TUSKER WAILEMEA KCB, WAPANDA HADI NAFASI YA SITA

Tusker FC walionyesha ukomavu na nidhamu ya hali ya juu kuibuka naushindi wa 2-1 dhidi ya KCB katika mechi ya Ligi Kuu ya Kenyailiyochezwa kwenye uwanja wa Kasarani Annexe. Ushindi huouliwawezesha Brewers kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamowa ligi wakiwa na pointi 27, pointi tisa nyuma ya vinara Gor Mahia. Tusker walilazimika kuvumilia presha […]

KIMANZI ASIFU UJUMUISHWAJI WA MICHEZO KATIKA CBE

Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars Francis Kimanzi amepongezauamuzi wa serikali wa kujumuisha michezo kama shughuli ya ziada yamasomo chini ya mfumo wa Competency-Based Education (CBE),akisema ni hatua muhimu kuelekea mafanikio ya muda mrefu yamichezo nchini. Kimanzi amesema kuwepo kwa mipango ya michezo iliyoandaliwavyema shuleni kutaboresha utambuzi na ukuzaji wa vipaji mapema,na kuhakikisha wanariadha chipukizi wanalelewa […]

RUTO ASIFIA CHAMA CHA UDA

Rais William Ruto amesema chama cha uda kinajiimarisha kuhakikisha kinapata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.  Ruto amesema kuwa ushirikiano wa chama cha UDA na ule wa odm kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 unalenga kuzoa ushindi wa kura milioni tatu dhidi ya wapinzani wa mrengo huo. Aidha Rais ametangaza kwamba uchaguzi wa chama hicho […]

KRA, KPA WAZINDUA MAGEUZI KUPUNGUZA MSONGAMANO BANDARINI MOMBASA

Mamlaka ya kukusanya ushuru, KRA, na Mamlaka ya Bandari ya Kenya, KPA, wamezindua mageuzi mapana ya pamoja yanayolenga kupunguza msongamano katika Bandari ya Mombasa, kupunguza muda wa kukaa mizigo na kuharakisha mchakato wa kuidhinisha. Marekebisho hayo yamefanyika huku kukiwa na msongamano wa umeme kwenye bandari ambao umetatiza uagizaji wa bidhaa, mauzo ya nje na biashara ya kikanda. Hatua hizo […]

RUKU: GACHAGUA ANAJISHAMBULIA

Mashambulizi dhidi ya ibada ya kanisa iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua katika eneo la Othaya kaunti ya Nyeri hapo jana yameendelea kuibua hisia mesto, baadhi ya viongozi wakimshutumu Gachagua kuhusiana na mashambulizi hayo. Wa hivi punde ni Waziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku, anayedai kuwa Gachagua alipanga vurugu hizo ili kujiwasilisha […]

MABWENI 3 YATEKETEA MATUNGULU BOYS

Polisi katika kaunti ya Machakos wanachunguza mkasa wa moto uliozuka katika shule ya wavulana ya Matungulu usiku wa kuamkia leo na kuteketeza mali ya thamani isiyojulikana. Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya upili Joseph Makau, amesema miongoni mwa majengo yaliyoathirika ni mabweni 3 na mali nyingine iliyokuwa ndani ya mabweni hayo. Kulingana naye, huenda wanafunzi […]

ARSENAL WATIWA PANCHARI NA UNITED

Manchester United waliwatia breki Arsenal katika azma ya kusaka taji la EPL baada ya zaidi ya miaka 20, kufuatia kichapo cha mabao 3-2 ugani Emirates jana jioni. Arsenal waliochukua uongozi kutokana na bao la kujifunga la Lisandro Martinez, walikosa kufunga mabao na kujihakikishia ushindi licha ya kutamalaki na kutishia kila mara katika dakika za ufunguzi. […]

LEOPARDS WAREJEA KILELENI

AFC Leopards waliendeleza azma yao ya kutwaa taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL, kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sofapaka hapo jana uwanjani Kasarani. Ushindi wa Ingwe ambao unawaweka pointi 36 sawa na mahasimu wao wa jadi Gor Mahia, ulijiri siku moja baada ya Gor kutoka chini bao 1-0 na kuvuna […]

NAIROBI UNITED WAJIKAANGA CAF

Masaibu ya klabu ya Nairobi United katika kombe la mashirikisho, CAF Confederations yameendelea baada ya kupokezwa kichapo cha 3 mfululizo baada ya kucharazwa mabao 2-1 na Azam FC ya Tanzania hapo jana. Naibois waliopoteza 3-1 dhidi ya Wydad Casablanca na 1-0 dhidi ya AS Maniema ya DR Congo kwenye mechi za ufunguzi za Group B […]

MPASUKO ZAIDI ODM

Tofauti za kisiasa zimeendelea kujitokeza katika chama cha ODM hasa kuhusiana na ushirikiano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kinara wa chama hicho Oburu Oginga akisisitiza kuwa ODM itafanya mazungumzo na UDA ili kubuni muungano wa kisiasa. Hata hivyo, kundi la viongozi likiongozwa na gavana wa Siaya James Orengo na katibu mkuu Edwin Sifuna, wamekariri […]