ULINZI STARS WAPANIA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA

Kocha wa Ulinzi Stars Mulinge Ndeto amesema timu hiyo itaendelea kupigania kusalia katika Ligi Kuu ya SportPesa hadi mwisho wa msimu. Kauli hiyo imejiri baada ya Ulinzi Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mathare United, ushindi uliowapa matumaini mapya ya kuepuka kushuka daraja. Timu hiyo sasa iko nafasi ya 15 ikiwa na […]

GOR MAHIA WATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA FKF

Gor Mahia wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF msimu wa 2025/26 baada ya AFC Leopards kufungwa mabao 2-1 na APS Bomet. K’Ogalo wameweka rekodi mpya kwa kutwaa taji lao la 22 licha ya kutocheza mechi yao dhidi ya Mara Sugar iliyositishwa kutokana na mzozo wa uwanja. Matokeo hayo yaliiacha AFC Leopards nyuma kwa alama […]

BUNGE LAPINGA TAARIFA ZA USHURU KWA ARDHI YA UMILIKI WA KUDUMU

Bunge la Kitaifa limekanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni kuwa Mswada wa Fedha 2026 unapendekeza Wakenya kulipa kodi ya kila mwaka kwa ardhi ya umiliki wa kudumu. Bunge hilo limesema madai hayo ni ya kupotosha na yanalenga kuwachanganya wananchi kuhusu yaliyomo kwenye mswada huo. Limefafanua kuwa Mswada wa Fedha 2026 hauna kipengele chochote kinachohusu ushuru wa ardhi, umiliki wa kudumu wala […]

BAADHI YA VIONGOZI WA ODM WAUNGA MKONO SERIKALI JUMUISHI

Baadhi ya viongozi wa Chama cha ODM wanaounga mkono serikali jumuishi wamesema wataendelea kushirikiana na serikali baada ya kuwa muda mrefu katika upinzani. Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama Gladys Wanga wamesema ushirikiano na serikali utasaidia maeneo yao kupata maendeleo na kunufaika zaidi. Wamewahimiza wafuasi wao kuunga mkono serikali huku baadhi wakipendekeza kuwepo kwa utaratibu wa […]

VIONGOZI WA KENYA KWANZA WAONYESHA IMANI KWA RUTO 2027

Baadhi ya viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza wameeleza imani kuwa Rais William Ruto atapata muhula wa pili kutokana na rekodi yake ya maendeleo na juhudi za kuunganisha taifa. Wakizungumza katika eneo bunge la Turbo, Viongozi hao Wamedai kuwa viongozi wa upinzani wanaendeleza siasa za mgawanyiko badala ya kuangazia maendeleo ya wananchi. Aidha wamemtetea Rais kuhusiana […]

MABADILIKO KATIKA ULINZI WA RAIS RUTO BAADA YA HITILAFU YA KIUSALAMA

Huduma ya Polisi imefanya mabadiliko katika kikosi cha usalama wa Rais William Ruto baada ya hitilafu ya kiusalama iliyotokea Kaunti ya Kilifi Katika tukio hilo, kijana mmoja alivunja ulinzi wa rais na kufika karibu na jukwaa wakati Rais alipokuwa akihutubia wananchi. Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais Noah Maiyo amehamishwa kwenda makao makuu ya […]

MWILI WA MWANAMKE WAPATIKANA KWENYE MFUKO WA PLASTIKI EMBAKASI

Maafisa wa upelelezi katika eneo la Embakasi wanafanya uchunguzi baada ya kiwiliwili cha mwanamke kupatikana ndani ya mfuko wa plastiki kando ya Barabara ya North Airport karibu na uzio wa uwanja wa ndege. Polisi walisema mwili huo uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana karibu na kituo cha mafuta katika eneo hilo, huku kichwa cha marehemu kikikosekana. Kamanda […]

KESI DHIDI YA  GACHAGUA INAENDELEA KUSIKIZWA MILIMANI

 Kesi ya kubanduliwa mamlakani kwa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigadhi Gachagua inaendelea kusikizwa  sasa hivi katika mahaka ya milimani jijini Nairobi. Upande wa mashtaka ukijibu maswali yaliyoibuliwa na mawakili wa Gachagua huku bunge la kitaifa, seneti na upande wa naibu rais profesa kithure kindiki ukiwasilisha ushaidi wao kuwa kubanduliwa kwa Gachagua  kulifuata haki. Imetayarishwa na […]

KINDIKI ATETEA SERIKALI YA RUTO KWA WAKENYA HUKO ELGEYO MARAKWET

Naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki anasema serikali imefanya kila juhudi za kushukisha bei za mafuta ila vita vya izraeli na marekani  dhidi ya Iran ndivo vimesababisha kupanda kwa bidhaa hizo. Akizungumza katika kaunti ya Elgeyo Marakwet,Kindiki anasema serikali inafanya kila iwezavyo kushukisha bei ya bidhaa hivyo na kuhakikisha inashukisha ushuru wake na kutenga fedha […]

SERIKALI YAJITETEA KUWAKINGA WAKENYA NA MAKALI YA BEI ZA MAFUTA

Ruto anasema kutokana na kuendelea  kuongeza kwa bei za mafuta duniani serikali yake imetumia takribani shilingi bilioni kumi na tatu za hazina ya maendeleo ya mafuta kuwakinga wakenya na gharama hizo huku akiongeza kwamba serikali yake imepunguza kodi ya thamani ya ziada kutoka asilimia kumi na sita hadi asilimia nane akisema katika mwezi wa Aprili […]