ITALIA KUKOSA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA 3?

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Italia Gennaro Gattuso amethibitisha kwamba wachezaji Gianluca Scamacca na Giacomo Raspadori wataanza mechi ya timu hiyo dhidi ya Moldova leo usiku, ila akasema anahisi kuwa mfumo wa kufuzu kwa kombe la dunia kwa bara Ulaya unahitaji mabadiliko. Mechi hiyo itaanza saa 22:45 usiku, na ushindi kwa […]

SUPER EAGLES WASITISHA MGOMO,WAREJELEA MAZOEZI

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Super Eagles, wamesitisha mgomo wao kuhusu malipo ya marupurupu na kurejelea mazoezi baada ya mzozo wa marupurupu hayo kuripotiwa kutatuliwa. Super Eagles wanajiandaa kwa pambano la mwondoano dhidi ya Gabon hii leo nchini Morocco, katika kipute cha timu 4 zinazowinda tiketi ya kushiriki kombe la dunia […]

KPA YAWAKA MOTO WA VIKAPU

Klabu ya mchezo wa vikapu KPA imeendeleza msururu wake wa matokeo bora katika dimba la Ligi ya wanawake barani Afrika mwaka huu toleo la FIBA Zone 5, ikiwabebesha Gladiators wa Burundi vikapu 100-42 katika pambano lao la 3 kwenye Pool A ugani Nyayo. Wanabandari hao ambao hajawapoteza mikononi mwa timu yoyote katika dimba hilo, walitawala […]

PROF. OKOWA ACHAGULIWA JAJI ICJ

Kenya imepiga hatua kubwa kwenye ngazi ya haki ya kimataifa baada ya Profesa Phoebe Okowa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa kuwa jaji katika mahakama ya kimataifa kuhusu haki ICJ. Profesa Okowa ambaye tayari ni mwanachama wa tume ya sheria ya kimataifa, amechaguliwa katika kura za baraza kuu la umoja wa mataifa UN na baraza la […]

RUTO AMWOMBOLEZA MBUNGE WA ISIOLO SOUTH

Risala za rambi rambi zimeendelea kutolewa kuhusiana na kifo cha mbunge wa Isiolo South Tubi Bidu, aliyefariki hapo jana katika Nairobi Hospital alikokuwa akipokea matibabu. Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii X, Rais William Ruto amemtaja Bidu kama mtumishi wa umma aliyejitolea kupigania elimu, aliyeamini katika kuimarisha jamii kupitia ujuzi na fursa. Mbunge huyo […]

KENYA YAPUZILIA MBALI VITISHO VYA MUSEVENI

Wizara ya masuala ya kigeni nchini imepuzilia mbali vitisho vya rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusu nia yake ya kuinyakua bandari ya Mombasa na Bahari Hindi katika eneo la Kenya, ikisema Museveni ana ufahamu kuhusu sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya mataifa. Akijibu maswali ya wanahabari, katibu mkuu katika wizara hiyo Korir Sing’oei, ameshikilia kuwa […]

WAKENYA 3 WAZUILIWA TANZANIA, MUDAVADI

Serikali imethibitisha kwamba raia wake walinaswa katika machafuko ya uchaguzi nchini Tanzania, wakenya 3 ambao ni Samuel Kagila, Stephen Ndung’u na George Odhiambo wakiwa bado mikononi mwa polisi huku wenzao 8 wakiachiwa huru bila mashtaka. Katika taarifa, Waziri wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi, amesema kuwa Albert Kamala na mwalimu John Ogutu waliuawa nchini humo, […]

WANAHARAKATI BOB, OYOO WASIMULIA MATESO

Hofu kwamba tungewachochea vijana wa kizazi cha Gen Z nchini Uganda ndicho chanzo chetu sisi kutekwa nyara na kuzuiliwa kwa siku 38 katika kambi ya kijeshi ya Kasenyi nchini humo. Ndiyo kauli ya wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo, wakisimulia masaibu waliyopitia mikononi mwa kikosi maalum cha jeshi la taifa hilo. Wamefichua kuwa zaidi ya […]

RUTO: NITAKOMBOA UKAMBANI KUTOKA UPINZANI

Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Ukambani iniangia siku ya 2 hii leo huku rais akitoa wito kwa eneo hilo kushirikiana naye kwenye uchaguzi mkuu ujao, akisema eneo hilo limekuwa kwenye upinzani kwa muda mrefu. Alikuwa akizungumza kwenye kaunti ya Makueni alikoanzia ziara yake hapo jana, akitumia ziara hiyo kutetea ushuru unaotozwa wakenya […]

CRISTIANO RONALDO KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA BAADA YA KOMBE LA DUNIA

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amethibitishakuwa Kombe la Dunia la mwaka 2026 litakuwa ni mwisho wa safariyake ndefu na yenye mafanikio katika soka la kimataifa.Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye amefungajumla ya magoli 953 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa, amesemaanapanga kustaafu soka la kulipwa ndani ya […]