IDADI YA WALIOFARIKI TODONYANG HAIJABAINIKA

Serikali itabuni kundi maalum litakaloendeshwa uchunguzi kubaini idadi kamili ya watu waliofariki wakati wa uvamizi ulitokea katika eneo la Todonyang huko Turkana. Akiongea baada ya mkao wa usalama huko Lodwar waziri wa usalama Kipchumba Murkomen anasema imekuwa vigumu kubaini idadi ya waliofariki katika tukio hilo la mwezi februari. Anasema huenda kuna watu waliozama katika ziwa […]

OCHOLLA AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

Kocha Msaidizi wa KPA Samuel Ocholla amefurahishwa na juhudi na dhamira ya timu yake baada ya kupata ushindi wa mechi zote mbili wikendi katika Ligi Kuu ya Kikapu ya Wanawake nchini.Siku ya Jumamosi, KPA iliishinda Strathmore Swords 73-51 na Jumapili wakaichapa ANU Panthers 83-39.Ocholla alisisitiza kuwa timu hiyo itasalia na umakini kwani sasa ipo kileleni […]

VILABU VIAJIZOLEA MINOFU KATIKA KOMBE LA VILABU LA FIFA

Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA lililomalizika hivi punde lilikuja na zawadi nzuri za kifedha kwa timu zilizoshiriki, pamoja na vilabu vinne vya Kiafrika vilivyowakilisha bara la Afrika.Vigogo wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ndio waliopata pesa nyingi zaidi kama klabu iliyoorodheshwa zaidi barani Afrika, na kuchukua dola milioni 13.6 (takriban Ksh1.625 bilioni).Al Ahly na […]

TRAVERS AONDOKA BOURNEMOUTH

Everton ilimsajili kipa wa Ireland Mark Travers kutoka Bournemouth kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 4.Travers alikubali kandarasi ya miaka minne na klabu hiyo ya Ligi Kuu, ambayo itafungua uwanja wao mpya mwanzoni mwa msimu ujao.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema anajivunia sana na anafurahi kuwa mchezaji wa Everton.Travers, ambaye aliichezea Bournemouth […]

HENDERSON AJIUNGA NA BRENTFORD

Kiungo wa kati wa England Jordan Henderson anasisitiza kuwa bado anaweza kuimarika katika Ligi ya Premia baada ya kujiunga na Brentford kwa uhamisho wa bila malipo kufuatia kuondoka kwake Ajax ya Uholanzi.Henderson alikubali kandarasi ya miaka miwili na Brentford aliporejea Ligi Kuu baada ya kuondoka Liverpool mwaka 2023.Atamenyana na klabu yake ya utotoni ya Sunderland […]

FKF YAOMBWA KUONGEZA MGAO WA PESA KWA LIGI KUU

shirikisho la Soka la Kenya (FKF) linafaa kuongeza zawadi ya pesa taslimu kwa mabingwa wa ligi ya nyumbani ili kuongeza ushindani wa vilabu vya Kenya katika ngazi ya bara.Alisema kuwa Kushiriki katika mashindano ya CAF kunagharimu kati ya Ksh15 na Ksh20 milioni kwa mechi za nyumbani na ugenini na bila ya tuzo nzuri ya ya […]

UGANDA YATANGAZA BEI NAFUU YA TIKETI YA CHAN

Huku zikiwa zimesalia siku 17 tu kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), Uganda imetangaza bei nafuu za tiketi ikilinganishwa na waandaji wenza Kenya.Uganda imeweka tiketi za kawaida USD1 (takriban Ksh129 na UGX3,586) huku tikiti za VIP zikiuzwa kwa USD2 (takriban Ksh258 na UGX7,052).Itagharimu mashabiki USD3 pekee (takriban Ksh387 na UGX10,578) kupata tiketi ya […]

SHIKANGWA AONDOKA SIMA QUEENS 

MSHAMBULIAJI wa Harambee Starlets, Jentrix Shikangwa ameondoka rasmi Simba Queens, na hivyo kuashiria mwisho ukurasa mzuri katika soka la wanawake Tanzania. Tangazo hilo limekuja ikiwa ni sehemu ya kile kinachoonekana kuwa ni mabadiliko makubwa ya kikosi kilichofanywa na wababe hao wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.Shikangwa alijiunga na Simba Queens Januari 2024 baada ya kusaini […]

STARS WACHEZA NA SHARKS KAMA MAANDALIZI YA CHAN

Harambee Stars ilianza maandalizi yake ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 kwa taabu kufuatia kufungwa 2-1 na Timu ya Sharks Family katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Kasarani Annex Grounds.Timu ya Sharks Family, inayojumuisha wachezaji wa zamani wa Kariobangi Sharks, ilipata mabao yake kupitia kwa Eli Asieche na Shaphan Oyugi huku Bao pekee la […]

MIHEMKO YA UHAMISHO

Liverpool wanatarajiwa kushindana na Newcastle kwa ajili ya Hugo Ekitike, Reds pia wanawania Ollie Watkins na Victor Osimhen, na Eintracht Frankfurt kukataa ofa ya Magpies kwa Ekitike. Liverpool wanatarajiwa kushindana na Newcastle United kumnunua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike, 23, baada ya kuambiwa kuwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, hauzwi katika dirisha […]