RUTO AONGOZA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NAIROBI

Rais William Ruto pamoja na Rais wa Msumbiji Daniel Chapo wameongoza kongamano la uwekezaji katika hoteli moja hapa jijini Nairobi. Zaidi ya kampuni 20 zimekubali kuwekeza zaidi ya dola bilioni 2.9 katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo afya, kilimo na madini, huku kaunti kama Kilifi, Nairobi, Tana River na Kitui zikitajwa kunufaika. Rais Ruto ametumia fursa hiyo kuwashukuru […]

KRA YAPENDEKEZA USAJILI WA LAZIMA WA VAT KWA BIASHARA ZOTE

Mamlaka ya kukusanya Ushuru nchini (KRA) imependekeza mageuzi makubwa ya ushuru ambayo yatafanya kuwa lazima kwa biashara zote, bila kujali ukubwa, kusajiliwa kama mawakala wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Hatua hiyo, ikiwa itapitishwa, itaondoa kiwango cha sasa cha mauzo ya kila mwaka cha Ksh5 milioni kwa usajili wa VAT, na kuwafanya wafanyabiashara wadogo wadogo kulipa ushuru kwa mara ya […]

SALAH KUIAGA LIVERPOOL MWISHONI MWA MSIMU

Mshambulizi wa klabu ya Liverpool Mohammed Salah, ametangaza kwamba ataondoka kwenye klabu hiyo ya Uingereza mwishoni mwa msimu huu, huku akiishukuru kwa kumpa alichokitaja kuwa wakati mwafaka zaidi wa maisha yake. Liverpool imesema tayari wamekubaliana kuachana na Salah ambaye amewajibikia klabu hiyo kwa miaka 9, na ataondoka kama mchezaji huru. Mkataba wake aliotia saini Aprili […]

KENYA KUWA MWENYEJI WA FIFA SERIES APRILI

Kenya itakuwa mwenyeji wa mojawapo ya makala ya FIFA Series kitengo cha wanawake, yatakayoandaliwa nchini mwezi ujao. Mashindano hayo yatajumuisha wenyeji Harambee Starlets, Australia, Malawi na India. Kenya itashuka dimbani katika mechi ya pili dhidi ya India baada ya Malawi kumenyana na Australia, mechi zote zikiratibiwa kuchezwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi. Kulingana na […]

MABADILIKO YA DAKIKA ZA MWISHI KIKOSINI HARAMBEE STARS

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanaume Harambee Stars, Benni McCarthy, amelazimika kukifanyia mageuzi kikosi chake dakika za mwisho kutokana na majeraha kwa takribani wachezaji 10 akiwemo nahodha Michael Olunga. Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda lango Brian Omondi, mabeki Eric Ouma, Joseph Okumu, Sylvester Owino na Collins Sichenje. Aidha, Tylor Onyango, […]

KABURI LA PAMOJA: UCHUNGUZI HURU WASHINIKIZWA

Shinikizo zimeendelea kutolewa kwa taasisi huru kama vile mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi, IPOA, na tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu kuendesha uchunguzi huru ili kubaini iwapo kuna nia fiche kuhusiana na miili 32 iliyozikwa kwenye kaburi la pamoja katika kaunti ya Kericho. Kulingana na wanaharakati ambao wamekita kambi eneo hilo, utata huo […]

KUFAA KUFAANA: WANASIASA ‘WASIMAMA’ NA TUJU

Utata wa umiliki wa mali unaomkabili Waziri wa zamani Raphael Tuju umechukua mkondo wa kisiasa, viongozi kutokana mrengo wa upinzani na ule wa serikali wakionekana kutumia suala hilo kwa manufaa yao ya kisiasa. Akizungumza kwenye siku ya mwisho ya ziara yake eneo la Nyanza, Rais William Ruto amehusisha masaibu ya Tuju na viongozi wa upinzani […]

KWS YAKANA KUHUSIKA NA KUTOWEKA KWA MVUVI

Shirika la kutoa hifadhi kwa wanyamapori nchini, KWS, limeendelea kujitenga na madai ya kuhusika katika kutoweka kwa mvuvi Brian Odhiambo katika mbuga ya Lake Nakuru mwanzoni mwa mwaka jana. Akiwa mbele ya kamati ya seneti kuhusu usalama, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Erastus Kanga, ameiambia kamati hiyo kwamba Odhiambo, anayedaiwa kukamatwa na maafisa wa KWS, […]

UPASUAJI WA MIILI YA KERICHO KUFANYWA

Zoezi la upasuaji wa miili 32 iliyofukuliwa kutoka kaburi la pamoja kwenye kaunti ya Kericho hapo jana linatarajiwa kuanza muda wowote ili kubaini chanzo cha vifo vya waathiriwa hao wasiojulikana, huku ikiibuka kuwa huenda miili hiyo ilisafirishwa kutoka hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyamira. Kulingana na mwanapatholojia wa serikali Dakta Richard Njoroge, miili 7 […]

VIJANA WALIOSAJILIWA NI WACHACHE BADO, IEBC

Jumla ya wapiga kura wapya 250,391 wamesajiliwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, tangu kuanzishwa kwa zoezi hilo la kitaifa Septemba mwaka jana. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, kamishna wa IEBC Alutalala Mukhwana, amefichua kwamba asilimia kubwa ya waliosajiliwa inatoka katika maeneo ya mijini, kaunti ya Nairobi ikiongoza na kufuatiwa na […]