RUTO ATAKA MAGEUZI YA HARAKA KATIKA UMOJA WA AFRIKA

Rais William Ruto ametaka kuharakishwa kwa mageuzi ndani ya Umoja wa Afrika ili bara la Afrika liweze kujitegemea zaidi kupitia taasisi imara na ufadhili endelevu. Rais amesema Afrika lazima ipunguze utegemezi wa nje na kuimarisha uwezo wake wa kushughulikia changamoto zake kupitia utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika. Ruto amezungumza baada ya kuongoza […]

MAANDAMANO YASHUHUDIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI

Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini yamefanyka katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Roysambu, nyeri, Nyahururu miongoni mwa maeneo mengine. Waandamanaji hao wamefunga baadhi ya barabara na kuchoma magurudumu hali ilyolemaza shuguli za uchukuzi katika maeneo hayo huku polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwatanya waandamanaji hao waliokuwa wamefunga sehemu  ya barabra  kuu ya […]

MBADI  AWATAKA VIONGOZI WA UPINZANI KUSOMA NA KUUELEWA MSWADA WA FEDHA

Waziri wa fedha John Mbadi amewasuta vikali viongozi wa upinzani kwa madai ya kuwapotosha wakenya kuhusu mswada wa fedha wa 2026-2027. Akizungumza katika vikao na wanahabari jijini Nairobi, Waziri Mbadi amewataka viongozi haswa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka  kukoma kuupotosha umma kuhusu baadhi ya vipengee vilivyomo ndani ya mswada huo. Imetayarishwa na Hilda […]

KINDIKI ASUTA VIONGOZI  WA SIASA WENYE MATAMSHI MABAYA

Naibu wa Rais Kithure Kindiki amejitenga na baadhi ya matamshi ya viongozi wa chama cha UDA kuwa wanalenga kuhitilafiana na matokeo ya Urais mwaka wa 2027 ili kumpa ushindi Rais William Ruto iwapo atapata kura chache katika uchaguzi mkuu ujao. Akijibu kauli ya viongozi  hao akiwemo  naibu wa gavana wa kaunti ya kakamega Ayubu Savula, […]

RAIS MUSTAAFU UHURU AONGOZA HAFLA YA CHAMA CHA JUBILLEE

Rais mustaafu Uhuru Kenyatta anaongoza mkutano wa wajumbe wa chama cha Jubilee katika kaunti ya Kiambu. Akizungumza kwenye hafla hiyo Uhuru amewashtumu wandani wa Rais William Ruto wanaomtaka astaafu katika ulingo wa siasa. Kulingana na Uhuru  tangu alipostaafu uongozini  mwaka wa 2022 chama chake kimekua kikikabiliwa na misukosuko akiapa kukiimarisha chama hicho. Imetayarishwa na Hilda […]

EPRA YAAHIRISHA MIKUTANO YA HADHARA KUHUSU MAPENDEKEZO MAPYA YA USHURU WA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imeahirisha vikao vya mashauriano vya umma nchini kote kuhusu mapendekezo ya ombi la bei ya reja reja ya umeme kwa mara ya tano kwa Udhibiti wa Ushuru wa mwaka wa kifedha 2026/27 hadi 2028/29. Katika notisi ya umma ambayo imetolewa, EPRA imetangaza kwamba mabaraza hayo, ambayo yalipangwa […]

CARRICK AONA NAFASI YA TATU KAMA MWANZO MPYA UNITED

Kocha wa Manchester United Michael Carrick amesema kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya uingereeza ni msingi mzuri wa kujenga mafanikio ya baadaye. Carrick alitoa kauli hiyo baada ya United kuhitimisha msimu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion. Kocha huyo alithibitishwa rasmi kupewa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuboresha […]

ARTETA SASA ALENGA UBINGWA WA ULAYA

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema sasa analenga kutwaa ubingwa wa UEFA Champions League baada ya kushinda Ligi Kuu ya uiingereza. Arteta alisema hayo baada ya Arsenal kusherehekea ubingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya mwisho ya msimu. Mabao ya Gabriel Jesus na Noni Madueke yaliihakikishia Arsenal kumaliza msimu ikiwa […]

KENYA YASHINDWA KUTAMBA CAPE TOWN MARATHON

Mashindano ya Sanlam Cape Town Marathon yalikuwa magumu kwa wanariadha wa Kenya huku nchi ikipata nafasi moja pekee ya jukwaani katika mbio za wanaume na wanawake. Kalipus Lomwai ndiye aliyekuwa Mkenya pekee kumaliza katika tatu bora baada ya kushika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:05:06 katika mbio za wanaume. Mbio hizo zilitawaliwa na […]

OMANYALA BADO ANA NJAA YA MAFANIKIO ZAIDI

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala amesema bado hajaridhishwa na mwanzo wake mzuri wa msimu wa mwaka 2026 huku akilenga mafanikio makubwa zaidi. Omanyala ameonyesha kiwango bora katika mashindano ya Diamond League nchini China ambapo aliibuka mshindi katika mbio za mita 100 kwa muda wa sekunde 9.94 mjini Xiamen. Mkenya huyo mwenye umri […]