MVURYA AWARAI WAKENYA KUUNGA MKONO HARAMBE STARS

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amewataka Wakenya kuunga mkono Harambee Stars kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika ya 2024-CHAN- itakayoanza Agosti 2 hadi Agosti 30, 2025. Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya Uwanja wa Nyayo na viwanja viwili vya mazoezi, Police Sacco na Ulinzi Complex kwa Kamati ya andalizi, Mvurya alisema Kenya iko katika […]

YAMAL KURITHI JEZI LA MESSI

Nyota chipukizi wa Barcelona Lamine Yamal alirithi jezi nambari 10 ya klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na nguli wa muda wote Lionel Messi, Jumatano. Winga huyo mwenye umri wa miaka 18, mara nyingi akilinganishwa na supastaa huyo wa Argentina ambaye pia alipitia akademi ya vijana ya klabu hiyo ya La Masia, aliwasaidia wababe hao […]

MACARTHY AWATEMA WACHEZAJI WATANO

Kocha wa Harambee Stars Benni MCarthy amewatema wachezaji watano kwenye kikosi chake kuelekea michuano ya CHAN. Wachezaji waliotemwa ni; Yakeen Muteheli na Staphod Odhiambo wa Ulinzi Stars, Keith Imbali wa Shabana, Kelly Madada wa AFC Leopards na kipa wa Tusker FC Brian Opondo. Kocha huyo alieleza ugumu wa uamuzi wake kuzima ndoto za wachezaji hao […]

CELTIC WADHIBITISHA UHAMISHO WA KIBET

Hali tata kuhusu mustakabali wa nyota wa Kenya wa U-20, Aldrine Kibet hatimaye zimepata jibu baada ya klabu ya ligi kuu ya Uhispania RC Celta Vigo kuthibitisha rasmi uhamisho wake kwa kandarasi ya miaka minne itakayotumika hadi 2029. Tangazo hilo lilitolewa kwenye kurasa rasmi za kilabu, na kueleza kwamba Kibet anajiunga na Celta Fortuna, timu […]

ONDOA NYASI YAZINDULIWA WEST POKOT

Hali ya kimaisha ya wakazi wa kaunti ya West Pokot inatarajiwa kuimarika chini ya mpango wa Ondoa Nyasi Initiative wa serikali ya kaunti hiyo unaolenga kuwajengea nyumba za mabati na kuwahamisha kutoka nyumba za nyasi. Mpango huo unaogharimu shilingi milioni 50, unalenga kuwafaidi wakazi 2,500 ambao watapokea mabati 10 kila mmoja. Simon Kachapin ni gavana […]

WIZARA YAWATAKA WAZAZI KUKUMBATIA CHANJO

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dakta Ouma Oluga, amewataka wakenya kuhakikisha wanapokea chanjo inayoendelea kutolewa dhidi ya homa ya tumbo na ukambi kwenye zoezi ambalo limeratibiwa kukamilika hapo kesho. Oluga amekuwa akizungumza Kisumu ambako amewataka wazazi kupuuza alichokitaja kuwa propaganda inayotolewa kuhusiana na chanjo hiyo. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KANJA KUFIKA BUNGENI KUHUSU MGOGORO WA NPS-NPSC

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja anatarajiwa kufika mbele ya bunge la kitaifa kutoa mwanga kuhusu mgogoro uliopo kati ya idara ya polisi NPS na tume inayosimamia raslimali ya polisi nchini c Hii ni baada ya mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, Peter Lelei kuwasilisha lalama akidai kwamba Kanja ameweka kimaksudi mikakati inayozuia tume hiyo kutekeleza […]

RAIS BIYA AFANYIA MAGEUZI UONGOZI WA JESHI

Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye ni kiongozi wa taifa mkongwe zaidi ulimwenguni kwa sasa amefanya mageuzi katika safu za juu za jeshi lake, wachanganuzi wakisema hatua hiyo inalenga kumhakikishia ushindi kwenye uchaguzi wa urais mwezi Oktoba mwaka huu. Mageuzi hayo yamefanywa katika vitengo vyote vya jeshi, ikiwemo uteuzi wa […]

SIKUMWUUA REX, AFISA WA POLISI AKANA MAHAKAMANI

Afisa wa polisi kwa jina Isaiah Murangiri, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kumwua Rex Maasai amekana kuhusika na mauaji hayo, akikana Ushahidi wa picha video na deta za simu uliowasilishwa mahakamani. Wakati wa kikao cha hapo jana, afisa huyo alikana ushahidi unaoonekana kuwa wazi, ikiwemo deta za mawasiliano ya sim una picha inayomwonyesha akiwa karibu […]

UGONJWA USIOJULIKANA MOMBASA WACHUNGUZWA

Wakenya na hasa wakaazi wa Mombasa wametakiwa kutokuwa na hofu serikali ikiendesha uchunguzi katika ugonjwa usiojulikana unaodaiwa kusababisha vifo vya watu 4 huko Migadini Mombasa. Akiongea huko Kisumu mkurugenzi wa afya Dkt Patrick Amoth anasema uchunguzi wa awali umebaini kuwa waliofariki walikuwa pia wanaugua magonjwa mengine. Naye waziri wa afya Aden Duale anasema chembe chembe […]