KENYA KUANDAA PARA VOLLEY

Kenya iko tayari kuandaa Mashindano ya Para Volley Africa 2025 yanayoanza Jumamosi hii katika uwanja wa ndani wa Kasarani, huku zaidi ya nchi 10 zikitarajiwa kushiriki. Kwa mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, timu ya wanaume ya Kenya itapata fursa adimu ya kufukuzia ubingwa wa bara katika ardhi ya nyumbani, na Kocha Mkuu […]

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

Faith Mboya, mshambulizi wa klabu ya Kibera Soccer Women, anajivunia kushinda taji la kombe la shirikisho la FKF na pia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya kina dada, katika msimu wake wa kwanza na timu hiyo. Mboya hana shaka kwamba angeibuka mfungaji bora iwapo angeshiriki ligi hiyo […]

MURUNGA AKASHIFU MIZOZO YA RAGA

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Kenya Harlequins Paul ‘Pau’ Murunga amekashifu mizozo ya uongozi inayokebehi Muungano wa Raga ya Kenya akisema ni matokeo ya ubinafsi na uchoyo. Pau hakughairi maneno yake alipokuwa akitoa tathmini kali kwa bodi ya sasa ya wakurugenzi wa Muungano huo, akisema wengi wao wamekaa kupita kiasi katika nyadhifa zao. Mchezaji […]

NITABADILISHA AFC ASEMA AMBANI

Mwenyekiti mpya wa AFC Leopards, Boniface Ambani anasema anataka kukumbukwa kama kiongozi aliyekuja na kubadilisha mambo makubwa kwa manufaa ya timu, kufikia wakati atakapokuwa akipeana uongozi miaka ya baadaye. Ambani anatarajiwa kuchukua wadhifa huo rasmi leo kutoka kwa mwenyekiti anayemaliza muda wake Dan Shikanda, kufuatia kuchaguliwa kwake Jumapili iliyopita. Ambani ameapa kuhakikisha Leopards inasikika kwenye […]

MAHAKAMA ELDORET KUMHUKUMU ALIYEKIRI KUWAUA WATOTO 5

Mahakama kuu ya Eldoret imeratibiwa kutoa hukumu hapo kesho dhidi ya Evans Juma Wanjala, mshtakiwa aliyekiri kutekeleza mauaji dhidi ya watoto 5 katika eneo la Moi’s Bridge kaunti ya Uasin Gishu. Hii ni baada ya jaji Reuben Nyakundi kumpata na hatia ya kutekeleza unyama huo dhidi ya watoto hao wa kati ya umri wa miaka […]

BLOGA NDIANG’UI APATIKANA

Bloga Ndiang’ui Kinyagia, aliyeripotiwa kutoweka yapata wiki 2 zilizopita, amewasiliana na familia yake na kuthibitisha kwamba yuko hai na salama. Kulingana na taarifa ya wakili wa familia yake Wahome Thuku, Kinyagia aliwasiliana na mwanafamilia Jumanne jioni ila hakufichua alikokuwa, akifichua kuwa alielekea mafichoni baada ya kubaini kuwa alikuwa akitafutwa na maafisa wa DCI. Haya yanajiri […]

HATUMTAKI DIAZ WAEMA LIVERPOOL

Liverpool wamekataa ombi rasmi kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji Luis Diaz. Mkurugenzi wa spoti wa Bayern Max Eberl amefahamishwa kuwa klabu hiyo ya Premier League haina nia ya kumuuza Diaz na haitaingia kwenye majadiliano ya mshambuliaji huyo. Diaz, 28, alikabiliwa na hali kama hiyo kutoka kwa Barcelona mapema msimu jana lakini […]

BAENA AJIUNGA NA ATLETICO MADRID

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Alex Baena amesajiliwa na Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitano, klabu hiyo ya La Liga ilitangaza Jumatano. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anawasili kutoka Villarreal kwa ada ambayo haijawekwa bayana, ingawa vyombo vya habari vya Uhispania vinaripoti kuwa dili hilo linaweza kufikia karibu euro milioni 50 ($58.8 […]

PEDRO ASAJILIWA NA CHELSEA

Joao Pedro amekuwa mshambuliaji wa 18 kusajiliwa na Chelsea kwa zaidi ya miaka mitatu chini ya wamiliki wao wa sasa. Anajiunga kutoka Brighton katika mkataba wa thamani ya Ksh 10.6 bilioni (£60m), akichukua jumla ya matumizi yao kwa washambuliaji katika kipindi hicho hadi Ksh 99.3 bilioni (£560m.) Na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 […]

RANGERS WASALIA KWA LIGI KUU

Posta Rangers wamehifadhi nafasi yao ya Ligi Kuu ya FKF (FKFPL) licha ya kupokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Naivas FC katika mkondo wa pili wa mchujo wa kupanda daraja/kushuka daraja uliochezwa mjini Murang’a. Wanabarua hao walishikilia faida ya jumla ya 2-1, baada ya kupata ushindi wa 2-0 katika mkondo wa kwanza mjini Thika wikendi […]