu yake kwa kurejea […]