NG’ENO, WENGINE 5 KUPEWA BURIANI

Miili ya watu 6 walioangamia kwenye ajali ya ndege kaunti ya Nandi akiwemo mbunge wa Emurua Dikirr kaunti ya Narok Johana Ng’eno, itasafirishwa leo hii kwa ibada ya pamoja katika shule ya msingi ya Emurua Dikirr ambako pia wakazi watapata fursa ya kuitazama kabla ya mazishi hapo kesho. Ibada ya leo inajiri baada ya nyingine […]

ODM: HAKUNA MAKATAA YA RIPOTI

Chama cha ODM kimetetea kinachoonekana kuwa kucheleweshwa kwa uwasilishaji wa ripoti kuhusu utekelezaji wa ajenda 10 zilizoafikiwa baina yake na UDA ikiwemo kuwapa fidia waathiriwa wa maandamano, kikisema hakuna makataa kuhusu uwasilishwaji huo. Kwa mujibu wa baraza kuu la chama hicho likiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Gladys Wanga, mchakato huo ni endelevu na hauna muda […]

MOSHI WA MAKOMBORA UARABUNI WACHEMUA KENYA

Athari za mapigano yanayoendelea katika ukanda wa Mashariki ya kati zimeanza kujitokeza katika sehemu mbali mbali za dunia, wafanyabiashara wa hapa nchini wanaouza nyama, majani chai na maua katika ukanda huo wakisema wamepata hasara ya mamilioni ya pesa tangu kuzuka kwa mapigano hayo. Kwa mujibu wa wafanyabishara hao, hasara hiyo imetokana na kusitishwa kwa safari […]

MGAWANYIKO UTAKAOMWOKOA SAKAJA

Huenda hoja ya kubanduliwa kutoka mamlakani kwa gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ikakosa kufaulu kutokana na migawanyiko miongoni mwa wawakilishi wadi katika bunge la kaunti hiyo, wawakilishi walio upande wa serikali jumuishi wakijitenga na azma hiyo. Wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi Peter Imwatok, wawakilishi wadi hao zaidi ya 70 wamesema mswada huo utatatiza utoaji […]

SHERIA YAWAGAWANYA WABUNGE

Wabunge wamechukua misimamo kinzani kuhusiana na sheria ya kuanzishwa kwa hazina ya kitaifa ya miundombinu inayopendekezwa ya mwaka 2025 kwa lengo la kuanzisha hazina ya kufadhili miradi mikubwa iliyoidhinishwa na baraza la mawaziri kama sehemu ya kuokoa uchumi. Wabunge wa upande wa serikali akiwemo Owen Baya wa Kilifi North na Silvanus Osoro wa South Mugirango, […]

MGOMO WA MADAKTARI MOMBASA WASITISHWA

Maafisa wa Union KMPDU wakiongozwa na Katibu Mkuu Davji Atellah, wamesitisha mgomo wa madaktari katika kaunti ya Mombasa hatua inayokuja baada ya mazungumzo ya saa nne yaliyofanyika katika ofisi ya Gavana wa Mombasa. Uamuzi huo umefikiwa kufuatia kikao kati ya viongozi wa muungano huo na Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir, ambapo pande zote zilijadili masuala yaliyokuwa […]

NYUTU AKANUSHA MADAI YA SIFUNA KUJIUNGA NA DCP.

Seneta wa Murang’a Joe Nyutu amekanusha madai kwamba Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna atakighura chama cha ODM na Kujiunga na chama cha DCP. Akizungumza katika mahojiano na Kituo kimoja cha runinga humu nchini, Nyutu amesema kuwa Kiongozi wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua alitoa tu mwaliko kwa sifuna kufuatia mzozo uliopo kwenye chama cha ODM. […]

ICHUNG’WA AMUENZI JOHANA NG’ENO

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung’wa, amemuenzi marehemu Johana Ng’eno akimtaja kama mwanasheria mahiri aliyetoa mchango mkubwa katika masuala ya kisheria ya Bunge. Ichung’wa amesema Ng’eno alikuwa akishiriki kikamilifu katika mashauri ya kisheria, akiwashauri mawakili waliokuwa wakilitetea Bunge mahakamani kuhusu namna bora ya kuendeleza hoja zao. Ichung’wa ameongeza kuwa historia ya mageuzi […]

NAYIANOI NG’ENO: NIMEPOTEZA MUZIKI WA UJANA WANGU

Naiyanoi Ntutu Ng’eno, mke wa marehemu Mbunge Emurua Dikirr Johana Ng’eno, ameomboleza mumewe kama mtu aliyejitolea kuipenda na kuilinda familia yake. Naiyanoi amesema kwamba mumewe alikuwa na hamu ya kukuza uhusiano wao na wa watoto wao wawili, akikumbuka kumbukumbu za siku zao za mwanzo katika ndoa. Alikuwa akizungumza wakati wa ibada ya waathiriwa sita miongoni mwao Mbunge Ng’eno , waliofariki […]

AFRIKA MASHARIKI YAKADIRIA HASARA WENYE MELI WAKISITISHA SAFARI UARABUNI

Kampuni mbali mbali za usafiri wa meli za mizigo zinazohudumia Afrika Mashariki zimetangaza usumbufu katika usambazaji wa bidhaa kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israeli na mshirika wake Marekani dhidi ya Iran, zikibainisha kuwa yameanzisha gharama zinazohusiana na hatari katika shughuli zao. Katika ushauri,kampuni hizo zimetangaza kwamba zinasimamisha shughuli zote za mizigo inayokwenda Mashariki ya Kati, na meli ambazo tayari ziko katika maeneo yaliyoathiriwa […]