KENYA YAJIUNGA NA MPANGO WA KIMATAIFA WA AFYA

Katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga, Kenya imetangaza kujiunga na mpango wa kimataifa wa afya kwa muda wa miaka 5, mpango utakaogharimu kima cha shilingi bilioni 11. Kulingana na mkurugenzi mkuu wa idara ya afya Daktari Patrick Amoth, mpango huo utatekelezwa katika kaunti 12 ambazo huchangia asilimia 50 ya vifo hivyo, akisema kaunti […]

MAHAKAMA YATOA AGIZO KWA POLISI KUHUSU BUNDUKI

Idara ya polisi imepewa makataa ya siku 90 kubuni mwongozo kuhusu matumizi ya bunduki miongoni mwa maafisa wake, ili kudhibiti visa ambapo baadhi ya maafisa hao wamekuwa wakitumia visivyo bunduki zao na kusababisha vifo vya raia. Kwenye uamuzi wake alipoagiza fidia ya shilingi milioni 38.6 kwa waathiriwa 28 waliodhulumiwa na polisi wakati wa maandamano ya […]

GACHAGUA ATETEA MSIMAMO WA HISA, AKISEMA ODM WAMEIGA

Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, ametetea msimamo wake wa kupigania hisa za eneo la Mlima Kenya serikalini, akisema msimamo sawa umechukuliwa na chama cha ODM kinapopanga ushirikiano wa kisiasa na UDA. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini, Gachagua ambaye pia ni kinara wa chama cha DCP, amesisitiza kwamba kila upande kwenye ushirikiano huo […]

MSIHOFU KUHUSU MAFUTA, SERIKALI

Serikali imewahakikishia wakenya kwamba kuna hifadhi ya kutosha ya mafuta nchini licha ya kufungwa kwa eneo la bahari la usafirishaji wa mafuta la Hormuz katika eneo la Mashariki ya Kati, ikisema taifa lina akiba ya kutosha ya mafuta. Kwa mujibu wa Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, wananchi hawana sababu ya kuwa na wasiwasi na kwamba […]

SHUJAA WAJIPANGA MASHINDANO BRAZIL

Timu za taifa za raga ya wachezaji saba kwa upande wa wanaume na wanawake zinajiandaa kwa wikendi muhimu nchini Brazil, ambapo hatua ya mwisho ya mashindano ya daraja la pili itafanyika São Paulo kuanzia Machi 28 hadi 29 Kwa matumaini ya kupanda daraja, Shujaa na Kenya Lionesses wanaingia mashindano wakiwa na kila sababu ya kupigania […]

ULINZI STARS WAPIGA HATUA DHIDI YA KUSHUKA DARAJA

Ulinzi Stars wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupambana na kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nairobi United katika mechi ya Ligi Kuu ya msimu wa 2025/2026. Ingawa ushindi huo umepunguza presha ya haraka, timu hiyo bado iko kwenye vita vikali vya kusalia ligini, huku timu tatu za mwisho zikikumbwa na hatari […]

AROKO ALENGA KUOKOA KARIOBANGI SHARKS

Mshambuliaji chipukizi wa Kariobangi Sharks, Humphrey Aroko, amesema lengo lake kuu ni kusaidia timu hiyo kuepuka kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Kenya. Aroko alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari baada ya kuonyesha kiwango bora na kufikisha mabao 12 hadi sasa msimu huu. Hata hivyo, amesema mafanikio hayo binafsi si muhimu sana kulinganisha […]

NATEMBEYA AITAKA SERIKALI KUSAIDIA WAKULIMA

Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ameitaka serikali ya kitaifa kushirikiana na kaunti kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa bei nafuu ili kuimarisha sekta ya kilimo. Akizungumza katika wadi ya Hospital wakati wa hafla ya kugawa mbegu kwa zaidi ya wakulima elfu kumi, Natembeya amesema serikali yake imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wakazi laki tatu […]

VIFO VYA MAFURIKO VYAFIKIA 88

Idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini imefikia watu 88. Kwa mujibu wa taarifa ya Huduma ya Polisi ambayo imetolewa hii leo, maelfu ya familia pia wameathiriwa huku miundombinu muhimu ikiharibiwa vibaya katika maeneo mbalimbali. Zaidi ya familia 2,690 zimelazimika kuyahama makazi yao na kwa sasa zinaishi katika vituo vya muda huku mvua […]

MAGEUZI YA POLISI YAFIKIA ASILIMIA 55

Katibu Mkuu wa Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, amesema Kenya imefikia utekelezaji wa asilimia 55 ya mageuzi ya polisi yanayoendelea nchini kufuatia mkutano wa ngazi ya juu wa kamati ya usalama wa taifa. Mageuzi hayo, yaliyoanzishwa kwa maelekezo ya rais, yanalenga kuimarisha taasisi za usalama, kuboresha utoaji huduma na kuboresha mifumo ya kipolisi kote nchini. […]