BEN WHITE AITWA TIMU YA UINGEREZA

Mlinzi wa Arsenal, Ben White, ametajwa katika kikosi cha uingereza kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka mitatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hajahusiana na timu tangu alipoondoka kambi ya Kombe la Dunia 2022 Qatar kwa sababu binafsi, na baadaye kujitokeza kuwa hafai kuchaguliwa chini ya kocha Gareth Southgate. Uingereza itacheza mechi za kirafiki dhidi […]

LUANDA VILLA WAFUFUKA CHINI YA SALEH

Luanda Villa wanaonyesha dalili za kurejea katika kiwango kizuri kufuatia kurejea kwa kocha mkuu Leonard Saleh, huku wakipata ushindi wa mechi mbili mfululizo na kuongeza matumaini ya kuepuka kushuka daraja katika Ligi ya Kitaifa. Saleh, aliyerejea klabuni hivi karibuni baada ya kuondoka Januari kutokana na kutotekelezwa kwa ahadi na kumalizika kwa mkataba wake, ameiongoza timu […]

MWANGI ALENGA KIATU CHA DHAHABU NSL

Mshambuliaji wa Fortune Sacco, Collins Mwangi, ameweka malengo ya kumaliza msimu kama mfungaji bora katika Ligi ya Kitaifa huku akiendelea kung’ara mbele ya lango. Kwa sasa Mwangi yuko nafasi ya pili akiwa na mabao 14, mabao matatu nyuma ya kinara Syphas Otieno mwenye mabao 17, huku Vincent Nyabuto akishika nafasi ya tatu kwa mabao 13. […]

TUSKER YAJITOA MBIO ZA UBINGWA WA LIGI

Kocha mkuu wa Tusker FC, Julien Mette, amekiri kuwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu hazipo tena mikononi mwao, akiwataka wachezaji kuhamisha nguvu zao kwenye mashindano ya Kombe la FKF. Timu hiyo, iliyotwaa ubingwa mara 13, itakabiliana na Kariobangi Sharks katika hatua ya 16 bora, huku ikiwa nafasi ya saba kwenye jedwali la ligi ikiwa […]

KNH YATOA NOTISI KUHUSU MIILI ISIYODAIWA

Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta imetoa tangazo kwa umma ikizitaka familia kudai miili 480 iliyopo katika hifadhi yake, ikionya kuwa itazikwa ndani ya siku saba iwapo haitatambuliwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa hii leo, miili hiyo inajumuisha watu wazima 102 na watoto 378, jambo linaloonyesha uzito wa hali hiyo. Uongozi wa hospitali hiyo umetoa wito kwa jamaa na walezi […]

VIONGOZI WA PWANI WATAKA JOHO KUWA NAIBU RAIS 2027

Baadhi ya wanachama wa chama cha ODM kutoka eneo la Pwani wanaendeleza kampeni za kumtaka Waziri wa Madini, Hassan Joho, kuwa Naibu Rais mwaka 2027. Wakiongozwa na Naibu Kiongozi wa chama na Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir, pamoja na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro,viongozi hao wameonyesha  imani kuwa chama kitashinda nafasi zote za uongozi. Nassir amesema […]

MAGAVANA WATAKA ONGEZEKO LA MGAO WA KAUNTI

Baraza la Magavana limetaka mgao wa shilingi bilioni 534 katika mwaka ujao wa kifedha, likisema kaunti zinahitaji fedha zaidi kulipa wafanyakazi na kutekeleza majukumu yao. Mwenyekiti wa baraza hilo, Ahmed Abdulahi, ameeleza kuwa mahitaji ya kaunti yameongezeka na yanahitaji kuzingatiwa katika upangaji wa bajeti. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Rasilimali, Mary Chebukati, […]

RUTO AZURU NYANZA AKARIBISHWA NA ORENGO

Rais William Ruto amezuru kaunti za Siaya na Migori leo katika mwendelezo wa ziara yake eneo la Nyanza huku akikaribishwa na Gavana wa Siaya James Orengo hata baada ya mvutano wa kisiasa unaoshuhudiwa. Rais anaendelea na mikutano yake na wananchi akielezea ajenda ya maendeleo katika maeneo hayo huku akiendelea kupigia debe miradi ya serikali yake akisisitiza umuhimu […]

KENYA YATEKA MASOKO YA KIMATAIFA KUPITIA UZALISHAJI WA AINA MPYA YA MAUA

Kenya imeendelea kukumbatia aina mpya ya uzalishaji wa maua, hatua inayopanua zaidi masoko ya kimataifa kwa taifa hili linalochukua nafasi ya nne bora duniani katika uuzaji nje wa maua yaliyokatwa na ya mapambo. Kulingana na ripoti ya Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Maua nchini Clement Tulezi, katika miaka ya hivi karibuni wakulima wa maua wameongeza uzalishaji wa maua aina ya waridi na […]

MASAI ALENGA KUJIKOMBOA KATIKA PARIS MARATHON

Bingwa wa mbio za Toronto Marathon mwa ka 2019 Magdalyne Masai atalenga kuimarisha msimu wajke katika mashindano ya Paris Marathon itakayoandaliwa tarehe 12 baada ya kuanza mwaka vibaya. Masai mwenye umri wa miaka 32, alianza kampeni yake tarehe 15 mwezi jana katika mashindano ya Barcelona Half Marathon, ambako alimaliza katika nafasi ya 5 kwa muda […]