SWAZURI NA WENZAKE WAACHILIWA HURU KWENYE KESI YA ARDHI

Mahakama ya hakimu imemuachilia huru aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi, Mohammed Abdalla Swazuri, pamoja na washitakiwa wengine kadhaa katika kesi ya ardhi iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu. Watu 17 walikuwa wakishtakiwa kwa njama na fidia isiyo halali ya ardhi ya Shirika la Reli la Kenya yenye thamani ya shilingi milioni 221. Katika uamuzi […]

UTOAJI WA VITAMBULISHO WAONGEZEKA NCHINI

Serikali imeripoti ongezeko la utoaji wa vitambulisho vya kitaifa, ikisisitiza umuhimu wake katika utambuzi wa raia na upatikanaji wa huduma muhimu. Zaidi ya vitambulisho milioni 4.1 vimetolewa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, huku milioni 1.6 vikitolewa katika miezi sita iliyopita, sambamba na kuanzishwa kwa mfumo mpya ulio salama na wenye uwajibikaji zaidi. Kwa mujibu […]

WAWEKEZAJI WAKUTANA NCHINI HUKU MAPATO YA MITAJI YA KIGENI YAKIONGEZEKA  

Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Kenya (KIICO) umefunguliwa rasmi mjini Nairobi, huku viongozi wakitia saini mikataba ya uwekezaji yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 2.9 za Marekani, ambazo zinatarajiwa kuzalisha zaidi ya ajira 63,000 za moja kwa moja nchini Kenya. Mkutano huo wa siku tatu umefunguliwa kwa pamoja na Rais William Ruto na Rais […]

WANGA AKANA LINDA MWANANCHI

Wakati uo huo, mwenyekiti wa kitaifa wa ODM Gladys Wanga, amepinga madai kwamba chama hicho kimegawanyika kwenye makundi mawili, akisema vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna halina uhusiano na ODM. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Wanga amesema ODM iko imara, na kwamba matayarisho ya kongamano la kitaifa la wajumbe […]

SIFUNA KUFAHAMU HATMA YAKE YA KUFURUSHWA LEO

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, atafahamu hatima yake hii leo kuhusiana na kutimuliwa kutoka wadhifa huo, kwenye uamuzi ambao utatolewa leo na jopo la kushughulikia mizozo ya vyama vya kisiasa nchini. Jopo hilo awali lilitoa agizo la kuzuia kwa muda utekelezaji wa uamuzi wa baraza kuu la ODM kumfurusha Sifuna kama katibu […]

ITALIA WAAZIMIA KUKATA KIU CHA KOMBE LA DUNIA KWENYE MWONDOANO

Timu ya taifa ya soka ya Italia inaazimia kumaliza kijibaridi cha kukaa nje ya kombe la dunia kwa miaka 12, inapoingia katika awamu ya mwondoano ili kusaka tiketi ya kipute hicho muhimu zaidi katika ulimwengu wa soka. Italia wataikaribisha Northern Ireland katika eneo la Bergamo, katika kinachotarajiwa kuwa semi fainali yenye ushindani wa hali ya […]

AFCON 2025: CAS YATHIBITISHA KUPOKEA RUFAA YA SENEGAL

Mahakama ya usuluhishaji wa migogoro ya michezo, CAS, imethibitisha kupokea rufaa kutoka kwa timu ya taifa ya Senegal inayolenga kubatilisha uamuzi wa kupokonya ubingwa wa AFCON 2025. Shirikisho la soka barani Afrika, CAF, lilitangaza uamuzi huo tarehe 17 mwezi huu wa kuwapokonya Senegal ubingwa na kuwavika Morocco, miezi 2 baada ya kukamilika kwa fainali iliyokumbwa […]

RISING STARLETS MBIONI KUFUZU FIFA U17

Timu ya taifa ya chipukizi ya wanawake, Rising Starlets, imeingia kambini kwa matayarisho ya mechi za kufuzu mashindano ya kombe la dunia kwa wachezaji wa umri usiozidi miaka 17, yaani FIFA World Cup U17. Kenya itachuana na Namibia tarehe 12 mwezi ujao kwa mkondo wa kwanza nchini Namibia, kabla ya marudiano wiki moja baadaye jijini […]

MAKACHERO WAZIMA JARIBIO LA UJAMBAZI KITENGELA

Idara ya upelelezi wa jinai, DCI, amezima jaribio la wizi lililokuwa likimlenga afisa wa ngazi ya juu wa jeshi, na kuwakamata washukiwa 6 mtaani Kitengela, ikisema jaribio hilo liliwahusisha maafisa wa jeshi, KDF, na raia. Kupitia taarifa, DCI imesema operesheni yao ilitokana na taarifa za kijasusi zilizopokelewa Jumatatu kuhusiana na mpango wa ujambazi, na kwamba […]

WANANCHI WATEKETEZA LORI KAKAMEGA BAADA YA AJALI

Polisi wameanzisha uchunguzi katika tukio ambapo umma wenye ghadhabu umeliteketeza lori la kusafirisha bidhaa za sukari katika eneo la Khu Msalaba kaunti ya Kakamega, baada ya lori hilo kudaiwa kumgonga na kumwua mwanafunzi wa grade 6 eneo hilo. Kulingana na OCPD wa Ikolomani Maasai Makau, amesema mvulana huyo alikuwa akirejea nyumbani kutoka shuleni alipogongwa na […]