DIG LAGAT KUREJEA KAZINI LEO

Naibu inspekta mkuu wa polisi aliyejiondoa kwa muda Eliud Lagat ameratibiwa kurejea kazini hii leo baada ya ripoti ya uchunguzi kukosa kumpata na ushahidi unaomhusisha moja kwa moja na mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang. Walio karibu na Lagat waliwadokezea wanahabari kwamba Lagat amechukua uamuzi wa kurejea kazini baada ya vitengo vyote vya uchunguzi […]

WANNE WANASWA KWENYE MSAKO WA POMBE HARAMU THARAKA NITHI

Polisi huko Tharaka Nithi wanazuilia washukiwa 4 walionaswa wakati wa msako dhidi ya pombe haramu na dawa nyingine za kulevywa katika soko la Kibunga. Wanne hao walipatikana na lita 200 za pombe na misokoto 31 ya dawa za kulevywa aina ya bangi na sasa wanasubiri kufikishwa kotini siku ya jumatatu. Idara ya usalama sehemu hiyo […]

MGOMO WAFUTILIWA MBALI MACHAKOS

Ni afueni kwa wakaazi wa Machakos baada ya maafisa wa kliniki kufutilia mbali mgomo wao uliopangwa kuanza usiku wa leo. Hii ni baada ya maafisa wa muungano wa wahudumu hao kutia Saini mkataba wa maelewano na serikali ya kaunti ya Mchakos ukilenga kuangazia lalama walizoibua. Kupitia mwenyekiti wao wa kitaifa Peterson Wachira wanasema miongoni mwa […]

TAHADHARI YATOLEWA KUHUSU MPOX

Unashauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Mpox ambao unazidi kuenea nchini Kenya ikiwa na zaidi ya visa 200 vya maambukizi. Kaunti ya Mombasa imeripotiwa visa 98 hasa katika maeneo ya Nyali na Changamwe watu 2 wakiripotiwa kufariki kutokana na Mpox. Maafisa wa afya huko Mombasa wanasema ugonjwa huo unazidi kuenea katika jamii […]

IDADI YA WALIOFARIKI SABA SABA YAFIKIA 38

Idadi ya watu waliofariki kutokana na vurugu za maandamano ya siku ya saba saba imefikia 38 na wengine 130 wakisalia na majeraha. Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za kibnadamu linalosema waathiriwa walishambuliwa na wahuni na wengine kupigwa na maafisa wa polisi waliokuwa wametumwa kushika doria. Watu 8 walifariki […]

NAIBU GAVANA KERICHO AIBUA MADAI YA UFUJAJI

Naibu Gavana wa Kaunti ya Kericho, Fred Kirui ameibua madai ya kufujwa kwa zaidi ya shilingi milioni 80 katika serikali ya kaunti hiyo, akitaka uchunguzi kufanywa na kuwawajibisha wahusika. Kirui ambaye amekuwa na utofauti na Gavana Eric Mutai, amesema pesa hizo zililipwa kwa zaidi ya kampuni 33 za kandarasi na usambazaji bidhaa. Anadai kuwa malipo […]

BARAZA LA MAGAVANA LALAMIKIA MADENI

Huenda wakazi katika maeneo ya mashinani wakakosa huduma muhimu zinazotolewa na serikali za kaunti kutokana na kucheleweshwa kwa mgao wa serikali hizo ambao umesababisha kuongezeka kwa madeni. Kulingana na baraza la magavana likiongozwa na mwenyekiti wake Ahmed Abdullahi, serikali hizo zimepokea shilingi bilioni 400.26 pekee, kati ya shilingi bilioni 600.69 zilizotengwa kwa mwaka wa kifedha […]

MWENYEKITI WA IEBC, MAKAMISHNA KUAPISHWA LEO

Jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa kuongoza hafla ya kumwapisha mwenyekiti mpya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon na makamishna 6 hii leo, ili kuanza majukumu yao rasmi. Hafla hiyo itafanyika chini ya siku moja baada ya Rais William Ruto kuwateua 7 hao rasmi na kuchapisha majina yao kwenye gazeti rasmi la […]

OBILO KUTUMIA MECHO ZILIZOSALIA KUJIANDAA KWA MSIMU UJAO

Kocha Mkuu wa Zetech Sparks Maurice Obilo atatumia mechi zilizosalia za msimu wa kawaida kama maandalizi ya mchujo ujao, katika Ligi Kuu ya kitaifa ya Kikapu ya Wanawake nchini. Wanafunzi hao walilaza Stanbic Aces 53-37 kabla ya kupata ushindi mwingine wa 63-56 kwa wenzao wa vyuo vikuu Strathmore Swords wikendi katika uwanja wa Nyayo na […]

ARTETA AFURAHISHWA KUIJIUNGA KWA NORGAARD KATIAKA KIKOSI CHAKE

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amefurahishwa na ujio wa Christian Norgaard, akisema kwamba analeta tajiriba ya uzoefu baada ya kusajiliwa na The Gunners kutoka Brentford leo. Kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 31 amejiunga kwa ada ya awali ya Shilingi bilioni 1.9, kwa mujibu wa The Athletic. Norgaard alifunga mara 13 […]