GOR WAPIGWA JEKI LIGINI WANAPOSAKA UBINGWA

Viongozi wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Gor Mahia, wamepigwa jeki katika juhudi zao za kusaka ubingwa wa ligi hiyo msimu huu, kufuatia kurejea kwa mshambulizi wao Felix Mboya aliyekuwa amekaa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha. Mshambulizi huyo wa timu ya taifa Harambee Stars amekuwa nje kwa miezi kadhaa baada ya kufanyiwa […]

SERIKALI YAFICHUA WAKENYA WALIOUAWA URUSI

Imeripotiwa kuwa wakenya wasiopungua 19 wameuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, serikali ikisema wakenya 291 wamethibitishwa kuajiriwa kama wanajeshi wa Urusi. Akiwa mbele ya kamati ya uajiri na Leba katika bunge la seneti, Waziri wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi, amesema wakenya 42 hawajulikani waliko huku wengine 2 wakizuiliwa kama wafungwa wa […]

SHA YATIKISWA, TENA

Mamlaka ya afya ya jamii, SHA, kwa mara nyingine inakabiliwa na hatari ya kuvunjiliwa mbali kutokana na kesi iliyowasilishwa mahakamani ambapo mlalamishi anataka amri itolewe kuizuia mamlaka hiyo kukusanya fedha kutoka kwa wakenya. Kwenye kesi hiyo, mkenya kwa jina Francis Awino, anapinga uhalali wa SHA, akitaka izuiwe kuhudumu kama kampuni nyingine za bima kwa misingi […]

DUALE ATISHIA KUWASHTAKI WANAOSEMA KENYA INAUZA DAMU

Waziri wa afya Aden Duale sasa ametishia kuwachukulia hatua za kisheria watu walioibua madai kwamba Kenya inauza damu iliyochangwa na wakenya katika mataifa ya kigeni kinyume na sheria. Kulingana na Duale, ripoti za Kenya kuuza damu zilitokana na tafsiri potovu za takwimu za biashara, zilizochapishwa kwenye jukwaa la World Integrated Trade Solutions, akisema bidhaa nyingi […]

11 WAJERUHIWA RUMOS HILL WEST POKOT

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la Rumos Hills kaunti ya West Pokot kufuatia mkasa wa kuporomoka kwa mgodi na kuwajeruhi watu 11 huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama kwenye mgodi huo. Kulingana na shirika la Kenya Red Cross, mansura watatu wako katika hali mahututi, na wanatibiwa katika hgospitali ya rufaa ya Kapenguria walikopelekwa haraka. […]

GACHAGUA APIGA HATUA KUSHINIKIZA FIDIA

Kesi ya kushinikiza fidia kutokana na kutimuliwa kutoka afisini kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, itaendelea wiki ijayo baada ya kikao cha pili hapo jana ambapo Gachagua alifanikiwa kuishawishi mahakama kuidhinisha ushahidi kwamba aliugua ghafla hoja dhidi yake ilipokuwa ikijadiliwa katika bunge la seneti. Licha ya pingamizi za mawakili wa serikali kuhusiana na ushahidi huo, […]

JAJI WARSAME AAPISHWA RASMI

Jaji Mohamed Warsame ameapishwa rasmi hii leo kuwa jaji mkuu wa mahakama ya upeo nchini katika hafla iliyofanyika kwenye  ikulu ya Nairobi, Warsame anakua jaji wa kumi na nne wa mahakama ya juu zaidi nchini baada ya  kujaza nafasi ilyowachwa wazi na jaji Mohamed Ibrahim aliyeaga dunia Decemba mwaka jana. Rais William Ruto alimteua rasmi […]

KESI YA GACHAGUA KUNG’ATULIWA YAENDELEA

Mawakili wa kumuakilisha aliyekuwa Naib Rais Rigadhi Gachagua wamewasilisha maombi kadhaa katika vikao vya kusikiza kesi ya kumfurusha afisini vinavyoendelea katika mahaka ya milimani. Gachagua kupitia mawakili wake amewasilisha vipengee saba anavyotaka viangaliwe kwa ufasaha mahakamani na kusema kuwa kung’atuliwa kwake mamlakani hakukushirikisha umma ipasavyo. Imetayarishwa na Hilda Ajema

MUDAVADI AONGOZA KAMATI KUJADILI HALI YA WAKENYA WANAOISHI UGHAIBUNI

Mkuu  wa mawaziri nchini  Musalia Mudavadi pamoja na mawaziri Kipchumba Murkomen na Alfred Mutua wamekutana hii leo na kamati ya leba ya mawaziri  kujadili ustawi wa Wakenya wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi. Kikao hicho kimelenga kupokea maelezo kuhusu hali ya usalama, ulinzi wa haki za wafanyakazi na changamoto zinazowakumba raia wa Kenya ughaibuni. Miongoni mwa masuala yanayoangaziwa ni […]

WIZARA YA ELIMU YASISITIZA  MPITO WA JSS UPO SAWA

Waziri wa Elimu Julius Ogamba na RaiS William Ruto wamesisitiza kuwa mpito wa wanafunzi wa gredi ya kumi imefikia asilimia 99 kinyume na takwimu kubaini kua kiwango cha wanafunzi waliojiunga na gredi hiyo ni cha chini Akizungumza mjini Naivasha Ruto ametaja umuhimu wa wazazi kulipa karo kupitia mfumo wa E-Citizen ili kuzuia ufujaji wa pesa. […]