BAYERN NA MAN UNITED WANG’ARA USIKU WA LIGI YA MABINGWAYA WANAWAKE

Klabu ya Bayern Munich ilipindua matokeo kwa kishindo baada yakutoka nyuma kwa mabao mawili na kuishinda Arsenal mabao 3–2katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake usiku waJumatano. Arsenal walionekana kuwa na udhibiti kamili wa mchezo kupitia baola kichwa la mapema la Emily Fox na shuti kali la Mariona Caldenteydakika ya 23, lakini Bayern walipambana […]

TUCHEL AMPA ONYO BELLINGHAM KUHUSU NAFASI YAKE KATIKAKIKOSI CHA ENGLAND

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Thomas Tuchel, amemuonyakiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham, kwamba atapaswakupigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Uingerezakuelekea Kombe la Dunia.Bellingham amerudi kwenye kikosi cha Tuchel kwa michezo yamwisho ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Albania wiki hii,baada ya kukosa mwito mwezi Oktoba kutokana na […]

KPA YANG’ARA KWENYE MASHINDANO YA FIBA ZONE FIVE WBLA2025

Kocha mkuu wa Kenya Ports Authority (KPA), Anthony Ojukwu,amesema hatima ya timu hiyo katika mashindano ya kufuzu kwa FIBAZone Five Women’s Basketball League Africa (WBLA) 2025 imomikononi mwao, huku akiwataka wachezaji wake kutochukulia mechiyoyote kwa urahisi.Timu hiyo ya Mombasa, ambayo ilinyakua nishani ya fedha mwaka2023, imeanza kampeni zake kwa nguvu katika Ukumbi wa NyayoGymnasium. KPA […]

KOCHA WA SHABANA FC AJIUNGA NA TIMU YA TAIFA YA U-17

Kocha mkuu wa Shabana FC, Peter Okidi, ameonyesha imani kamilikwa msaidizi wake Bernard Mwalala, atakayesimamia timu hiyowakati yeye akiungana na timu ya taifa ya wanafunzi wa chini yamiaka 17, Junior Stars, kwa mashindano ya kufuzu AFCON U17 mwaka2026 yatakayofanyika nchini Ethiopia.Okidi atahudumu kama kocha msaidizi wa William Muluya waKariobangi Sharks katika mashindano hayo ya kanda […]

BUNGE LA SIAYA LAPITISHA MSWADA WA KUWALINDA WAJANE

Juhudi za kuimarisha haki za wajane katika kaunti ya Siaya zimepigwa jeki baada ya bunge la kaunti hiyo kupitisha kwa kauli moja mswada wa kuwalinda wajane dhidi ya kudhulumiwa ikiwemo kurithiwa kwa lazima na jamaa za mumewe. Usajili wa wajane umeratibiwa kuanza baada ya gavana James Orengo kutia Saini mswada huo kuwa sheria. Imetayarishwa na […]

KANJA AKATA RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA KUZUIA USAJILI

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amewasilisha rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu kusitisha kwa muda zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na idara ya polisi, akitaka amri hiyo ifutiliwe mbali. Kwenye ombi lake, Kanja ametaja usitishwaji huo kuwa hatari, ikizingatiwa kuwa idara ya polisi inalenga kuimarisha usalama, akiitaka mahakama kuzingatia sheria inayoitaka idara […]

VIONGOZI, MATAIFA YAPONGEZA UCHAGUZI WA PROF. OKOWA

Uchaguzi wa Prof. Phoebe Okowa kuhudumu kama jaji wa mahakama ya kimataifa kuhusu haki ICJ umeendelea kupongezwa na viongozi na nchi mbali mbali, akiwa ni mwanamke wa kwanza kutoka Kenya kuchaguliwa kwenye wadhifa huo. Wa hivi punde ni mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, katibu katika wizara ya masuala […]

MAHAKAMA YARUHUSU UTEUZI WA BODI YA UAJIRI BUNGOMA

Bodi ya uajiri wa umma katika kaunti ya Bungoma imepata afueni baada ya mahakama ya ajira na leba mjini Bungoma kutupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa kupinga uteuzi wa wanachama kuhudumu kwenye bodi hiyo. Kwenye uamuzi katika kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa Rodgers Siboe ambaye hakuorodheshwa baada ya kutuma maombi, jaji David Nderitu ameamuru kuwa mwanasiasa huyo […]

OGAMBA AKANA MADAI YA KUTOLEWA KSH1.1B KWA SHULE HEWA

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amepuuzilia mbali madai kwamba serikali ilitoa Ksh1.1 bilioni kwa shule hewa. Kulingana na ripoti ogamba amefafanua kuwa matamshi yake Bungeni yalitafsiriwa vibaya, akieleza kuwa pesa hizo hazijatolewa kwa sababu takriban shule 990 zilikosa kuwasilisha data inayohitajika ili kuthibitishwa. Kufuatia hali hiyo, Wizara ilitoa asilimia 50 tu ya shule kwa baadhi […]

SERIKALI KUDHIBITI UAGIZAJI WA SIMU “KUU KUU”

Serikali inapanga kupiga marufuku uingizaji wa vifaa vya kielektroniki vya zaidi ya miaka 12, vikiwemo TV, friji, simu za kisasa, kompyuta, na vifaa vingine vya nyumbani na viwandani, katika hatua ya kuzuia utupaji taka wa kielektroniki. Rasimu ya kanuni hizo, iliyopendekezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA), inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya sumu zinazohusishwa […]