MSHUKIWA WA NYAMA YA PUNDA AKAMATWA KIRINYAGA

Mshukiwa mmoja ametiwa mbaroni baada ya kunaswa kwa nyama ya punda wapatao 20 katika soko la Red Soil, eneo la Mwea Mashariki, Kaunti ya Kirinyaga na anatarajiwa kufikishwa mahakamani. Inadaiwa kuwa punda hao waliibwa na kuchinjwa kinyume cha sheria, kabla ya nyama hiyo kuanza kusafirishwa kuelekea soko la Kiamaiko, jijini Nairobi. Imetayarishwa na Janice Marete

MURKOMEN: MIZOZO YA ARDHI IMECHOCHEA UKOSEFU WA USALAMA

Kenya inakabiliwa na ongezeko la ukosefu wa usalama Kaskazini Mashariki kutokana na mizozo ya ardhi na mipaka, Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema. Akiwa Tharaka Nithi katika kongamano la Jukwaa la Usalama, Murkomen amesema mizozo hii imeenea katika kaunti nyingi na ni chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii. Aidha amehimiza utekelezaji wa ripoti ya Kikosi Kazi […]

KENYA KUNUFAIKA NA USHIRIKIANO MPYA NA MAREKANI

Kenya inatarajiwa kunufaika zaidi na ushirikiano wake na Marekani kufuatia mkutano wa ngazi ya juu kati ya Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta Marco Rubio, jijini Washington DC. Mazungumzo yao yamelenga kuimarisha usalama wa kikanda, kuharakisha mkataba wa biashara huru kati ya Kenya na Marekani, na kuunga mkono […]

RAIS RUTO ASAINI SHERIA MPYA YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Rais William Ruto amesaini Mswada wa watu wenye mahitaji maalum wa mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Ikulu, Nairobi. Amesema sheria hiyo ni hatua ya maendeleo inayothibitisha haki na utu wa watu hao, sambamba na Ibara ya 54 ya Katiba ya Kenya. Sheria mpya inapiga marufuku ubaguzi na kutaka mazingira ya umma, usafiri na teknolojia ya […]

ONG’ONDO: MAWAKILI WADAI DHULUMA DHIDI YA MSHUKIWA

Mawakili wa mfanyabiashara Philip Aroko anayezuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri kwa kuhusishwa na mauaji ya mbunge Ong’ondo Were, wameibua hofu ya haki za mteja wao kukiukwa, wakisema amezuiliwa bila mashtaka huku wakimzuia kukutana na mawakili, familia na marafiki zake. Katika hatikiapo ambayo imewasilishwa kwenye mahakama kuu, mawakili wakiongozwa na Danstan Omari wamesema juhudi […]

RISING STARS YAONDOLEWA KWA MASHINDANO YA AFCON

Rising Stars ya Kenya ilitoka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON) ikiwa na pointi moja baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Nigeria katika mechi ya mwisho ya Kundi B kwenye Uwanja wa June 30 mjini Cairo, Misri hapo jana. Kama kawaida, Kenya ilitangulia […]

ONG’ONDO: MFANYABIASHARA KUHOJIWA NA DCI

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanatarajiwa kumhoji mwanasiasa na mfanyabiashara wa kaunti ya Homa Bay Philip Nahason Aroko aliyewekwa korokoroni baada ya kuagizwa afike katika kituo chochote cha polisi kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were. Nahashon aliyejisalimisha katika makao makuu makuu ya DCI usiku wa kuamkia leo, […]

BASTOLA ILIYOTUMIKA KUMWUA MBUNGE WERE YANASWA

Uchunguzi katika kuwanasa waliohusika na mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were umepiga hatua kubwa, polisi wakitangaza kupata bunduki iliyotumika kutekeleza mauaji hayo ya wiki jana. Akiwahutubia wanahabari, Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amesema uchunguzi kuhusu matumizi ya bunduki umebainisha kwamba bastola iliyonaswa kutoka kwa mmoja wa washukiwa ndiyo iliyotumika. Ameongeza kuwa bastola […]

SHA YAINGIA GEREZANI

Serikali imeimarisha juhudi zake za kuhakikisha kila mkenya anasajiliwa chini ya bima ya afya ya kitaifa SHA, sasa ikianzisha zoezi la kuwasajili wafungwa katika magereza yote nchini. Zoezi hilo linajumuisha utoaji wa vitambulisho kwa wafungwa, limezinduliwa katika gereza la wanawake la Lang’ata, likiongozwa na makatibu Ouma Oluga wa afya, Belio Kipsang wa uhamiaji, Salome Beacco […]

PENDEKEZO LA MINONG’ONO

Viongozi kutoka eneo la Northrift wamepinga vikali mpango wa serikali kuiondoa kaunti ya Elgeyo Marakwet kwenye orodha ya maeneo yanayostahili wafanyakazi wa umma kulipwa fedha za ugumu wa mazingira, wakitaja mpango huo kuwa wa kusikitisha. Miongoni mwa viongozi hao ni mwakilishe wa kike wa kaunti hiyo Caroline Ng’elechei, mbunge wa Mogotio Reuben Kiborek na mwenzake […]