SIMBAS WAVUNA USHINDI MNONO KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA

Kenya Simbas walianza safari yao ya Kombe la Afrika la Raga mwaka huu kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2027 kwa ushindi mnono wa 32-24 dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Kampala. Griffin Chao alianza kufunga dakika ya 20 kabla ya Barry Young kuongeza ‘tri’ ya pili, na kuifanya Kenya kuongoza […]

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA NYAMIRA

Taharuki imetanda katika eneo la Bonyunyu kaunti ya Nyamira, baada ya wakazi wenye hasira kukiteketeza kituo cha polisi cha Itibo wakilalamikia kufyetuliwa risasi kwa mwanamme mwenye umri wa miaka 19 wakati wa makabiliano kati ya kundi la wanafunzi na polisi. Polisi wamesema kituo hicho mwanzo kiliporwa kabla ya kuchomwa, ila wakathibitisha kuwa hakuna bunduki zilizopotea. […]

KARUA AMTAKA RUTO NJE

Shinikizo zinaendelea kutolewa zikitaka serikali ya Kenya Kwanza ikiongozwa na Rais William Ruto ijiondoe mamlakani kutokana na mabacho kimetajwa kuwa ukiukaji wa wazi wa kanuni za kidemokrasia kufuatia wimbi la maandamano ya kuipinga serikali hiyo. Wa hivi punde kutoa shinikizo hizo ni kinara wa chama cha PLP Martha Karua, akisema serikali ya kidemokrasia inafaa kuwasikiliza […]

MUKUNJI AKABILIWA NA KESI YA UGAIDI

Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji atasalia katika kituo cha polisi cha Muthaiga hadi Jumanne wiki ijayo wakati ambapo mahakama ya Kahawa itatoa uamuzi kuhusu ombi lake la kupewa dhamana. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama imzuilie kwa muda wa wiki 2 kutokana na uchunguzi unaoendelezwa katika madai ya mbunge huyo kufadhili na […]

GAVANA GUYO APUMUA

Gavana wa Isiolo Abdi Guyo ameponea shoka la kubanduliwa kutoka afisini baada ya seneti kutupilia mbali hoja ya kumbandua kwa misingi kwamba bunge la kaunti hiyo halikufuata mwongozo hitajika wa kujadili na kupigia kura hoja hiyo lililipombandua. Kulingana na taarifa ya seneti, maseneta 31 walipinga uamuzi wa wawakiklishi wadi wa Isiolo kumbandua huku 18 pekee […]

PINDA PINDUA ZA MAANDAMANO

Maandamano yanayoendelezwa nchini yamechukua mkondo tofauti, baada ya wahudumu wa afya kutishia kusitisha utoaji huduma iwapo usalama wao utaendelea kuwekwa hatarini jinsi ilivyoshuhudiwa Jumatatu ambapo wahuni walivamia hospitali ya Kitengela Subcounty. Wakiwahutubia wanahabari katika hospitali hiyo, maafisa wa miungano ya afya wakiongozwa na katibu mkuu wa KUCO George Gibore, wametishia kutoingia kazini siku ya maandamano. […]

LUSAKA ATIA SAINI BAGETI

Makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025-26 ya shilingi bilioni 15.9 katika kaunti ya Bungoma yameanza kutekelezwa, baada ya gavana Ken Lusaka kutia Saini rasmi kuwa sheria mswada wa makadirio hayo. Akizungumza baada ya hafla hiyo, Lusaka ameweka wazi mpango anaosema utahakikisha usawa wa maendeleo katika maeneo yote ya kaunti hiyo, shilingi bilioni […]

SIKU 2 KUU ZA GAVANA GUYO ZAANZA

Siku 2 za kuamua hatma ya gavana wa Isiolo Abdi Guyo zinaanza hii leo wakati gavana huyo atawasili katika bunge la seneti kujitetea dhidi ya madai ya ufisadi na utumiaji mbaya wa afisi yaliyosababisha wawakilishi wadi katika bunge la kaunti hiyo kumbandua. Bunge la seneti wiki jana liliafikia kuandaa kikao cha maseneta wote badala ya […]

FLUMINENSE WAKABILIANA NA CHELSEA

C wanafurahia kuitwa kinyong’onyea, kama timu ya chini ya Kombe la Dunia la Vilabu wanapoelekea kwa mechi ya Leo ya nusu fainali dhidi ya Chelsea, huku meneja Renato Gaucho akikumbatia mawazo ya “sisi dhidi ya ulimwengu” ambayo yameifanya timu hiyo ya Brazil kufikia hatua isiyowezekana. Klabu hiyo ya Rio de Janeiro iliwasili Marekani ikipewa nafasi […]

MAREKANI WALEMEWA KWA ROBO FAINALI

Timu ya taifa ya Marekani ilishindwa katika fainali ya Kombe la Dhahabu la CONCACAF kwa kuchapwa 2-1 na Mexico lakini itachukua mafunzo muhimu kutokana na michuano hiyo inapojizatiti kuelekea Kombe la Dunia mwaka ujao, kulingana na kocha Mauricio Pochettino. Marekani walifungiwa na Chris Richards katika mchezo huo wa Houston, Texas lakini Mexico wakashinda kupitia Raul […]