UPINZANI WATAKA MSWADA WA FEDHA 2026 UKATALIWE

Vyama vya upinzani vya Jubilee na DCP vimewataka Wakenya kuupinga kikamilifu Mswada wa Fedha wa mwaka 2026 wakidai unalenga kurejesha ushuru unaowaumiza wananchi wa kipato cha chini na cha kati. Viongozi wa vyama hivyo pia wanataka EPRA kuweka wazi mfumo unaotumika kupanga bei ya mafuta nchini huku wakiwasuta viongozi wa sekta ya uchukuzi kwa makubaliano yao na serikali. […]

BUNGE LAKUBALI MAPENDEKEZO YA NDINDI NYORO KUHUSU MAFUTA

Bunge la Taifa limekubali kuyazingatia mapendekezo ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro yanayolenga kupunguza bei ya mafuta nchini. Kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Bajeti ya Bunge, Bunge limethibitisha kupokea barua ya Nyoro ya Mei 15 yenye mapendekezo ya marekebisho ya sheria yanayolenga kupunguza gharama ya dizeli kwa angalau shilingi 54 kwa lita. Hatua hiyo imejiri […]

KINDIKI ATAKA UWIANO KATI YA GHARAMA YA MAFUTA NA MAENDELEO

Naibu Rais Kithure Kindiki amewataka Wakenya kuwa na uwiano kati ya matakwa ya kupunguzwa kwa bei ya mafuta na mahitaji ya kuendesha serikali pamoja na kufadhili miradi ya maendeleo. Akizungumza katika hafla tofauti jijini Nairobi na Machakos Kindiki amesema serikali inaendelea kufanya kazi usiku na mchana kudhibiti gharama ya bidhaa hiyo muhimu. Kauli hiyo imejiri […]

RUTO KUREJEA NCHINI LEO

Rais William Ruto anatarajiwa kurejea nchini hii leo huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wakenya kuhusu swala ya bei ya Mafuta. Ruto anatarajiwa kufanya mazungumzo na washikadau katika sekta ya uchukuzi kuhusiana na kupunguza bei ya mafuta baada ya sekta hiyo kusitisha mgomo kwa wiki moja ili kufungua njia ya mazungumzo. Wakenya sasa wanasubiri […]

JUBILEE YAMTETEA UHURU KENYATTA KUHUSIANA NA MAANDAMANO

Chama cha Jubilee kimekosoa matamshi ya viongozi wa UDA kwa madai ya kumhusisha rais mstaafu Uhuru Kenyatta na maandamano ya kupinga bei ya mafuta nchini. Chama hicho kimetaka heshima itolewe kwa rais huyo mstaafu huku kikisisitiza kuwa siasa za lawama hazitasaidia taifa. Naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i amesema viongozi wanapaswa kuacha kulaumiana na badala yake kujikita katika masuala […]

SHINIKIZO ZAONGEZEKA KUHUSU MGOMO WA MATATU

Muda wa kusitishwa kwa mgomo wa sekta ya matatu kwa wiki moja unaendelea kuyoyoma huku shinikizo zikiongezeka kwa serikali kutafuta suluhu ya kudumu kabla ya Jumanne ijayo. Makubaliano ya kusimamisha mgomo huo yalifikiwa kati ya serikali kupitia Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, Waziri wa kawi Opiyo Wandayi pamoja na wadau wa sekta ya uchukuzi. Hata hivyo, viongozi […]

MBADI AKOSOA WANAOPINGA MSWADA WA FEDHA

Waziri wa Fedha John Mbadi amemkosoa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i pamoja na viongozi wengine wa upinzani wanaotaka Mswada wa Fedha 2026 ukataliwe. Mbadi amesema viongozi wanaowataka Wakenya kupinga mswada huo wanapaswa kwanza kueleza vipengele wanavyopinga badala ya kutoa matamshi ya kisiasa ya jumla. Mbadi amesema ni makosa kuwahamasisha wananchi kuandamana dhidi […]

AISHA JUMWA AONDOLEWA KAMA MWENYEKITI WA BODI YA BARABARA NCHINI (KRB)

Mahakama Kuu imeondoa uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mawaziri Aisha Jumwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara za Kenya KRB, ikitoa uamuzi kwamba mchakato huo umekiuka Katiba na mahitaji ya kisheria. Kulingana na Jaji Mwamuy aliyetoa hukumu hiyo ni  kuwa uteuzi wa Jumwa umefanywa bila kuthibitishwa kufuata Kifungu cha 7 cha Sheria ya Bodi ya Barabara za Kenya […]

MAKAMISHNA WA NCIC WAAPISHWA RASMI NA KOOME

Hatimaye makamishna wapya walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu katika tume ya uwiano na utangamano kitaifa  NCIC wameapishwa. Rais wa idara ya mahakama nchini jaji mkuu  Martha Koome ameapisha makamishna hao katika shuguli iliyofanyika katika mjengo ya upeo wa mahakama hapa nchini. Makamishna hao wanaongozwa na mwenyekiti wao mpya  Daktari Kefa Nyamea Omae, ni Makamishna […]

KNEC YAITAKA UMMA KUWA MAKINI KUZUIA KUTAPELIWA

Baraza la Mitihani nchini  (KNEC) limekanusha habari zinazosambaa mitandaoni za kutoa matangazo ya mafunzo bandia  kuhusu tathmini za shule za upili, huku likiwataka  walimu na wanafunzi kuwa makini dhidi ya watapeli wanaotumia jina lake kuwalaghai wananchi.   Kupitia taarifa rasmi, KNEC imesisitiza kuwa haihusiki kwa njia yoyote na mafunzo hayo yanayotangazwa, na kwamba taasisi hiyo haiombi fedha kutoka kwa wadau kwa […]