KINDIKI:DARAJA LA NITHI KUJENGWA KWA UFADHILI WA CHINA

Wakazi wa eneo la Nithi, Kaunti ya Tharaka Nithi, wanatarajiwa kunufaika na mradi wa ujenzi wa daraja la Nithi, ambao utaendeshwa na serikali kuu. Kwa mujibu wa Naibu Rais, Prof. Abraham Kindiki, serikali imekamilisha mipango ya kuanza ujenzi huo baada ya kupata ufadhili kutoka kwa serikali ya China. Imetayarishwa na Janice Marete

GACHAGUA AMLAUMU RUTO KWA KUKATAA NYACHAE KUWA MWENYEKITI WA IEBC

Mjadala kuhusiana na uteuzi wa mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wazidi kupamba moto, baada ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kudai kuwa Rais William Ruto alipinga uteuzi wa Charles Nyachae na badala yake kumchagua Erastus Ethekon. Gachagua amesema kuwa jopo la uteuzi lilikuwa limewasilisha majina ya Nyachae na Ethekon kwa […]

HUDUMA BORA ZA MAHAKAMA KUZINDULIWA KISUMU NA NYANZA

Wakazi wa Kisumu na maeneo ya Nyanza wanatarajiwa kunufaika na huduma bora zaidi za mahakama kufuatia uzinduzi wa huduma za pamoja za mabaraza ya usuluhishi (Tribunals Shared Services) unaotarajiwa kufanywa leo asubuhi na Jaji Mkuu Martha Koome, hafla ambayo imeratibiwa kufanyika katika ofisi za Lake Victoria South Water Works Development Agency, Nyalenda, kuanzia saa 9:30. […]

WEZI WA KUTUMIA NGUVU WATATU WAKAMATWA ATHI RIVER

Maafisa wa upelelezi eneo la Athi River wamewatia mbaroni washukiwa watatu wanaohusishwa na visa kadhaa vya wizi na wanatarajiwa kufikishwa mahakami huku polisi wakiendelea na juhudi za kuwatafuta washirika waliotoroka, huku mali zilizopatikana zikihifadhiwa kama ushahidi Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), waliokamatwa ni Kelvin Baraza Andayi almaarufu Kevoo, Titus Mutuku Maingi […]

ARSENAL YAKARIBIA KUFUZU LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE YA 2-2 NA LIVERPOOL

Arsenal walikubaliana na Liverpool kwa sare ya 2-2 baada ya kurudi kutoka nyuma kwa mabao mawili, wakijikatia tiketi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa. Liverpool waliongoza kwa mabao ya Cody Gakpo na Luis Diaz, lakini Gabriel Martinelli alifunga bao la kwanza la Arsenal, na Mikel Merino kusawazisha. Ingawa Merino alionyeshwa kadi nyekundu, Arsenal walishikilia sare muhimu […]

KINALE GIRLS YAIBUKA MABINGWA WA BLACK ROCK 7S

Kinale Girls yaibuka mabingwa wa Western Black Rock 7s kwa ushindi wa 14-7 dhidi ya St. Joseph Girls-Kitale ‘Joga’ Kinale Girls walitwaa taji la 10 la mashindano ya Western Black Rock 7s kwa kuishinda St. Joseph Girls-Kitale 14-7. Kate Elizabeth alifunga mabao mawili muhimu, akiwaletea ushindi baada ya St. Joseph kusawazisha 7-7 kipindi cha kwanza. […]

APS BOMET YAPANDA HADI NAFASI YA PILI

APS Bomet imepanda hadi nafasi ya pili kwenye Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza baada ya kuichapa Vihiga United 2-0, mabao yakifungwa na Daniel Odhiambo na Lawrence Kibet. Katika uwanja wa Serani, Mombasa United walirejea kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Luanda Villa kupitia mabao mawili ya Bakari Nyae na moja kutoka kwa Khamis Nyale […]

DEMBELE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGUE 1 BAADA YA KUIBUKA KINARA PSG

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligue 1 msimu huu, baada ya kuiongoza PSG kutwaa taji lao la 13 la Ufaransa na kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Dembele ndiye kinara wa mabao msimu huu akiwa na mabao 21 katika Ligue 1, na jumla ya mabao 33 katika mashindano yote, […]

Winter Tournament Wins: Inside the Seasonal Success Stories at Casino Seven

Winter Tournament Wins: Inside the Seasonal Success Stories at Casino Seven Holiday tournaments turn ordinary play into a festive challenge. Players chase larger prize pools, extra spins, and exclusive rewards. The excitement of a timed leaderboard adds a competitive edge that regular slots lack. During the winter months, many online casinos boost their offers with […]

SHUGHULI ZAVURUGIKA KWENYE KIWANDA CHA NZOIA KUFUATIA MAANDAMANO

Shughuli katika kiwanda cha sukari cha Nzoia zimetatizika baada ya wafanyakazi kuandamana kupinga ubinafsishaji wa kiwanda hicho. Wafanyikazi hao aidha wanasema kuwa hawatakubali usimamizi mpya kabla ya kulipwa mishahara yao yote, wakidai serikali inapuuza maslahi yao na sheria za ajira licha ya huduma yao ya muda mrefu. Inaarifiwa kuwa tayari serikali imekamilisha mchakato wa kubinafsisha […]