VIJANA WAWILI WAUWAWA NA POLISI BUSIA

Shuguli za uchukuzi zimerejea  katika maeneo mbalimbali nchini baada ya wahuduma wa sekta za umma kusitisha mgomo wao uliokuwa umeathiri huduma  za usafiri na shuguli  za biashara. Huku haya yakijiri familia mbili katika kaunti ya Busia zinawaomboleza wanao wawili walioaga dunia hapo jana na maafisa wa polisi wakati wa madaandamano ya kupinga kuongezwa kwa bei […]

GUARDIOLA AMTAKIA ARSENAL BAADA YA UBINGWA WA EPL

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameipongeza Arsenal pamoja na kocha Mikel Arteta baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini uingereza Guardiola amesema Arsenal, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wanastahili ubingwa huo, akisisitiza kuwa wamefanya kazi kubwa msimu huu. Ameongeza kuwa ushindi wao ni wa haki kutokana na kiwango walichoonyesha katika msimu mzima. Imetayarishwa na Cyrus […]

ARSENAL WATWAA UBINGWA WA EPL BAADA YA MIAKA 22

Arsenal hatimaye wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kusubiri kwa miaka 22, kufuatia sare ya 1-1 baina ya Manchester City na Bournemouth. Matokeo hayo yamewafanya Arsenal kuhitimisha msimu wakiwa kileleni, na kukata ukame wa mataji uliodumu kwa miaka sita chini ya kocha Mikel Arteta. Timu hiyo imekuwa na msimu imara, ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu […]

JUNIOR STARLETS KUWAKABILI UGANDA KUTAFUTA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

Junior Starlets watakutana na timu ya akina dada ya Uganda ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Ijumaa katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mchujo wa kufuzu kombe la Dunia la akina dada wasiozidi miaka 17. Kocha Mildred Cheche ameendeleza kikosi kilichofanya vizuri dhidi ya Namibia, akifanya mabadiliko machache kutokana na majeraha. Beki Rose Nangila na Lindey Weey wamekosa […]

POLICE BULLETS YAPANGA KUIMARISHA KIKOSI KUELEKEA CECAFA

Mwenyekiti wa Kenya Police Bullets Munga Nyale ametaka kikosi hicho kuongezewa nguvu kuelekea michuano ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ukanda wa CECAFA. Police Bullets walitwaa taji lao la tatu mfululizo la Ligi Kuu ya Wanawake nchini baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Madira Soccer Assassins katika mechi […]

HARAMBEE STARS KUMENYANA NA AFRIKA KUSINI KUFUZU AFCON 2027

Safari ya kuelekea mashindano ya AFCON 2027 imeanza rasmi baada ya droo ya mechi za kufuzu kufanyika mjini Cairo ambapo Harambee Stars imepangwa Kundi D pamoja na Afrika Kusini, Guinea na Eritrea Ingawa Kenya tayari imefuzu moja kwa moja kama mwenyeji mwenza pamoja na Uganda na Tanzania, mechi hizo zitakuwa kipimo muhimu cha maandalizi ya timu hiyo. Kocha […]

AFYA YA UMMA NAIROBI YATAHADHARISHA MGOMO

Maafisa wa afya ya umma jijini Nairobi wameituhumu bodi ya huduma ya kaunti kwa kuajiri maafisa wasio na sifa kushughulikia usalama wa chakula na uthibitisho wa afya. Kupitia Chama cha Maafisa wa Afya ya Mazingira na Afya ya Umma, Katibu Mkuu wa chama Brown Ashira amesema hatua hiyo inakiuka sheria za afya ya umma na kanuni za usimamizi wa […]

NPS YAPINGA HABARI ZA KUKAMATWA KWA OCS WA NAIROBI CENTRAL

Huduma ya Kitaifa ya Polisi imekosoa taarifa zilizosambaa kuhusu kukamatwa kwa OCS wa Nairobi Central Dishen Ongoya, zikizitaja kama za upotoshaji. Katika taarifa yake, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga amesema madai hayo yaliyosambaa mitandaoni si ya kweli na hayapaswi kuaminika. Hata hivyo, taarifa hizo zimezua mjadala baada ya ripoti za awali kuashiria kuwa afisa huyo alikuwa […]

OMOLLO AKATAA WITO WA KUJIUZULU

Katibu mkuu katika Wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo amekataa wito wa baadhi ya viongozi wa upinzani wanaomtaka ajiuzulu, akisema hakuna msingi wa hatua hiyo. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja humu nchini, Omollo amesema madai hayo yanatokana na siasa na si ukweli wa mambo, akisisitiza kuwa anaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Wito wa kujiuzulu kwake […]

GACHAGUA AILAUMU SERIKALI KUCHOCHEA GHASIA NCHINI

Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ameisuta serikali kwa kuchochea hasira za wananchi kupitia namna inavyoshughulikia uchumi, sera za sekta ya usafiri na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Akizungumza akiwa nchini Uingereeza Gachagua alijibu kauli za Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar, aliyekuwa amehoji sababu za hasira za wananchi dhidi ya Rais William Ruto. Gachagua amesema viongozi wa […]