TIMU YA KENYA YAJIANDAA KWA MICHEZO ZA UFUKWENI

Timu ya Kenya ya soka ya ufukweni inajiandaa kwa wakati mkali huku nchi hiyo ikijiandaa kuandaa michuano ya CECAFA Beach Soccer 2025 mjini Mombasa. Baada ya kuahirishwa mara mbili kunakochangiwa na masuala ya vifaa, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) sasa limethibitisha kuwa michuano hiyo itafanyika kuanzia Julai 16 hadi 20, […]

TUPE MUDA TUTOE UAMUZI

Jopo linalokagua kesi ya rufaa iliyowasilishwa na Shule ya Upili ya Kakamega dhidi ya timu ya soka ya Shule ya Upili ya Musingu limeomba muda zaidi wa kuchunguza kesi hiyo kabla ya kutoa uamuzi wake. Haya yanajiri kufuatia kuwasilishwa kwa ushahidi wa maandishi na walimu wa Kakamega High, wakiongozwa na Mwalimu Mkuu Julius Mambili, wakidai […]

TUNA UWEZO WA KUCHEZA KITAIFA ASEMA MANAKA

Kocha mkuu wa Ebwali Nickson Manaka amewahakikishia mashabiki kuwa kikosi chake kina uwezo wa kurejea katika michuano ya soka ya kitaifa ya shule za upili licha ya changamoto ambazo timu hiyo imekuwa ikikabiliana nayo mwaka huu. Manaka ambaye timu yake ilikuwa na kibarua kizito kwenye hatua ya kata, baada ya kufungwa bao 1-0 na Kisangula […]

BANDARI WAJIVUNIA WACHEZAJI KUJIUNGA NA HARAMBEE STARS

Bandari FC kwa mara nyingine tena itakuwa na uwakilishi mkubwa katika ngazi ya taifa, huku nyota wake watano wakiitwa kwenye kikosi cha awali cha Harambee Stars kabla ya michuano ya CHAN 2025. Wanaoongoza ni mshambuliaji Beja Nyamawi, akiungana na kipa mzoefu Farouk Shikalo, mabeki Siraj Mohammed na Swaleh Pamba, pamoja na kiungo mbunifu David Sakwa. […]

HARAMBEE STARS KUSHIRIKI MASHINDANO YA CECAFA

Harambee Stars itashiriki Kombe la Mataifa Nne la CECAFA linalotarajiwa kuchezwa Julai 24-27 kwenye Uwanja wa Karatu jijini Arusha-Tanzania. Michuano hiyo itatumika kama jukwaa muhimu la maandalizi kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika ya 2024 (CHAN), ambayo inatazamiwa kuandaliwa Afrika Mashariki mnamo Agosti. Shindano hilo la timu nne huleta pamoja washindani wa kikanda Kenya, […]

BLOGA ALBERT OJWANG KUZIKWA TAHARUKI IKITANDA

Mazishi ya bloga na mwalimu Albert Ojwang yameratibiwa kufanyika hii leo katika kijiji cha Kokwanyo kaunti ya Homa Bay huku taharuki ikiwa imetanda, baada ya waombolezaji kuvamia na kuteketeza kituo cha polisi cha Mawego ambako Ojwang aliwasilishwa mara ya kwanza alipokamatwa kabla ya kifo chake. Waombelezaji hao wakiwemo wanafunzi wa chuo kimoja cha kiufundi eneo […]

KINDIKI AENDELEZA KAMPENI ZA MICHANGO

Naibu rais Kithure Kindiki ameendeleza kampeni zake na kuchangisha fedha kwa makundi ya akina mama, akidai anawapa uwezo wa kifedha. Kindiki ameratibiwa kuzuru kaunti ya Kilifi hii leo, baada ya mikutano sawa katika kaunti ya Taita Taveta hapo alikokuwa ameandamana na viongozi mbali mbali akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula. Wameendelea kuwashutumu viongozi […]

UPINZANI KUKAMILISHA ZIARA YA MAGHARIBI

Viongozi wa upinzani wameratibiwa kukamilisha ziara yao ya siku 2 katika eneo la Magharibi mwa nchi hii leo, ambako wamekuwa wakiwataka wakazi wa eneo hilo kuwaunga mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao. Miongoni mwa viongozi hao ni Rigathi Gachagua wa DCP, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Eugene Wamalwa wa DAP-K na aliyekuwa waziri wa usalama Fred Matiang’i, […]

NYOTA WA LIVERPOOL JOTA AUAWA KATIKA AJALI YA GARI!

Mshambulizi wa Liverpool, Diogo Jota amefariki dunia kufuatia ajali ya gari nchini Uhispania akiwa na umri wa miaka 28. Jota aliripotiwa kuwa alikuwa akisafiri kwa gari na kaka yake Andre, ambaye pia ni mwanasoka mwenye umri wa miaka 26, wakati gari hilo lilipotoka nje ya barabara. Tukio hilo lilitokea kwenye A-52 katika jimbo la Zamora, […]

BILA BILION KUMI NA MBILI EZE HAONDOKI

Crystal Palace haitafikiria kumuuza Eberechi Eze kwa punguzo la Shilingi bilioni 12 kifungu cha kutolewa kwenye mkataba wa mchezaji huyo, gazeti la The Mirror limeripoti. Haya yanajiri huku Arsenal ikionyesha nia ya kumnunua kiungo huyo, ambaye sasa anaibukia kama shabaha kubwa ya klabu hiyo katika dirisha hili. Eze amefurahishwa na uwezekano wa kuhamia kwa wababe […]