KENYA YAIMARISHA UKAGUZI WA EBOLA MPAKANI

Serikali ya Kenya imeimarisha uangalizi na ukaguzi katika mpaka wa Busia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo uliosababisha zaidi ya vifo 130. Serikali imetuma timu ya wahudumu wa afya kuwachunguza wasafiri wanaotoka ukanda wa Maziwa Makuu baada ya taarifa kuwa nchi jirani ya Uganda tayari imeripoti kifo kimoja kinachohusishwa na virusi […]

SERIKALI YATAKA HATUA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Huduma kwa Watoto imetoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukabiliana na ongezeko la ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto nchini. Waziri Hannah Cheptumo amesema Kenya ilirekodi visa 10,531 vya dhuluma dhidi ya watoto kati ya Januari mwaka jana na Machi mwaka huu. Amesema serikali na jamii lazima zishirikiane […]

MALI YAHARIBIWA WAKATI WA MAANDAMANO YA BEI YA MAFUTA

Mali ya thamani isiyojulikana imeharibiwa katika maeneo mbalimbali nchini baada ya wahuni kutumia maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta kuvamia na kupora biashara. Katika eneo la Naivasha, watu wawili walifariki baada ya polisi kufyatua risasi kwa kundi la watu waliokuwa wakivamia maduka na biashara. Huko Murang’a, benki na maduka ya jumla yalivunjwa huku […]

HUDUMA ZA USAFIRI ZAREJEA BAADA YA MGOMO KUSITISHWA

Ni afueni kwa wasafiri baada ya huduma za usafiri kurejea kote nchini kufuatia kusitishwa kwa mgomo wa kupinga ongezeko la bei ya mafuta. Magari ya uchukuzi wa umma yalianza tena kubeba abiria kuanzia Jumanne alasiri baada ya serikali na wadau wa sekta ya usafiri kufikia makubaliano ya kuendelea na mazungumzo kwa muda wa siku saba […]

KINDIKI ASIFIA SEKTA YA USAFIRI KUSITISHA MGOMO

Naibu Rais Kithure Kindiki ameisifu sekta ya usafiri wa umma kwa kuitikia wito wa serikali wa kusitisha mgomo wa kitaifa uliokuwa umepangwa. Kindiki amesema hatua hiyo imeleta afuweni kwa wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za usafiri katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha, Naibu Rais ameahidi kuwa serikali itaendelea kuchunguza njia zote zinazowezekana ili kupunguza gharama ya […]

RUTO AWASILI KAZAKHSTAN KWA ZIARA YA KISERIKALI

Rais William Ruto yupo nchini Kazakhstan kwa ziara ya siku mbili inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili. Ruto alipokelewa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Kazakhstan Yermek Kosherbayev. Ziara hiyo inalenga kupanua ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, usafirishaji na teknolojia. Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

GUARDIOLA AHOFIA UCHOVU KABLA YA FAINALI

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema ana matumaini kikosi chake kitaweza kushinda uchovu kinapoikabili Chelsea FC katika fainali ya Kombe la FA siku ya Jumamosi. Manchester City bado wanapambana kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal FC, lakini kwa sasa macho yao yataelekezwa Wembley wakisaka kutwaa taji la pili la nyumbani […]

AKONNOR ATAKA GOR MAHIA KUDUMISHA NIDHAMU NA UTULIVU KPL

Kocha mkuu wa Gor Mahia, Charles Akonnor, amewataka wachezaji wake kuwa watulivu, wenye nidhamu na kudhibiti presha kabla ya mechi dhidi ya Murang’a Seal Jumapili katika uwanja wa Nyayo. Mchezo huo ulihamishwa kutoka Murang’a hadi Nairobi kutokana na changamoto za miundombinu na maandalizi. Gor Mahia wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 65, saba mbele […]

KIPYEGON KUHAMIA MBIO NDEFU

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon amesema anaanza polepole kuhamia mbio ndefu baada ya kutawala mbio za mita 1500 kwa miaka kadhaa. Kipyegon ataanza msimu wake wa mwaka 2026 katika mbio za mita 5000 kwenye mashindano ya Diamond League yatakayofanyika mjini Keqiao nchini China siku ya Jumamosi. Akizungumza kabla ya mashindano hayo, Kipyegon alisema […]

NDINDI NYORO ATOA KAULI YAKE DHIDI YA KUPANDA KWA MAFUTA NCHINI

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema ongezeko la bei ya mafuta linaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa wananchi huku akitaka serikali kuweka mikakati ya haraka kupunguza gharama ya maisha kwa Wakenya walioathirika na kupanda kwa gharama za usafiri na bidhaa muhimu nchini Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari kuhusu suala la mafuta Mbunge huyo ameeleza kuwa […]