AFRIKA KUSINI YASHINDA U20, NIGERIA NAFASI YA TATU

Timu ya vijana ya Afrika Kusini chini ya miaka 20, Amajita, imeibuka mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Morocco 1-0 katika fainali iliyofanyika Misri Jana jumapili. Bao pekee lililofungwa na kiungo Gomolemo Kekana dakika ya 70 lilithibitishwa na VAR na likawa la ushindi. Timu zote […]

MVUA YAWAZIMA BANDARI NA LEOPARDS, WATOKA SARE TASA MBARAKI

Bandari na Leopards waligawana pointi katika sare ya 0-0 jana Jumapili katika Uwanja wa Mbaraki, Mombasa, katika mchezo ulioathiriwa sana na mvua iliyonyesha kwa muda mrefu. Pande zote mbili zilianza mchezo kwa tahadhari kwenye uwanja uliojaa maji, hali iliyobana kasi na ubora wa mchezo. Nafasi za kufunga zilikuwa chache katika kipindi cha kwanza, ambapo washambuliaji […]

POLICE FC WAZIDI KUIMARIKA, WAONGOZA LIGI KUU FKF KWA POINTI SITA

Police FC wamepiga hatua kubwa kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF baada ya kuifunga Talanta FC 1-0 na kuongoza kwa pointi sita huku wakibaki na mechi mbili. Ushindi huo ulisaidiwa na kipigo cha Tusker 7-1 kutoka kwa Sofapaka na sare ya Gor Mahia 0-0 na Murang’a Seal. David Simiyu alifunga bao pekee la Police […]

10 Winning Ways to Combine Football Fever and Live Casino Action at Ybets Online

10 Winning Ways to Combine Football Fever and Live Casino Action at Ybets Online Finding a casino that blends the excitement of football betting with the thrill of live dealer tables can feel like searching for a perfect match. Most players begin by scrolling through endless offers, hoping to spot the right mix of bonuses, […]

KPA KUONGEZA UWEZO WA BANDARI KWA TANI MILIONI 47

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini KPA inaendeleza mpango wa upanuzi na uboreshaji wa mabilioni ya dola ili kukidhi mzigo unaotarajiwa wa tani milioni 47 za shehena ndani ya miaka mitano. Mnamo mwaka wa 2024, KPA ilihudumia tani milioni 41.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.1% kutoka tani milioni 36.0 mwaka wa 2023. Muhimu katika […]

HATUA KUBWA YA AFYA MAKUENI

Wakazi wa kaunti ya Makueni wamepata afueni ya kusaka matibabu yanayohusu upasuaji, baada ya madaktari katiika kaunti hiyo kufanikisha upasuaji wa kwanza wa ubongo katika hospitali ya rufaa ya Makueni. Upasuaji huo ni hatua kubwa katika sekta ya afya, wakazi waliokuwa wakisaka huduma hizo katika hospitali za nje ya nchi wakitarajia kupunguza gharama za usafiri. […]

NEMIS NJE, KEMIS NDANI

Katika juhudi za kurahisisha shughuli za uhifadhi wa maelezo ya wanafunzi, serikali inapanga kuzindua mfumo mpya wa KEMIS unataochukua mahala pa mfumo wa sasa NEMIS. Kulingana na katibu mkuu katika wizara ya elimu Julius Bitok, mfumo huo utatekelezwa kwa awamu. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHERARGEI AKEJELI JUHUDI ZA UPINZANI

Uzinduzi wa vyama vipya vya kisiasa kwa lengo la kumbandua Rais William Ruto mamlakani kwenye uchaguzi mkuu ujao umepuziliwa mbali, baadhi ya viongozi wakisema kubuniwa kwa vyama hivyo ndiko hasa kutakakomfanikisha kuchaguliwa tena. Akizungumza na wanahabari, seneta wa Nandi Samson Cheragei ambaye ni mwandani wa Rais Ruto, amesema vyama hivyo vinakosa sura ya kitaifa. Imetayarishwa […]

ULINGO WA SIASA WAPATA MGENI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amezindua chama kipya cha Democracy for the Citizens Party DCP, anachopanga kukitumia kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Gachagua amesema anapanga kuzuru taifa zima akikusanya maoni ya wakenya kabla ya kuandika manifesto ya chama chake kipya. Kinara wa chama hicho ni Gachagua mwenyewe, kaimu naibu […]

EPRA: BEI ZA MAFUTA KUBAKI SAWA KWA MIEZI MITATU MFULULIZO.

Halmashauri ya Kudhibiti Bei za Bidhaa za Petroli (EPRA) imetangaza kuwa bei za mafuta zitasalia bila mabadiliko kwa mwezi wa tatu mfululizo. Kupitia taarifa rasmi, EPRA imesema kuwa imeendelea kutumia hazina ya ustahimilivu wa bei ili kuzuia ongezeko la gharama ya bidhaa hizo. Hii ina maana kuwa kuanzia usiku wa kuamkia leo, bei ya petroli […]