GOR YAACHILIA WACHEZAJI WAKE

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amesema wazi kwamba watawaachilia wachezaji ambao kandarasi zao zimeisha, akifichua hawataongeza kandarasi zao. Rachier aliongeza kuwa pia watawaachilia wachezaji walioshuka viwango, kuanzia na wenye kutotumika sana na wenye kukosa uthabiti. Mwenyekiti huyo wa muda mrefu alisema hayo jana baada ya kutimua benchi zima la ufundi kufuatia matokeo mabaya ya […]

KIKOSI CHA CHATAJWA

Kocha mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy ametangaza kikosi chake cha muda kwa ajili ya Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika (CHAN) ambayo ni ya kipekee kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani. Wanaoongoza kwa mashambulizi ni wafungaji bora wa ligi kuu iliyokamilika majuzi, Moses Shuma, Emmanuel Osoro na Ryan Ogam, ambao wametikisa nyavu mara […]

AMIN ATARAJIWA KUMWASILISHA NDIANGUI MAHAKAMANI

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI Mohammed Amin anatarajiwa kuviongoza vitengo vya usalama kumwasilisha mahakamani bloga Ndiangui Kinyagia mahakamani katika hali yoyote ile, baada ya mahakama kumwagiza Amin amfikishe bloga huyo mahakamani hii leo. Kwenye uamuzi wake Jumanne wiki hii, jaji Chacha Mwita alimwagiza Amin amfikishe Kinyangia mahakamani au mwili wake kabla ya […]

MCAS 2 WA MAKUENI KUFIKA MBELE YA DCI ALHAMISI

Idara ya usalama imezidisha msako dhidi ya wanasiasa wanaoaminika kufadhili vurugu na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya vijana wiki jana, wawakilishi wadi wawili katika kaunti ya Makueni wakiwa miongoni mwa watu wanaochunguzwa. Wawili hao ambao ni Albanus Wambua na Francis Mutuku wameagizwa kufika katika makao makuu ya DCI hii leo, baada yao […]

RUTO AKAANGWA NA MASWALI UGHAIBUNI

Rais William Ruto amekuwa na wakati mgumu kueleza ni kwanini taifa liko katika kampeni mara kwa mara licha ya kuwapa kwa muda mrefu kabla ya uchaguzi kufanyika Katika kikao na wakenya wanaoishi nchini Uingereza ambako Rais amekuwa ziarani, wakenya hao wameelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa taifa kujikokota kimaendeleo kutokana na kampeni hizo. Rais hata hivyo […]

WATOTO MILIONI 20 KUPEWA CHANJO DHIDI YA TYPHOID

Serikali inalenga watoto milioni 20 kote nchini katika kampeni ya kutoa chanjo ya kuzuia homa ya matumbo yaani typhoid pamoja na ugonjwa wa ukambi na surua. Mkurugenzi wa afya Dkt Patrick Amoth anasema chanjo hiyo itatolewa kwa watoto walio kati ya miezi 9 hadi miaka 14. Imetayarishwa na Maureen Mukhobe

KUPPET KUANZA MAZUNGUMZO NA TSC

Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo anuai cha Kuppet kitaanzia mazungumzo na tume ya kuwaajiri walimu Tsc kuhusu mkataba mpya wa mwaka wa 2025 hadi mwaka wa 2029. Katibu wa kuppet Akelo Misori amewataka wanachama wake kuwa na subira wanapoanzisha majadiliano hayo na waajiri wa walimu baada ya kukamilika kwa mkataba uliokuwepo […]

MBAPPE ATAKUA TAYARI KWA ROBO FAINALI

Kocha wa Real Madrid Xabi Alonso alisema Kylian Mbappe anakaribia kuwa fiti kamili kabla ya robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya timu yake kuiondoa Juventus 1-0 katika hatua ya 16 bora Jumanne. Mbappe alicheza mechi yake ya kwanza iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu katika michuano hiyo kama mchezaji wa akiba katika […]

MOFA YAACHANA NA KOCHA LLYOD

MOFA FC imetangaza kuachana na kocha mkuu Lloyd Wahome baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa muda mfupi. Klabu hiyo ilithibitisha habari hizo katika taarifa ya Jumanne, ikimshukuru mtaalamu huyo kwa utumishi wake. Wahome, ambaye hapo awali aliwahi kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Murang’a Seal FC, alirejea kwa mara yake ya pili MOFA mwezi […]

JERAHA LILINIKOSESHA KIATU CHA DHAHABU 

Mshambulizi wa Bungoma Queens, Catherine Khaemba anadai alikosa Kiatu cha Dhahabu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF 2024/25 kutokana na jeraha. Khaemba alikuwa akiongoza orodha ya wafungaji katika mkondo wa kwanza wa ligi kabla ya kukosekana kwa sababu ya jeraha la mguu, ambalo lilitoa fursa kwa fowadi wa Police Bullets, Rebecca […]