MICHEZO KAKAMEGA ZAENDELEA BAADA YA KUSITISHWA

Mashindano ya kandanda ya wavulana ya kanda ya Magharibi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa muda kufuatia rufaa ya Musingu High, kupinga uamuzi uliowaondoa kwenye kinyang’anyiro hicho sasa yataendelea kufuatia kukamilika kwa suala hilo leo jioni. Ilibainika kwamba Musingu ilichezesha wachezaji wawili wasiostahiki – Boaz Muchiri na Harrison Amalemba dhidi ya mabingwa wapya wa Kaunti ya Kakamega […]

DILI YA MBEUMO YAACHELEWA KUIVA

Vijana wa Ruben Amorim wamerejea katika mazoezi ya kabla ya msimu mpya huko Carrington huku matayarisho ya 2025/26 yakianza. Hata hivyo, bado kuna mkazo mkubwa kwenye biashara ya United ya uhamisho. Matheus Cunha tayari amewasili kutoka Wolves kwa pauni milioni 62.5 lakini Reds wametatizika kupata dili la kumnunua Bryan Mbeumo. Zabuni mbili zimekataliwa na Brentford […]

MADUEKE NDANI YA ASENALI

Arsenal wamefikia makubaliano ya kumsajili Noni Madueke kutoka Chelsea kwa £52m. Winga huyo wa Uingereza tayari amekubali masharti ya mkataba wa miaka mitano na huenda akakamilisha uhamisho wa kwenda Emirates Stadium. Arsenal, ambao pia wanatarajiwa kuongeza kasi ya kumsaka Eberechi Eze wa Crystal Palace, wamekuwa wakitafuta kuongeza kina zaidi kwenye safu ya ulinzi na wamechukua […]

ETIENNE ATUZWA KUA KOCHA BORA WA MWEZI

Kocha mkuu wa Kenya Police FC Etienne Ndayiragije amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi wa Chama cha Wanahabari wa Michezo nchini (SJAK) kufuatia mafanikio yake ya kuwaongoza wasimamizi wa sheria kutwaa taji lao la kwanza kabisa la Ligi Kuu ya FKF. Ndayiragije, ambaye alijiunga na Kenya Police mnamo Novemba 2024, amesimamia mabadiliko ya ajabu, na […]

MACARTHY ATETEA UTEUZI WAKE WA KIKOSI CHA STARS

Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy ametetea uteuzi wake wa kikosi cha CHAN, mashindano yatakayoanza mwezi ujao. Raia huyo wa Afrika Kusini anasema alichagua wachezaji bora zaidi wa ndani waliopo, huku kukiwa na mijadala tofauti baada ya kutaja kikosi chake cha kwanza ambacho kiko kambini kwa ajili ya mashindano ya bara. Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka […]

USALAMA WA WAMAFUNZI KUIMARISHWA, SERIKALI

Wizara ya elimu imetangaza kuwa itaendesha ukaguzi wa mara kwa mara shuleni kwa lengo la kutathmini hali ya miundomsingi ili kuwahakikishia wanafunzi usalama wao, hasa baada ya wanafunzi 3 katika wa chekechea katika shule ya Queen of Angels kaunti ya Uasin Gishu kuzama kwenye choo walimokuwa. Katibu katika idara ya elimu ya msingi Julius Bitok […]

POLISI BARASA ‘AJIPATA PEKEE YAKE’

Huenda familia ya mchuuzi Boniface Mwangi aliyefariki kutokana na majeraha ya risasi ikapata haki baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga kuidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya afisa wa polisi Klinzy Masinde anayedaiwa kumpiga risasi mchuuzi huyo. Mahakama imefahamishwa kuwa afisa huyo atashtakiwa hii leo mbele ya jaji wa mahakama kuu Kanyi Kimondo. […]

KAULI YA MBUNGE YASHTUA NCHI

Mbunge wa Belgut Nelson Koech ambaye ni pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi bungeni amelishangaza taifa kutokana na kauli yake kwamba polisi wanafaa kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji wanaovamia mali wakati wa maandamano. Koech amesisitiza kuwa sheria inawaruhusu polisi kutumia nguvu kama hizo ili kulinda mali na maisha. Kauli yake imekinzana na amri ya […]

MAHAKAMA YAIDHINISHA KUAPISHWA KWA USIMAMIZI WA IEBC

Mwenyekiti mpya wa IEBC Erastus Ethekon na makamishna 6 wanatarajiwa kuapishwa muda wowote baada ya mahakama kuu kutupilia kesi iliyokuwa ikipinga mchakato uliotumika kuwapiga msasa na kuwateua. Kwenye uamuzi wake, jopo la majaji 3 Roselyn Aburili, John Chigiti na Bahati Mwamuye wamesema kesi hiyo iliyowasilishwa na Kelvin Omondi na Boniface Mwangi haikuzingatia vigezo hitajika chini […]

TUKO TAYARI KWA CHAN

Kenya iko tayari kwa 98% kuandaa Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, kulingana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Ndani (LOC) Nicholas Musonye. Akizungumza chini ya mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, Musonye alithibitisha kwamba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefurahishwa na maendeleo ya Kenya, na kusifu uboreshaji wa miundombinu ya […]