KOCHA WA FORTUNE SACCO AAGA DUNIA

Jumuiya ya kandanda inaomboleza kifo cha kusikitisha na kisichotarajiwa cha kocha mkuu wa Fortune Sacco FC Sylvester Odero, aliyeaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani.Kisa hicho kilichothibitishwa na wasimamizi wa klabu hiyo kilizua mshtuko katika Ligi Kuu ya Taifa (NSL), ambapo Odero alikuwa amejidhihirisha kwa haraka kama mmoja wa wataalamu wa kutumainiwa na kuheshimiwa katika […]

COMPEL FC WAPANDISHWA DARAJA

Ndoto ya Compel FC ya kupandishwa daraja kutoka Ligi ya Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu ya Soka ya Kenya (NSL) hatimaye imetimia, baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bumbani katika mechi ya mchujo iliyochezwa wikendi katika uwanja wa Thika. Akizungumzia mafanikio yao ya ajabu, kocha mkuu wa Compel, George Mutimba alisema […]

MAKOCHA 148 WATUMA OMBI KUJIUNGA NA GOR MAHIA

Baadhi ya makocha 148 wametuma maombi ya nafasi ya kocha mkuu iliyo wazi katika klabu ya Gor Mahia FC ya Kenya. Makocha kadhaa wa kigeni – wenye makao ya Uropa – wamewasilisha hati zao ili kuzingatiwa, baadhi yao wakiwa wamewahi kuitumikia klabu hapo awali. Kwa jumla, kufikia tarehe ya mwisho ya kutuma maombi wiki iliyopita […]

MUHIDDIN ASIFIA ADRIAN KUJIUNGA NA CELTA

Aliyekuwa kocha mkuu wa Harambee Stars Twahir Muhiddin anasema kuhamia kwa Adrian Kibet kwenda Celta Vigo ya La Liga kutafungua milango zaidi kwa wachezaji wengi wa Kenya kuhamia nje ya nchi. Kulingana na Twahir, maskauti zaidi watakuwa wakiwafuatilia wachezaji wa Kenya, kwa nia ya kuibua vipaji vyao kulingana na mafanikio ya Kibet, ambayo yatakuwa na […]

CHELSEA BINGWA WA ULIMWENGU

Klabu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo klabu bingwa ulimwenguni baada ya kutawazwa mabingwa hapo jana katika fainali ya kipute cha klabu bingwa ulimwengu yaani FIFA Club World Cup iliyoshirikisha klabu 32 kutoka mashirikisho ya mabara yote. Hii ni baada ya Chelsea kuwacharaza mabingwa wa bara Ulaya Paris St Germain kwa mabao 3-0 katika uwanja wa […]

SHULE ZA KAKAMEGA ZATAMBA MAGHARIBI

Shule za upili katika kaunti ya Kakamega zilitamaliki mashindano ya michezo kwa shule za upili katika ukanda wa Magharibi, zikijinyakulia mataji mbali mbali na kujikatia tiketi za kushiriki mashindano ya kitaifa yatakayoandaliwa baadaye mwezi huu kwenye kaunti hiyo. Baadhi ya shule hizo ni Musingu Boys ambao walitawazwa mabingwa wa kandanda kwa wavulana, baada ya kuwafunga […]

UJUMBE WA KINDIKI KWA WAFANYABIASHARA

Naibu Rais Kithure Kindiki amepongeza juhudi za wafanyabiashara katika sekta ya kibinafsi kwa kuoanisha juhudi zao na vipaumbele vya kitaifa, hususan uwezeshaji wa vijana na Agenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi almaarufu bottom-up economy. Akizungumza wakati wa Maonyesho ya Kazi yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kindiki amesisitiza dhamira ya serikali ya kuweka mazingira wezeshi kwa […]

MIGUNA” MATIANG’I HAFAI KUWA RAIS”

Azma ya aliyekuwa waziri wa usalama Fred Matiang’i kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao imeendelea kuibua hisia mseto, wakili mwenye utata Dakta Miguna Miguna akishikilia kuwa Matiang’i hafai kuliongoza taifa hili kutokana na ukiukaji wa amri za mahakama alipokuwa waziri. Kwenye mahojiano na runinga moja nchini, Miguna ametaja kufurushwa kwake nchini kwa lazima na uharibifu […]

WANAFUNZI MARSABIT WAENDELEA KUTIBIWA KUFUATIA ‘KICHAPO’

Wizara ya elimu imeanzisha uchunguzi katika kisa cha kusikitisha ambapo wanafunzi 36 wa shule ya upili ya wasichana ya Maikoma kaunti ya Marsabit wanadaiwa kupewa adhabu kali na walimu baada ya wanafunzi hao kulalamika kwamba walishinda na njaa wakati wa tamasha za muziki. Kulingana na picha ambazo zimeibua shutuma, wanafunzi hao wanaonekana wakiwa na alama […]

MAZUNGUMZO YA WANARIKA YAKARIRIWA

Pendekezo la kinara wa ODM Raila Odinga kuhusu kuwepo kwa mazungumzo ya wanarika tofauti tofauti ili kuimarisha mshikamano wa nchi limeungwa mkono na viongozi wanaoegemea mrengo wa Kenya Kwanza, wakisema ndiyo njia pekee ya kuhakikisha maendeleo ya taifa. Wakizungumza katika maeneo mbali mbali ya nchi, viongozi hao aidha wamekariri agizo la Rais William Ruto kwa […]