JSC YAZUIWA KUSIKILIZA KESI YA KUMWONDOA JAJI SANKALE

Ni afueni kwa jaji wa mahakama ya rufaa Sankale Ole Kantai baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuizuia tume ya huduma za mahakama JSC kuendelea kusikiliza kesi inayotoka kuondolewa afisini kwa jaji huyo. Kwenye uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amesema vikao hivyo kuruhusiwa kuendelea ilhali kuna kesi mahakamani kuhusiana na malalamishi dhidi ya jaji […]

WAKENYA MILIONI 2.2 KUTIBIWA BURE, RAIS

Wakenya milioni 2.2 walio na mapato ya chini wamepata afueni ya matibabu baada ya serikali kutangaza kuwa itakuwa ikiwalipia ada za SHA ili kugharamia matibabu yao. Tangazo hilo limetolewa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi, akisema mpango huo utawawezesha walengwa kupokea huduma za matibabu bila malipo katika hospitali za humu nchini. Kulingana na […]

NAIROBI MIONGONI MWA KAUNTI ZILIZOORODHESHWA KWA MATUMIZI KUPITA KIASI YA USAFIRI

Serikali za kaunti zinakabiliwa na kuchunguzwa kwa matumizi ya kupita kiasi katika safari zisizo muhimu. Ripoti ya Mdhibiti wa Bajeti, Margaret Nyakang’o, ilifichua kuwa kaunti 23 kati ya 47 zilishindwa kufikia kiwango cha asilimia 30 ya matumizi ya maendeleo na kutumia mabilioni ya pesa kwa safari za kifahari. Kama ilivyoripotiwa na afisi ya mdhibiti wa bajeti, […]

BARCELONA YAKABA KOO NEWCASTLE

Marcus Rashford alifunga mara mbili wakati Barcelona ikianza kampeni ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Newcastle United siku ya Alhamisi, huku Erling Haaland akifunga bao lake la 50 katika shindano hilo katika ushindi wa Manchester City dhidi ya Napoli. Jioni ya tatu mfululizo ya mechi katika raundi ya kwanza ya […]

BADARI FC TAYARI KUNGURUMA

Huku msimu wa Ligi Kuu ya Kenya wa 2025-26 ukianza wikendi hii, macho yote yanaelekezwa kwa Bandari FC, ambayo kocha wake mkuu Ken Odhiambo ametangaza kwa ujasiri timu yake kuwa “tayari kunguruma.” Dockers wanaanza safari wakiwa na matamanio makubwa. Baada ya dirisha dogo la usajili ambalo lilishuhudia wimbi la usajili wa wachezaji wenye uzoefu wakijiunga […]

KCB WAANZA KAMPEINI DHIDI YA TUSKER FC

KLABU ya Soka ya KCB inakodolea macho sura mpya wanapoanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) Ijumaa dhidi ya Tusker FC, chini ya kocha mkuu mteule Robert Matano. The Bankers, ambao walimaliza katika nafasi ya tisa msimu uliopita wakiwa na pointi 42, wamepania kutwaa taji la ligi kuu ya kwanza huku Matano akiwa […]

MWAKILISHI WADI NAIROBI AJIUZULU

Wakazi wa wadi ya Githurai 44 jijini Nairobi wamejipata bila mwakilishi katika bunge la kaunti ya Nairobi baada ya mwakilishi wao Mwangi Waithera kujiuzulu kwa misingi kwamba serikali ya kaunti hiyo imekosa kutekeleza miradi yake mikuu katika wadi hiyo. Miongoni mwa miradi hiyo kulingana na Waithera ni ahadi ya kujengwa kwa uwanja wa michezo mbali […]

MVUTANO WA MFUMO WATISHIA HUDUMA

Mfumo mpya wa ununuzi wa e-Procurement umeendelea kutishia kusambaratika kwa huduma katika taasisi za umma kutokana na mvutano kati ya wabunge wa Waziri wa fedha John Mbadi, ambaye ameshikilia kuwa mfumo huo lazima utekelezwe. Akiwa mbele ya kamati ya utekelezaji wa katiba katika bunge la kitaifa, Waziri Mbadi ameutetea mfumo huo anaosema utahakikisha uwazi katika […]

MGOMO WA WAHADHIRI WANG’ATA VYUO VIKUU

Athari za mgomo wa wahadhiri zimeanza kujitokeza kwa siku ya 3 sasa, wanafunzi wakikosa kuanza masomo yao kwa muhula huu jinsi walivyokuwa wametarajia huku wahadhiri wakishikilia kuwa hawatarejea kazini hadi malalamishi yao yashughulikiwe. Wahadhiri wanashinikiza kutekelezwa kwa makubaliano yao na serikali, kwenye mkataba wa mwaka 2021-25 waliotia Saini na serikali. Hata hivyo, Waziri wa elimu […]

WAKENYA KUPATA UMEME NAFUU KUPITIA MIPANGO YA NISHATI YA JOTOARDHI NA NUKLIA

Serikali kuu ina mpango wa kuweka megawati 53 za ziada za nishati ya mvuke kwenye gridi ya taifa ifikapo mwezi Juni 2026 kwa wastani wa gharama ya Ksh8.9 kwa kilowati-saa, na kuifanya kuwa chanzo cha tatu cha bei nafuu zaidi cha umeme baada ya umeme wa maji na unaogizwa kutoka taifa jirani la Ethiopia. Uwezo wa ziada utatokana na upanuzi wa […]