WAKENYA WATARAJIA BEI MPYA YA MAFUTA HUKU KUKIWA NA WASIWASI WA UHABA

Wakenya wanasubiri kwa hamu tathmini ya bei ya mafuta ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) hapo kesho kufuatia tatizo kubwa la mafuta lililofuatia ukaguzi wa Aprili, ambao ulisukuma bei ya pampu kurekodi kupanda na kusababisha uhaba wa mafuta  kote nchini, ununuzi wa hofu na kupanda kwa gharama za usafiri. Bei ya Super Petrol ilipanda kwa […]

GUARDIOLA: SIJAWAHI KUWA NA IMANI NA VAR

Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola, amesema hajawahi kuamini chochote katika marefa wa EPL na msaidizi wa refa kupitia video, VAR, akirejelea uamuzi wa kuipokonya West Ham United bao la kusawazisha dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita. Arsenal waliongeza pengo la pointi kati yao na City hadi 5 kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya […]

SOUTHAMPTON, HULL WEMBLEY KUWANIA NAFASI EPL

Klabu ya Southampton iliilaza Middlesbrough katika muda wa ziada ugani St. Mary’s kuweka miadi dhidi ya Hull City katika fainali ya mwondoano yaani playoff ya kuwania nafasi ya kupandishwa daraja kuelekea ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL. Mechi hiyo ya semi fainali ya mwondoano wa ligi ya Championship, ilitatuliwa katika dakika ya 116 ya […]

LEOPARDS, ULINZI KUKABILIANA KPL GOR IKISUBURI

Klabu ya AFC Leopards ina fursa ya kupunguza pengo la pointi kati yake na viongozi wa ligi kuu ya soka, KPL, Gor Mahia, itakapoialika Ulinzi Stars uwanjani Nyayo hii leo katika mechi ambayo huenda ikawa na usemi mkubwa kuhusu mwelekeo wa ligi hiyo. Sare ama kichapo kwa Ingwe itaifaidi Gor Mahia katika kinyang’anyiro cha kuwania […]

HALI TETE YA USALAMA BUNGOMA, BUSIA

Polisi katika kaunti za Busia na Bungoma wanachunguza matukio mawili yaliyohusisha mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 12 na afisa wa afya aliyeuawa nyumbani kwake katika eneo la Nambaya, viungani mwa mji wa Bungoma. Katika tukio la kwanza, polisi wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 33 kuhusiana na mauaji ya mwanawe katika eneo la […]

KIFURUSHI KIPYA CHA SHA KWA WAJAWAZITO

Wakenya hasa wagonjwa wa saratani na akina mama wajawazito wameratibiwa kupata manufaa zaidi chini ya kifurushi kipya kilichoboreshwa chini ya mamlaka ya afya ya jamii SHA. Chini ya kifurishi hicho kutokana na agizo la Rais William Ruto, fedha zinazotengewa wagonjwa hao zimeongezwa kutoka 500,000 hadi 800,000, huku akina mama wanaojifungua katika hospitali za level 2 […]

GACHAGUA AIBUA MADAI YA UFISADI KWENYE ZIARA YA MACRON

Ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini imeendelea kuibua hisia mseto, kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua akiibua madai kwamba ziara hiyo ilihusu mashauriano kuhusu malipo ya shilingi bilioni 7 kwa mashirika ya Ufaransa baada ya kandarasi zao za kujenga barabara kufutiliwa mbali. Kulingana na Gachagua, mashirika hayo yalipewa kandarasi ya kukarabati barabara […]

AFRIKA YAPITISHA AZIMIO KUJITEGEMEA KIFEDHA

Viongozi wa mataifa ya Afrika wamepitisha rasmi azimio la Nairobi wakati wa kongamano la Africa Forward, likieleza ajenda mpya ya bara hili inayolenga kujitegemea kifedha, ukuaji unaochochewa na teknolojia na viwanda vya kisasa. Azimio hilo lililoafikiwa baada ya majadiliano ya siku mbili ya kongamano la pamoja kati ya Kenya na Ufaransa, litashuhudia bara la Afrika […]

UCHAGUZI MDOGO: WAKAZI EMURUA DIKIIR WAHAKIKISHIWA USALAMA

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya chaguzi ndogo katika eneo bunge la Emurua Dikiir na wadi mbili katika kaunti za Samburu na Elgeyo Marakwet, mshirikishi wa eneo la bonde la ufa Abdi Hassan amewahakikishia wakazi wa Emurua Dikiir kwamba usalama wao umeimarishwa. Katika kikao na wanahabari baada ya mkutano na maafisa wa usalama, amesema wanashirikiana […]

SADIKI AWAVUTIA CHELSEA NA MANCHESTER UNITED

Kiungo wa Sunderland Noah Sadiki anadaiwa kuvutia vilabu vya Chelsea na Manchester United baada ya msimu mzuri wa kwanza nchini Uingereza. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema mambo yamebadilika kwa haraka tangu aondoke Union SG, lakini hakutaka kufunga mlango kuhusu uwezekano wa kufanya uhamisho mkubwa katika dirisha la kiangazi. Sadiki amesema kwa sasa […]