COURTOIS NJE KATIKA MECHI YA KUFUZU

Huenda Ubelgiji ikakosa huduma za kipa wake Thibaut Courtois katika mechi yake ya kufuzu dimba la kombe la dunia dhidi ta Kazakhstan na Liechtenstein baada ya kupata jeraha la msuli wa mguu alipokuwa akiichezea klabu yake ya Real Madrid. Kulingana na kalbu hiyo, Courtois mwenye umri wa miaka 33, alipata jeraha hilo kwenye mechi iliyoishia […]

MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA WIKI HII

Mechi za mwondoano wa timu za shirikisho la soka barani Afrika CAF zimeratibiwa kuanza Alhamisi wiki hii, timu hizo zikiwania nafasi moja ya kumenyana na mataifa kutoka mabara mengine ili kupata nafasi ya kufuzu kombe la dunia mwaka ujao. Mataifa ya Cameroon, Gabon, Nigeria na DR Congo yatamenyana kupata mwakilishi wa kushiriki mwondoano wa mabara […]

SOFAPAKA WACHANA BARUA ZA POSTA

Klabu ya Sofapaka ilipata ushindi muhimu wa ligi kwa kuicharaza Posta Rangers mabao 2-0 hapo jana kwenye uwanja wa Dandora jijini Nairobi. Wachezaji Daniel Nganga na Josesph Kuloba, waliwafungia Batoto ba Mungu mabao hayo muhimu na kuwapa pointi 3 ambazo zinawaweka katika nafasi ya 7 kwa pointi 11, 5 nyuma ya vigogo Gor Mahia kwenye […]

WALIMU WAKUBALI KUINGIA SHA

Mvutano kati ya serikali na walimu kuhusu bima yao ya matibabu umefikia kikomo baada ya walimu kukubali kuhamia bima ya afya ya jamii SHA kutoka kwa ile ya kibinafsi ambayo mkataba wao unakamilika mwishoni mwa mwezi huu. Uamuzi huo umeafikiwa kufuatia misururu ya mikutano, kaimu afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuwaajiri walimu TSC Eveline […]

WAKENYA WAONYWA DHIDI YA SIASA UGENINI

Serikali imewaonya wakenya dhidi ya kujihusisha na siasa za mataifa mengine, ikisema mwenendo huo unaweza ukawa hatari. Katika kikao cha kiteknolojia na vijana jijini Eldoret, Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amesema kumeshuhudiwa ongezeko la wakenya wanaojipata katika hali tatanishi, wakihitaji msaada wa serikali katika mataifa ya kigeni. Aidha, amewatahadharisha vijana dhidi ya kuishambulia serikali. Imetayarishwa […]

MAHAKAMA YATIA PINGU USAJILI WA POLISI

Vijana wanaolenga kujiunga na idara ya polisi wamepata pigo kwa mara nyingine tena baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuzuia kwa muda zoezi la usajili lililokuwa limeratibiwa kufanya tarehe 17 mwezi huu. Kwenye uamuzi katika kesi iliyowasilishwa na mkenya kwa jina Eliud Matindi, jaji Bahati Mwamuye ameamuru kwamba zoezi hilo lisitishwe hadi kesi hiyo […]

KEPSHA YAWAKWAMIA WALIMU WA JSS

Muungano wa walimu wakuu wa shule za msingi KEPSHA umepinga pendekezo la walimu wa sekondari msingi JSS kuhamishiwa chini ya usimamizi wa shule za upili, ukiwataka walimu hao kuepusha siasa za miungano ya walimu kwenye uendeshaji wa shule. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano huo Fuad Ali, uamuzi wa JSS kuwa chini ya shule za […]

KESI YA MVUVI NAKURU KUENDELEA

Kesi kuhusu mauaji ya Mvuvi Brian Odhiambo aliyetoweka mapema mwaka huu katika mbuga ya wanyama ya Lake Nakuru itaendelea hii leo baada ya kurejelewa hapo jana, shahidi mmoja zaidi akiratibiwa kutoa ushahidi wake hii leo. Kesi hiyo inawajumuisha maafisa 6 wa idara ya wanayamapori, wanaohusishwa na kutoweka kwa mvuvi huyo. Hapo jana, mashahidi waliambia mahakama […]

Mastering European Roulette and Bonus Play at Ice36

Mastering European Roulette and Bonus Play at Ice36 European roulette offers players a better chance to win than the American version found in many Vegas casinos. When you combine those odds with powerful promotions, the result can be a very rewarding online experience. In this guide we’ll break down why the European wheel is smarter, […]

VIONGOZI WAMEWAHIMIZA WAKAAZI WA KASIPUL KUDUMISHA AMANI WAKATI HUU WA UCHAGUZI MDOGO

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wamewahimiza wananchi kudumisha  amani na maridhiano wakati wa kampeni za uchaguzi ndogo katika eneo bunge la kasipul kaunti ya Homa Bay. Haya yanajiri baada ya makabiliano yaliyoshuhudiwa katika eneo la Opondo ambapo vijana wawili waliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa Hata hivyo mwenyekiti wa chama cha ODM Gladys Wanga amekashifu kitendo hicho akiwataka wakaazi kudumisha […]